Dhana ya kwamba mshahara ukiongezwa na inflation itatokea ni dhana inayopaswa kufikiriwa na kichaa tu

Dhana ya kwamba mshahara ukiongezwa na inflation itatokea ni dhana inayopaswa kufikiriwa na kichaa tu

Matatizo yaliyopo nchini ni makubwa kuliko wstumishi kuongezewa mshahara. Watumishi hawafii hata 1% ya watanzania wote. Ukiweka wategemezi wao hata useme kila mmoja ni 20 bado haifiki hata robo ya watanzania.
Hivyo hili kundi kubwa watanzania wanalotegemea na ambalo Lina 75% ya watanzania wote ndio la kufikiriwa sana
Tufikiri kwa ubongo....!!!
 
Tatizo huna hoja! Mfanyakazi hana tofauti na wewe hapo unapodai au kupigania haki zako! Mfano haki ya kuishi, kuongea, kuabudu, nk.

Mfanyakazi kudai stahiki zake kutoka kwa Mwajiri, siyo dhambi. Ni jambo la kawaida duniani kote. Na hakuna uhusiano kati ya haki za wafanyakazi, na huo uouuzi ulio usema.

Yule kichaa wenu aliwaharibu sana akili. Na ndiyo maana Muumba alimchukua mapema ili kuwaokoa kuwa wendawazimu kabisa. Eti siwezi kupandisha mishahara, kwa sababu nanunua ndege kwanza!!

Sasa kuna uhusiano gani kati ya mshahara wa mfanyakazi na kununua ndege!
Sasa nijibu hili swali, mnataka muongezewe mishahara, kwani mmeongezewa kazi? Je, si sahihi zaidi kudai serikali ishushe bei za bidhaa kama umeme ili watu wazalishe kwa tija, bei za bidhaa zishuke na waTz wote tufaidi? Je na mimi ambae nimejiajiri nitamdai nani aniongezee mshahara ili na mimi nikapambane kugombania bidhaa chache zinazogombaniwa na pesa nyingi kwenye mzunguko (inflation)? Does it sound fair to you?
 
Wapuuzi wengi tu huongea hili hata humu jf . Mada yoyote ikigusa maslahi ya Watumishi tu wanakuja na huo upuuzi wao wa inflation.
Bahati mbaya wengine ni viongozi wa serikali wanalipwa pesa ndefu na kupewa mahitaji yao yote muhimu bure.
Mpaka chupi wananunuliwa kwa kodi zetu lakini hawataki waliochini wapate kidogo cha kuweza kujikimu. Ni ulafi na roho mbaya inawasumbua !!!
 
Kama wewe sio kichaa nijibu hili swali; Je, mnataka muongezewe mishahara, kwani mmeongezewa kazi?
Kwanini badala yake msidai serikali iboreshe mazingira ya uzalishaji mali na huduma ili bei za bidhaa zishuke? Mfano ukishusha bei ya umeme maana yake uzalishaji wa bidhaa utakuwa na tija zaidi na bei za bidhaa zitashuka. Ndio maana nasema abarikiwe alieanzisha mchakato wa bwawa la Rufiji, lile bwawa ndio mwarobaini wa matatizo kama haya
Rubbish!!
 
