Ingawa na matusi yametaradadi kwa wale wenye mawazo tofauti, ngoja nikazo moyo, nichangie hivyo hivyo.
Tumewahi kusikia mara kadhaa, wakuu wa serikali wakisema kuwa mishahara ikiongezeka leo, basi kesho tu bidhaa zinapanda bei. Kuna shule moja ya sekondari yenye heshima yake hapa kwa ufaulu mzuri, hawa hupandisha ada kila July kwakuwa mwaka wa fedha ndo umetamatishwa na mei mosi mishahara inakuwa imepanda.
Hili jambo la kuongezwa kwa mishahara, pengine liangaliwe upya, sababu za kutaka nyongeza isiwe miaka au vitu kupanda bei.
Kwa wale wanaofanya kwenye taasisi binafsi, wengi wanafahamu hiyo haiwezi kuwa sababu ya ongezeko la mshahara.
Kuna wazalishaji na watoa huduma, sijui TRA wapo kundi gani hapo. Sasa unaposema kwa miaka 5 mshahara haujapanda, vipi kuhusu utendaji wako? Utendaji wa taasisi kwa ujumla? Kama Tanesco wanazalisha 1600MW kwa takribani miaka 10, ambapo pengine 500MW zinatumiwa na wezi wanaoshirikiana na wafanyakazi, ni jinsi gani katika hiyo miaka 10 pato la shirika litaongezeka ili kulipa nyongeza ya mishahara?
Kama TRA wakikusanya 800b flat kwa miaka 5 na pengine kushindwa kukusanya ziada ya 800b ambayo iko wazi ila haiguswi kwa manufaa mapana ya wezi kushirikiana na wafanyakazi, tunapataje nyongeza kwaajili ya mishahara?
Kazi ya kukamilika kwa masaa 2, mtoa huduma atajitahidi akukere na kukuzungusha mpaka umalize siku yako mbele yake bila tija yoyote, huyu MALENGO ya siku/wiki/mwezi/mwaka anayafikiaje mpaka astahili nyongeza bwerere kila mwaka?
Bahati mbaya hayo yote si sehemu falsafa ya watumishi wa umma, na hii ndio sababu serikali haiwezi endesha taasisi yoyote inayopaswa kuwa PROFIT ORIENTED, Tanesco, TTCL, TRC, TRL, BRT, POSTA, ATCL n.k
Taasisi kama hizo, zikienda kwa wawekezaji, zitazalisha faida mara dufu, tutaendelea kuwasifia wanawalipa staffs wao vizuri n.k TBL, TCC, VODACOM, AIRTEL, PANAFRICAN, SONGAS n.k
Kazi iendelee.