Uchaguzi 2020 Dhana ya "mkono mtupu haulambwi" yaendelea kuonekana katika kura za maoni

Uchaguzi 2020 Dhana ya "mkono mtupu haulambwi" yaendelea kuonekana katika kura za maoni

✓kwanza pole Sana coz tz ni nchi ya ajabu Sana na ndo maana unaona wasanii wote wanashindana kutunga nyimbo nzuri ya kumsifu mwenyekiti wenu huku wakijiua baada ya October wanarudi kwny msoto

✓Pili hakuna kitu ninachokichukia Kama huyo mshenzi kupewa Hilo Jimbo manake yy naye ni sehemu ya umaskini wa hapo mkoani coz Kuna moproco kiwanda cha mafuta kakiua,komoa sabuni kakiua na kiwanda Bora Cha canvas kichokuwa kinauza sn nje maturubai mazito nacho kaua na kibaya kukageuka zizi la mbuzi

✓tatu Moro elimu bado ipo nyuma Sana manake kwa maelezo yako ingekuwa Moshi,Arusha au mbeya wanepindua meza ungepita!!!wao kupewa gari la kuzikia wameona wamepewa maisha wakati hvyo viwanda vingekuwa vinafanya kazi wangekodisha Yao badala ya Hilo bovubovu

✓nne nawe umerudi kule kule kujionesha,kwangu sijaona sababu ya kutuwekea umesoma nn na namba yako ya simu Kama siyo kutaka wakuone na hii ishara unachokilalamikia ndo utakachofanya hata ww ukiwa kwny mfumo

all in all umejaribu kwa Mara ya kwanza madhaifu ya Leo yakawe darasa awamu ijayo na mandalizi yaanze sasa
 
Kwani ulikua hujui wenzio hua wanafanyaje ili wapigiwe kura nyingi za ndio?(unafiki), Unasema una wasiwasi ccm usije kurudi kwenye azimio la Zanzibar baada ya magufuli😂 Mbona unajaribu kudanganya nafsi yako na ukweli unaujua?(unafiki). Toka lini ccm imekua ya siasa za azimio la Arusha Toka mwalimu alipoachia madaraka? Mmebaki na propaganda tu lakini ccm ya magufuli Ni Ile Ile tu ya wahuni, wezi, Wala rushwa, na mafisadi. Endelea kuwa na Moyo ule ule usikate tamaa na chama chako. Maelezo yako mengi Ni kulalamika. UKOME 😂😂😂😂😂
 
Mkiambiwa mtaji wa ccm ni ujinga wa Watanzania walio wengi huwa mnabisha. Na kwa kauli yako mwenyewe mwana ccm hii ya Magufuli umekiri kuwa kuna Watanzania (tena uliokuwa unawaomba kura- which means angalau wanapaswa kuwa na uelewa japo kidogo) hawamjui Magufuli; sasa hoja yenu kuwa Jiwe anapendwa na kukubalika na kila mtu msingi wake ni upi?

Welcome to the real world.
 
Watu wanataka mtu aliyepamoja nao..
Mkono mtupu haulambwi sometimes siyo pesa..
Morogoro mwarabu anaishi nao, wanamuona, wanaziona biashara zake, wanamuona wakipatwa msiba, harusi, barabara zikiingia dhahma na majanga ya maji. Na shida zao za buku buku wakienda kulialia anawapa.

Abood hata waarabu wenziye kumwangusha itabidi wafanye yale anayoyafanya na zaidi..
Al-Saedy kaanguka kura za maoni, watu wameona mchoyo tu, mabasi anayo mbona hayasaidii mtu.

Nimeona hata Kwimba, Mansoor wa MOIL..
Kishapu kwa Nchambi..
Wao hawakai Dar-Es-Salaam, wanakaa huko majimboni.
Marehemu Filikunjombe naye muda mwingi aliutumia Ludewa, siyo Dar-Es-Salaam..

Mkuu 2025, anza kuifanyia kazi sasa, changia miradi ya maendeleo, shiriki na uwepo katika shughuli za kijamii..
Elimu, watu walishaelimika huwezi kuwaambia utawajengea ndege na viwanda wakaamini.. Wana uelewa mbunge hana huo uwezo!

Everyday is Saturday.......................... 😎
 
Morogoro sio wajinga wanathamini vya kwao na wapo tayari kuvilind vilivyo vyao...Abood kazaliwa Morogoro na still bado anaishi Morogoro kwahyo anazijua shida za Moro nje ndani..wewe umeukimbia mji ajabu zaidi hata tawi lako LA ccm lipo kimara baruti(Dar).. umeshindwa kusoma alama za nyakati na nahisi huwajui watu wa Morogoro...Morogoro sio kama maeneo mengine huwezi kuwa mbunge wa Moro kama hujawahi kuishi hapo Mbunge lazima uwe mkazi wa Morogoro ndio watakuchagua.. vinginevyo ukiwaletea historian ulizokalilishwa km ww ukivyokuwa watakubwaga tu
Ina maana yule wa Kilosa nae ataangukia pua?
 
Umeandika mengi, lakini siasa si cv za kuonyesha jukwaani, siasa ni kuwa mtu wa watu, uishi nao, wakujue,uwajue.

wengi wanafikiri siasa ni usomi.......tujifunze hili.

anza sasa kuwa na watu, ishi nao, jua shida zao, wakujue, ndipo utashinda.