Ninasema kuwa dhana hii ni mfu kwa sababu zifuatazo;
1. Je, kwa miaka 5 ya Magufuli bei za vifaa vya ujenzi iko palepale Kwakuwa mshahara haujaongezwa?.
2. Je, Tangu tupate uhuru mpaka sasa Marais waliopita ndio walichangia kuongezeka kwa bei za bidhaa kwa kuruhusu ongezeko la mshahara kwa watumishi?.
3. Mbona wabunge wanalipwa pesa nyingi kuliko watumishi wa umma ?. Kama kiasi cha pesa anacholipwa mtendaji wa mtaa ni sawa na hakipaswi kuongezeka ili kukwepa inflation, je kwanini wabunge nao wasilipwe kwa figure sawa na huyu mtendaji wa mtaa . Si mnasema kinatosha .
4. Je, mshahara wa mtumishi wa umma wa ngazi ya kawaida ( sio kiongozi) unatosha kupata mahitaji yake yote muhimu ?.
Haya mawazo ya kutokuwaongezea watumishi mishahara kisa inflation ni ya kipumbavu na hayapaswi kufikiriwa na mtu mwenye utu na akili timamu.
Mtu analipwa zaidi ya milioni kumi halafu anakuja kutoa mawazo mfu namna hii huku akisahau kuwa kuna watu take home yao ni 400,000 au pungufu.
Kuongeza mshahara hakufanyi inflation, kawaida nyongeza inakuja baada ya inflation kwa maana CB wanakuwa na inflation ya ule mwaka nyongeza inakuja kujazia au control ile inflation ndio maana nyongeza zinakuwa number kama asilimia 10 au 5 au 15 hata 20 hii itategemea na inflation ya ule mwaka. Na inflation sio kitu kibaya ni pande mbili ya coin wakati mwingine inflation inakupa dalili ya kuwa watu wana pesa na mahitaji yanakuwa mengi ila bidhaa kama ilikuwa nanunuliwa na watu 10 tu sasa kuna watu 20 wanataka kununua bei itapanda ili kukocontrol inflation ni kuongeza uzalishaji kama wateja wamekuwa 20 mahitaji yameongezea basi ongeza bidhaa ili wote 20 wanunue. Na wakati mwingine inflation ikiwa inapanda sababu zilezile pesa zipo na quality za huduma zinapanda na gharama zinapanda. Hili ni somo kubwa sana unaweza kujaza page. inflation mbaya ni ile kipato kiko palepale lakini bidhaa zinapungua uzalishaji mahitaji makubwa lakini bidhaa hakuna vitu vinapanda lakini kipato hakipandi. natoa mfano mdogo tu kunaweza kuwa na mifano 1000. Mshahara haujapanda uleule kila siku unanunua sukari kilo 1000 mara sukari imeadimika kwa sababu zozote labda uzalishaji umepungua na mahitaji yako palepale ile sukari itaanza kuisha haraka madukani hapo bei itapanda kilo 2000 hapo wewe mtumishi utaanza kuumia. Lakini kwa picha kubwa inflation ni nzuri ikiwa imekuja positive way kwamba mzunguko wa pesa mzuri watu wanapesa wengi wateja wengi changamoto ni kuzalisha zaidi kukidhi mahitaji kama mji ulikuwa unachinja mbuzi 100 kwa siku watachinja 200 sababu wala nyama wengi uwezo upo. Nyongeza ya mshahara ni haki na ina base na inflation ya mwaka ulioisha na pia kuongeza kipato ili kuwezesha watu kununua nje ya mahitaji basic na kuanza kutoka out kula dinner na hii inachochea kukuwa kwa uchumi. ujumbe mrefu lakini somo la inflation ni kubwa, kazi ya serikali ni ku manage inflation in positive way lakini ni kitu kizuri.
 
Kwa hili uliloandika unamdhalilisha huyo kwenye avatar yako....!!

Mnachojua ni maslahi yenu binafsi na matumbo yetu SGR maana ake nn ili hali watu wanalia na ugumu wa maisha...yule aliyeanza kazi 2014 akiwa hana familia leo hii ana familia na wategemezi kibao halafu unamlipa kiasi kile kile.....akidai haki yake mnampa visingizio kibao na mwisho wa picha mnawaambia kama hawataki kazi waache.....dah...siku nikimiliki bunduki nitafyatua ubongo wa watu wengi😊🍺🍺🍺
Kaanza 2014 akiwa hana familia, kaongeza familia, je, ni jukumu la nani kutunza familia yake? Lake yeye aliyepanga idadi ya watoto wa kuzaa au la serikali? Na je, aongezewe mshahara bila kuongezewa kazi? Kwanini basi asidai serikali iboreshe mazingira ya uzalishaji mali ili bei za bidhaa zishuke na kila mTZ apate unafuu, mfano ukishusha bei ya umeme (Rufiji) basi bidhaa zitashuka bei na waTz wote tutapata unafuu.
 
Ingawa na matusi yametaradadi kwa wale wenye mawazo tofauti, ngoja nikazo moyo, nichangie hivyo hivyo.

Tumewahi kusikia mara kadhaa, wakuu wa serikali wakisema kuwa mishahara ikiongezeka leo, basi kesho tu bidhaa zinapanda bei. Kuna shule moja ya sekondari yenye heshima yake hapa kwa ufaulu mzuri, hawa hupandisha ada kila July kwakuwa mwaka wa fedha ndo umetamatishwa na mei mosi mishahara inakuwa imepanda.

