Dhana ya Kuinuana Kiuchumi baina ya Wanafamilia; Kuna haja unapompa ndugu yako Mtaji wa biashara umtoze riba ili kuongeza uwajibikaji?

Uzuri wake nimeshampa malengo na kuwaeleza Wazee ikiwa pamoja na kupokelea huo mtaji mbele yao kabisa.

Akishindwa this time hakutakuwa na mswalie mtume
 
kwanza hongera kwa juhudi zako....ndugu kumsaidia ni kazi sana,,,,..ndio maana kuna watu hiwa wanaamua kuhama nchi kabisa.....
Wakati mwingine tunakosea sisi kuwapa mitaji....ni vema kama kweli unataka kumsaidia...mjadiliane kwa kina ni mradi gani anataka kuanzisha,,,then wewe kama donor mshauri...ukubali kujitoa kwa muda pia...then anza nae kama …partnership,,,, wekeza kwa kadri mradi unavyosonga.....mtafika mahali wewe utaona amekomaaa...mwache asonge.....atasaidia na wengine....but kumpa just like give away ni mbaya sana....tunaona wengi wanafeli na wanarudi home....ukimuona daily home unaanza kujisikia vibaya........angalia waorombo.....mmoja anainua ukoo mzima wacha familia tuu...
 
Kwa upande wangu ndoano niliyodhani nawapa ilikuwa Mtaji, najua ingekuwa wako serious enough tungekuwa tumeshashinda adui umasikini kwa sehemu.

Nimegundua suala la kuvunja mnyororo wa Umasikini kwenye level ya familia zetu si lelemala
Gumu sana, ukiwapa wanakula bata kuliko wewe ulietafuta, ukiwamaindi mama anaingilia kati, unaogopa kumkwaza unakua mpole....somesha ndugu achana na kutoa hela hazifiki popote!
 
Very constructive idea, sikuifikiria hii Mkuu.

Nitaifanyia kazi hii idea, huenda hata zile Kampuni za Familia perhaps zilianza kwa namna hii.
 
Gumu sana, ukiwapa wanakula bata kuliko wewe ulietafuta, ukiwamaindi mama anaingilia kati, unaogopa kumkwaza unakua mpole....somesha ndugu achana na kutoa hela hazifiki popote!
Mtu mzima kumrudisha class kuna ugumu wake.

Next idea naifikiria ni kumshawishi akakope kwenye taasisi za fedha, akikumbana na stress za marejesho akili yake itamkaa vizuri
 
Very constructive idea, sikuifikiria hii Mkuu.

Nitaifanyia kazi hii idea, huenda hata zile Kampuni za Familia perhaps zilianza kwa namna hii.
utakuwa na wigo mpana wa kumdhibiti....najua mwanzo atakuona mnoko.....but hakika mtafaulu....mtasahau yote....atajifunza na kufundisha wengine....
 
utakuwa na wigo mpana wa kumdhibiti....najua mwanzo atakuona mnoko.....but hakika mtafaulu....mtasahau yote....atajifunza na kufundisha wengine....
Ubarikiwe Mkuu πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ™
 

Kwanza kabisa hongera kwa moyo wa kusaidia.

DDC Mlimani Park walikuwa na wimbo wao mmoja, baadhi ya mashairi ya ule wimbo yanasema.

"Usitumie peeesa, kama fimbo baba
Mambo ya pesa hutaka makubaliano, hapo ndipo pesa huwa na thamani eee".

Pesa inataka makubaliano kwanza, si kutoa tu ukifikiri itamaliza kila tatizo.

Mimi nilimkopesha ndugu mmoja (a cousin) mtaji miaka mitatu iliyopita, akapotea hakulipa. Hilo halikuwa tatizo kwangu, kwani nilivyompa hela sikutegemea zirudi.

Ikafikia wakati akapatwa na msiba namtafuta simpati, mpaka nikajiuliza, huyu anashindwa kupokea simu zangu za rambirambi kwa sababu anafikiri nitamkumbushia kumdai zile pesa ama vipi? Nilihuzunika sana.

Mwaka huu kanirudia tena ana matatizo, kanisihi sana, najua ana matatizo. Tangu kipindi cha huo msiba hajakaa sawa.

Nimemsaidia tena. Kwa kuwa naelewa matatizo yake. Safari hii nimemwambia nampa tu msaada, asiwe na pressure ya kunilipa pengine hata kuogopa kupokea simu.

Kikubwa ni kutaka kuelewa tatizo na kusaidia zaidi ya pesa tu.

Pesa unatuma muamala tu umemaliza. Kwa hiyo kama unazo, ni kitu rahisi sana.

Kuna cousin wangu mmoja alikuwa anasema "kitu kinachotatuliwa na pesa si tatizo, hiyo ni gharama tu, expense. Matatizo halisi hata pesa haiwezi kuyatatua".

Kwa hiyo, elewa tatizo.

Kwa mfano. Inawezekana ndugu yako hana business plan, au haja target business nzuri, au ame target business nzuri lakini eneo si zuri.

Hapo hata ukimsaidia pesa atashindwa biashara tu na kurudi kutaka pesa zaidi.

Naelewa na wewe una maisha yako na labda huna muda wa kuchukua majukumu ya mtu mwingine kuhakiki mambo, lakini, hatua hii inaweza kukufanya uelewe tatizo vizuri zaidi, na uepuke matumizi mabaya ya pesa huku ukiwa unamsaidia ndugu yako vizuri zaidi.

Kitu kikubwa zaidi ni hiki, saidia kwa moyo, usisaidie kwa sababu mtu kakushitaki kwa wazazi.

 
Hapana mkuu.. ndugu yako ndo atakaye kabiziwa mwili wako pindi utakapo kata roho,....msaidie Ila mwambie akiichezea hiyo pesa asikutafute tena..
Mimi pia nimehisi hivyo, ndiyo maana nimewaza kuweka hata kipengele cha riba ili kuongeza uwajibikaji. Yaani ajihisi kama vile anadaiwa Rejesho Saccos hivi
 
Mkuu napokea pongezi zako kwa hiki nilichokifanya πŸ™πŸ™πŸ™

Lengo la kufanya hilo ilikuwa kuvunja mnyororo wa umasikini though inaonekana approach iliyotumika haikuwa sahihi.

Hata hivyo nimejifunza jambo, nitafanyia kazi.
 
Hapana mkuu.. ndugu yako ndo atakaye kabiziwa mwili wako pindi utakapo kata roho,....msaidie Ila mwambie akiichezea hiyo pesa asikutafute tena..
Hilo pia limekuwa likinifikirisha sana, upande wetu bado wamekumbatia mila za kurithi wajane. Probably nikifa, yeye atakabidhiwa familia yangu aendelee kuilea.

Now you can see the problem and predict the consequences πŸ™†πŸ˜­
 
Hilo pia limekuwa likinifikirisha sana, upande wetu bado wamekumbatia mila za kurithi wajane. Probably nikifa, yeye atakabidhiwa familia yangu aendelee kuilea.

Now you can see the problem and predict the consequences [emoji134][emoji24]
We mkurya?
 
Uko sahihi Mkuu, sasa kama mtu unampa mtaji 3 times anaua si manake unayeumia ni wewe uliyempa? Manake wakati mwingine inakulazimu uingie benki ukope ili kumpa mtaji ndugu yako
Read this:

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…