Kuna watu wanafurahia Mh Mbowe kuondoka kwenye nafasi ya Uenyekiti,kuna wanaotaka hata kuandamana ili aondoke,je chama ni cha kikabila kwasababu tu kwamba mwenyekiti ana kabila?Kwahiyo mwenyekiti akiwa mgogo basi cha ni cha kigogo?
Kuna anayeweza kuniambia ukabila uko wapi kwenye chama cha cdm?Je ni kweli kuwa mwenyekiti mchagga akiondoka ndo chama kitakuwa si cha wachagga?Ili linanitatiza sana tu!
JMushi nadhani kuna haja ya chadema kueleza kwa kina na kwa mijadala mipana zaidi nini haswa 'misingi ya chama'. Hapa wataalamu wanaweza kuhusishwa kwa ajili ya kutoa technical clarifications kuhusu baadhi ya issue za kitaaluma.
Kwa nini nasema hivyo. Nimesikia mara kadhaa kwenye hotuba za Mbowe akisema 'hakuna aliye juu ya chama'. Lakini pia nimeshasikia one time Mnyika alikuwa akitoa ufafanuzi juu ya sera ya mrengo wa kati wa chadema. Kuna hatuba nyingine ya Mbowe aliitoa alipokwenda USA, akaeleza kwa kirefu sana juu sera za CDM, kwamba cdm siyo chama kinacho kumbatia umaskini, kwamba cdm ni chama kinacho amini katika individual ability to develop themselves rather than waiting for the goverment, serikali iwawezeshe watu. Kwa mtazamo wangu hizi ni baadhi ya misingi ya chama. Ila katika kuongelea mambo haya, ambayo kwa mtazamo wangu yanareflect misingi ya chama, huwa haiwekwi wazi sana pale mtu anapozungumzia hakuna mtu aliye juu ya chama. Nadhani katika kauli kama hizi, ni vizuri watu wakaelezwa nini maana ya 'kutokuwa juu ya chama'.
Nikienda kiundani zaidi kuhusu misingi ya chama. Misingi ya chama ndio chama chenyewe. Na hapa mtu anapozungumzia katiba ya chama inabidi atofautishe na misingi ya chama. Katiba ya chama naweza kusema ni mwongozo tu ambao unaweza usitoe ufafanuzi kuhusu misingi ya chama. Misingi ya chama ni yale maono ya chama ambayo kwa hayo ndio chama kilianzishwa. Yanaweza kuwa ni maono ya kamati kuuu au wajumbe ambao either wameshiriki katika kuyadecifer maono hayo na kuya transfer maono hayo kwa wale wote ambao utumishi wao ni wa kutukuka katika kusimamia misingi hiyo. Na kwenye hii misingi kuna kuwa na utaratibu wakiziboresha na kuzibadilisha bila kuathiri utendaji wa chama.
My point ni kwamba watu wengi haswa maccm na hta baadhi ya viongozi wa cdm kwa kushindwa kuelewa hilo wanashindwa kuelewa dhana nzima ya chadema na misingi ya kuundwa kwa chama. Ni uwazi usio na kificho kwamba katika hili misingi ya cdm ni tofauti sana na ccm. Inabidi waelewe pia Misingi ya chama pia siyo katiba ya chama. LAkini hili halijawekwa wazi sana na viongozi wa cdm. Ndo maana watu wanaropoka tuu udini, ukabila, ukanda nk. Kwa sababu hawaelewe misingi ambayo cdm inaisimamia. CCM misingi yake ilishakufa, hili swala la misingi linaweza kuwapatabu, ndo maana kwenye mambo mengi sana wanashindwa kufanya maamuzi. Muungano upo hoi, azimio la arusha limeshazikwa. CCM ni chama cha kishikajishikaji tu!! Its like a group of cannibals animals, which if they dont get food they will eat each other.
Haya mambo ya kifafanuliwa sana kwa undani kupitia makongamano, vijarida tV sessions, magazetini yatasaidia sana kufungua akili za watu kuepukana na hizi kasumba za watu waccm wanasambaza sera zao za udini, ukabila na uakanda.
Misngi ya chama ielezwe vizuri na maana ya kutokuwa juu ya chama ifafanuliwe zaidi, haswa baada ya kufukuza akina zitto.