Hili jambo la kuongezwa kwa mishahara, pengine liangaliwe upya, sababu za kutaka nyongeza isiwe miaka au vitu kupanda bei.

Kwa wale wanaofanya kwenye taasisi binafsi, wengi wanafahamu hiyo haiwezi kuwa sababu ya ongezeko la mshahara.

Kuna wazalishaji na watoa huduma, sijui TRA wapo kundi gani hapo. Sasa unaposema kwa miaka 5 mshahara haujapanda, vipi kuhusu utendaji wako? Utendaji wa taasisi kwa ujumla? Kama Tanesco wanazalisha 1600MW kwa takribani miaka 10, ambapo pengine 500MW zinatumiwa na wezi wanaoshirikiana na wafanyakazi, ni jinsi gani katika hiyo miaka 10 pato la shirika litaongezeka ili kulipa nyongeza ya mishahara?

Kama TRA wakikusanya 800b flat kwa miaka 5 na pengine kushindwa kukusanya ziada ya 800b ambayo iko wazi ila haiguswi kwa manufaa mapana ya wezi kushirikiana na wafanyakazi, tunapataje nyongeza kwaajili ya mishahara?

Kazi ya kukamilika kwa masaa 2, mtoa huduma atajitahidi akukere na kukuzungusha mpaka umalize siku yako mbele yake bila tija yoyote, huyu MALENGO ya siku/wiki/mwezi/mwaka anayafikiaje mpaka astahili nyongeza bwerere kila mwaka?

Bahati mbaya hayo yote si sehemu falsafa ya watumishi wa umma, na hii ndio sababu serikali haiwezi endesha taasisi yoyote inayopaswa kuwa PROFIT ORIENTED, Tanesco, TTCL, TRC, TRL, BRT, POSTA, ATCL n.k

Taasisi kama hizo, zikienda kwa wawekezaji, zitazalisha faida mara dufu, tutaendelea kuwasifia wanawalipa staffs wao vizuri n.k TBL, TCC, VODACOM, AIRTEL, PANAFRICAN, SONGAS n.k

Kazi iendelee.
 
Sasa nijibu hili swali, mnataka muongezewe mishahara, kwani mmeongezewa kazi? Je, si sahihi zaidi kudai serikali ishushe bei za bidhaa kama umeme ili watu wazalishe kwa tija, bei za bidhaa zishuke na waTz wote tufaidi? Je na mimi ambae nimejiajiri nitamdai nani aniongezee mshahara ili na mimi nikapambame kugombania bidhaa chache zinazogombaniwa na pesa nyingi kwenye mzunguko (inflation)? Does it sound fair to you?
Ngoja nikuelimishe. Mshahara hauongezwi kwa sababu ya kuongezeka kwa kazi. Mshahara huongezwa kwa mfanayakazi, kwa mujibu wa sheria, taratibu, kanuni na mikataba iliyoingiwa baina ya Mwajiri na Mwajiriwa!

Pia katika utumishi, kuna suala la wafanyakazi kupandishwa vyeo/madaraja kila baada ya muda fulani! Kwa taarifa yako, magufuli aliendelea kuwapandisha vyeo/madaraja baadhi ya makundi ya wafanyakazi! Huku akiyabagua makundi mengine!!

Ni zaidi ya miaka 6 sasa kuna kundi ka wafanyakazi halijapewa stahiki zao kwa mujibu wa sheria na taratibu za kiutumishi, kwa sababu tu za kipuuzi. Kwa bahati nzuri huyu MAMA ana akili! Hivyo kupitia Waziri mwenye dhamana wa Tamisemi, ameahidi kuwapa wafanyakazi stahiki zao!

Ulichokiandika hapo juu, ni UGORO usio na uhusiano kabisa na hiki nilicho kuambia hapa. Unaonekana una ulelewa mdogo kwenye masuala ya ajira na haki za wafanyakazi. Hivyo siyo mbaya iwapo utakubali kuuficha huu udhaifu wako.
 
Mtu aliepo kigoma ananufaika VP na SGR?
Aliepo mpanda ananufaika VP na SGR?
Seriously? Kweli hujui kwamba gharama ya usafirishaji wa bidhaa toka bandarini zinaposhuka basi hata hiyo bidhaa itakapofika Kigoma itakuwa ya bei nafuu zaidi? Tunachotakiwa ni kupambana kuhakikisha bei za bidhaa zinashuka nakuwa nafuu zaidi ili waTz wote tufaidi, na sio kuwaongezea mishahara watu ambao hawajaongezewa kazi.
 