Abood pamoja na madhaifu yake, lakini yupo na shida za wananchi.....hizo wee unazoziona ndogo wananchi wanamwona ni mwenzao
 
Umeandika mengi, lakini siasa si cv za kuonyesha jukwaani, siasa ni kuwa mtu wa watu, uishi nao, wakujue,uwajue.

wengi wanafikiri siasa ni usomi.......tujifunze hili.

anza sasa kuwa na watu, ishi nao, jua shida zao, wakujue, ndipo utashinda.

Abood pamoja na madhaifu yake, lakini yupo na shida za wananchi.....hizo wee unazoziona ndogo wananchi wanamwona ni mwenzao
Asante...umeongea point!

Amechukulia siasa za kugombea ubunge kama JOB INTERVIEW..
Wananchi waangalie academic qualifications, kujibu maswali kama, Y do u think u r the most suitable candidate for this job.

Everyday is Saturday........................... 😎
 
Será zako tamu tamu hawajaanza kuzisikia kwako zishatamkwa mara mía na wagombea mbalimbali waliopita miaka dahali so ulipaswa ujiongeze baba
Kuna Mdogo wangu Ni Katibu wa CCM Wilaya Moja ivi; ALinambia kwamba Wajumbe wa CCM Huwa hawaitaji sana Sera; Huwa wako Money Oriented; Kama Utakuwa na Sera na Hela then you will be in Good position; Sera tupu hawahitaji.

Lakini pia Anasema Kama hata umekuwa na pesa kidogo, ambayo unaweza kuwa unasapoti au ukawa unawatoa kwenye maisha ya kawaida ya kila siku; Yaan kama maisha yako na wa jumbe huwa unawapa support, ndo ivo akija Yule ambaye ana hela, wanakula hela zake then Kura wanakupa wewe, Wajumbe life lao gumu wanapenda sana mtu ambaye anawajali kwenye Shida zao na Raha pia wako pamoja.

Baadhi ya Wabunge hata wakiwa nje ya jimbo huwa wanaendelea kushiriki shughuli za jimboni kupitia kwa Viongozi wa chama, au wakirudi majimboni wanawaita wajumbe wa kata zote ili kukaa nao na kupata chochote; Ilimradi kugawana

Mfano mwaka jana nilikuwa Tz, Nilienda moro kuna rafiki yangu nilisoma naye primary alifariki; Plae home mambo hayakuwa vizuri na msiba ulikuwa upelekwe Lushoto; Kupitia Mjumbe mmoja wapo wa kata moja, Alionge na Abood, Jamaa akatoa Basi lake, akaweka mafuta watu wakaenda huko lushoto kuzika na kurudi, kwa Gharama zake; Vitu kama hivi ni vizuri sana.

Suala namba moja ni kuishi nao vizuri wale viongozi na wajumbe; Sio kipindi cha uchaguzi tu, hiyo iwe ni life style yako.
 
Uzi wako umeelezea kila kitu.... Hongera kwa uchambuzi mzuri...
Watoto wote tuliokulia Moro tumebanana Dar kunakopatikana ugali.
 
IMG-20200722-WA0012.jpg
 
Kaka Umeongea kwa uchungu Mkubwa sana na Umewakilisha kilio cha Watu Wengi kwa tathmini ya haraka CCM ina wenyewe ndio Hao Wamerudi tena kwa kura nyingi Prof Kapuya,Magreth Sitta,Jerry Slaa,Mama Salma Kikwete,Ridhwan,Mtemvu nk Nilitegemea kuhesabu kura kwa uwazi ingewabeba Vijana lakini imekuwa tofauti nadhani hata Mwenyekiti hatapenda japo ndio Wameshinda wengi sana yaani Tumepatikana Watanzania Vijana Wameshinda wachache sana



Hivi kwanini mnadhani vijana ndio watu sahihi? mbona wametuangusha sana? hawana lolote kazi yao kulialia tu na kufanya kazi kwa sifa na maneno ya dharau na kukosa heshima kwa watu.
 
Kwanza sera zako zenyewe tu zilikuwa hazitekelezeki

wajumbe wamekuona kijana una njaa kali sana bora wamchague alieshiba ili nao wale makombo ya alieshiba

Hiyo masters yako tafuta kazi ufanye upate pesa ukalamwe mikono na wajumbe mwaka 2025
 
Uliambiwa mapema kabisa CCM ina wenyewe ukajipa moyo utavuka.Haikutosha ukaambiwa Moro ina mwenyewe hata ukagangwe wapi hutoboi ukabisha.

Mtoto akililia wembe wewe mpe umkate apate akili.Siku nyingine ingia kwenye ngoma huku unajua kucheza,siyo kukurupuka tuu,maana wenye smart phone watakurekodi uonekane kituko.
 
Huwezi kuutenganisha umoja uliopo Kati ya rushwa na CCM kamwe haiwezekani.

Kama samaki anaweza kuishi nje ya maji Basi rushwa itakwisha.
 
Bora hata wewe umepata kura moja. Mimi nimekwenda na wajumbe kwenye gari yangu. Safari nzima wananiimbia mapambio. Kura zulipohesabiwa nina kura sifuri.
[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2] chezea siasa wew.

Kuna watu wanawatafutia wajumbe Hadi sehem za kulala, chakula na usafir na bado wanapata sifuri wew lift tu unalalamika.
 
Back
Top Bottom