Kaanza 2014 akiwa hana familia, kaongeza familia, je, ni jukumu la nani kutunza familia yake? Lake yeye aliyepanga idadi ya watoto wa kuzaa au la serikali? Na je, aongezewe mshahara bila kuongezewa kazi? Kwanini basi asidai serikali iboreshe mazingira ya uzalishaji mali ili bei za bidhaa zishuke na kila mTZ apate unafuu, mfano ukishusha bei ya umeme (Rufiji) basi bidhaa zitashuka bei na waTz wote tutapata unafuu.
Unabisha Ila uonekane mtu wa kutetea hoja Ila ukweli wake unaujua unao moyoni....Tuishie hapa mzee tusijaze server za JF
 
Rubbish ni kujibu hoja bila hoja. Kwanini usijibu hoja kwa hoja?
Sioni na sitaweza ona. Hoja hujengwa kwa nia njema. Hoja yako imejikita katika nia ovu yenye lengo la kuona wengine wanaishi kwa mateso na wengine wakiendelea kufurahia keki ya taifa. Hiyo hoja yako ni valid kwa utawala ulioazimia watu kuishi kama mashetani. Unazijua taratibu na sheria za ajira ????
 
Rubbish!!
Ni bahati mbaya sana kuna watu wanashikwa akili na wana siasa kwa kudhani operating cost basi ni umeme tu maana hata nyanya huwa zinapanda bei sasa sijui zinazalishwa na umeme? Inflation ni mchanganyiko wa vitu vingi sana bidhaa zote zinaweza kuwa bei ilele lakini ikatokea uhaba wa nyumba kodi zikapanda na ikaleta inflation kubwa kabisa dawa ni kujenga nyumba zaidi. nyongeza za mishahara ni haki ya mfanyakazi based on inflation central Bank wanatoa inflation ya mwaka ule na kuonesha inflation imetokana na nini. nchi bila kuwa na inflation hiyo imesimama uchumi haukui na watu hawana pesa.
 
Sasa nijibu hili swali, mnataka muongezewe mishahara, kwani mmeongezewa kazi? Je, si sahihi zaidi kudai serikali ishushe bei za bidhaa kama umeme ili watu wazalishe kwa tija, bei za bidhaa zishuke na waTz wote tufaidi? Je na mimi ambae nimejiajiri nitamdai nani aniongezee mshahara ili na mimi nikapambame kugombania bidhaa chache zinazogombaniwa na pesa nyingi kwenye mzunguko (inflation)? Does it sound fair to you?
Hii ndo inaitwa ku think outside the box...

Miaka 8 iliyopita nlihama kutoka kampuni moja kwenda nyingine, nikaacha cheo nikafuata mpunga bt cheo kidogo kuliko nlichokua nimeahidiwa nlipotoka, bro wangu akaniambia within 3 month matumizi yangu yatapanda kulingana na mshahara and from there sitaona tofauti na nlipotoka so bora nibaki coz pale kuna career growth. sikumskiliza bt now i know what he meant....

A salary is just a trap given to keep you there wasting your time to your employer.

Kifupi kupanda kwa mshahara hakujawahi kua suluhisho la matatzo, kila mshahara ukipanda na matumizi nayo lazima yapande, it will just be an endless loop kila mwaka unalilia upande while huna cha maana unachofanya.
Shtuka, Think outside the box..
 
Kuongeza mshahara hakufanyi inflation, kawaida nyongeza inakuja baada ya inflation kwa maana CB wanakuwa na inflation ya ule mwaka nyongeza inakuja kujazia au control ile inflation ndio maana nyongeza zinakuwa number kama asilimia 10 au 5 au 15 hata 20 hii itategemea na inflation ya ule mwaka. Na inflation sio kitu kibaya ni pande mbili ya coin wakati mwingine inflation inakupa dalili ya kuwa watu wana pesa na mahitaji yanakuwa mengi ila bidhaa kama ilikuwa nanunuliwa na watu 10 tu sasa kuna watu 20 wanataka kununua bei itapanda ili kukocontrol inflation ni kuongeza uzalishaji kama wateja wamekuwa 20 mahitaji yameongezea basi ongeza bidhaa ili wote 20 wanunue. Na wakati mwingine inflation ikiwa inapanda sababu zilezile pesa zipo na quality za huduma zinapanda na gharama zinapanda. Hili ni somo kubwa sana unaweza kujaza page. inflation mbaya ni ile kipato kiko palepale lakini bidhaa zinapungua uzalishaji mahitaji makubwa lakini bidhaa hakuna vitu vinapanda lakini kipato hakipandi. natoa mfano mdogo tu kunaweza kuwa na mifano 1000. Mshahara haujapanda uleule kila siku unanunua sukari kilo 1000 mara sukari imeadimika kwa sababu zozote labda uzalishaji umepungua na mahitaji yako palepale ile sukari itaanza kuisha haraka madukani hapo bei itapanda kilo 2000 hapo wewe mtumishi utaanza kuumia. Lakini kwa picha kubwa inflation ni nzuri ikiwa imekuja positive way kwamba mzunguko wa pesa mzuri watu wanapesa wengi wateja wengi changamoto ni kuzalisha zaidi kukidhi mahitaji kama mji ulikuwa unachinja mbuzi 100 kwa siku watachinja 200 sababu wala nyama wengi uwezo upo. Nyongeza ya mshahara ni haki na ina base na inflation ya mwaka ulioisha na pia kuongeza kipato ili kuwezesha watu kununua nje ya mahitaji basic na kuanza kutoka out kula dinner na hii inachochea kukuwa kwa uchumi. ujumbe mrefu lakini somo la inflation ni kubwa, kazi ya serikali ni ku manage inflation in positive way lakini ni kitu kizuri.
Badala ya kuwaongezea mishahara watu ambao hawajaongezewa kazi, ni kwanini tusishushe bei za bidhaa kwa kuongeza tija katika uzalishaji kwa kushusha bei za umeme kwa mfano (Rufiji) ili bei zitakaposhuka mshahara ule ule utoshe na waTz wote kwa ujumla wanufaike? Yule ambae amejiajiri anamdai nani ili nayeye aongezewe mshahara?
 
Ngoja nikuelimishe. Mshahara hauongezwi kwa sababu ya kuongezeka kwa kazi. Mshahara huongezwa kwa mfanayakazi, kwa mujibu wa sheria, taratibu, kanuni na mikataba iliyoingiwa baina ya Mwajiri na Mwajiriwa!

Pia katika utumishi, kuna suala la wafanyakazi kupandishwa vyeo/madaraja kila baada ya muda fulani! Kwa taarifa yako, magufuli aliendelea kuwapandisha vyeo/madaraja baadhi ya makundi ya wafanyakazi! Huku akiyabagua makundi mengine!!

Ni zaidi ya miaka 6 sasa kuna kundi ka wafanyakazi halijapewa stahiki zao kwa mujibu wa sheria na taratibu za kiutumishi, kwa sababu tu za kipuuzi. Kwa bahati nzuri huyu MAMA ana akili! Hivyo kupitia Waziri mwenye dhamana wa Tamisemi, ameahidi kuwapa wafanyakazi stahiki zao!

Ulichokiandika hapo juu, ni UGORO usio na uhusiano kabisa na hiki nilicho kuambia hapa. Unaonekana una ulelewa mdogo kwenye masuala ya ajira na haki za wafanyakazi. Hivyo siyo mbaya iwapo utakubali kuuficha huu udhaifu wako.
Kwahiyo unaamini mimi sifahamu kwamba nyongeza ni jambo la kikatiba na kimkataba? Huu mjadala lengo lake ni kuwezesha hayo mabadiliko ya kikatiba na kimkataba kwa siku za usoni. Sasa turudi kwenye hoja yangu;
Mnataka muongezewe mshahara bila kuongezewa kazi? Je si sahihi zaidi kudai maboresho katika uzalishaji bidhaa ili watu wazalishe kwa tija ba bei zishuke ili waTZ wote tufaidi? Mfano kushusha gharama za umeme (Rufiji) na gharama za usafirishaji (SGR) Ili kushusha bei za bidhaa na huduma. Hali kadhalika, mimi niliejiajiri, nimkabe nani ili aniongezee mshahara? Si mimi mwenyewe ninae takiwa kujichapa mijeledi na kufanya kazi hadi saa saba usiku ili kipato changu kikue, sasa iweje wengine mtake tuwabebe mgongoni kwa kuvuna msichopanda? Mbona mnajitia utaahira watu wazima na akili zenu? Hovyo kabisa!!
 
Back
Top Bottom