Dhana ya udini, ukabila na ukanda wa CHADEMA

Dhana ya udini, ukabila na ukanda wa CHADEMA

Umeona eeeeeeeee!

Jamaa hata hawajitambui kabisa kwenye maisha yao wanatumikia kafiri wapate ulaji.

mtatapatapa sana na hiyo hoja yenu mfu.kama ni ukanda mzee wetu makani alitokea moshi sio? au heche naye ni mchaga? watu waliofilisika sera huwaza ukabila na udini.kwa taarifa yenu cdm ina wanachama na wapenzi wengi kanda ya ziwa kuliko hata kaskazini.
 
Kumbe pakuanzia ni kwa shonza,mtela,mwigamaba,zito,shibuda na wengine wa aina hii sijui kama wewe ni muumini wa demokrasia pengine wewe ni mnufaika wa hawa wanaowanyanyasa hawa watu na kujiita wao ni miungu watu kwenye jamii na chadema kwa ujumla lakini wanajaribu kina cha maji kwa miguu yote miwili.

pls go to the point.
 
mnyukano mkali unaoendelea ndani ya chadema ni dhahiri ni baina ya kundi ambalo halitokei kaskazini na watu wa kaskazini(slaa, lema, mbowe, mnyika, n.k) wanaoamini kuwa chama kiliasisiwa kaskazini, kikalelewa kakskazini na pengine wana imani kuwa bila ya watu wa kaskazini chadema hakitakuwepo tena.

Ombi langu ni viongozi wengine wa cdm ambao hawatokei kaskazini(mimi namjua heche peke yake kwa sababu ni ndugu yangu) waje waseme, hii nguvu waliokuja nayo akina lema kama zina chembechembe za u-kaskazini au la, na kama ndiyo hivyo hawaoni kama wao kuendelea kuwepo chadema wanasaliti wenyeji wa mikoa kwa vile na wao wanawahitaji kuwapigania?

tuzungumzie meno ya tembo kwanza,nani anawajibika kwa kuwakumbatia wachina hapa nchini.hiyo ndiyo issue yenye maslahi ya taifa.achana na habari ya cdm
 
Huwa najiuliza sana, Hivi Lengo la Edwin Mtei kuanzisha CHADEMA lilikuwa ni nini?

Ndio maana nyie magamba hovyo kabisa. Kwani hivyo vingine havikuanzishwa na mtu? kwa taarifa yenu kaskazini haikwepeki. Mrema, Mbatia, etal wote ni wa kaskazini. Wake wa hao viongozi wenu asilimia 90 ni kask. Au mnabisha? HATA KINANA ni wa kaskazini, ukiacha Sumaye, na Mamvi yule fisadi LOwasa.

BTW je hivi ni nani mwasisi/mwanzilishi wa hili ccm lenu tokea TAA na alikuwa na lengo gani? Je alikuwa wa Kusini, mashariki, magharibi au kati?

Hizo alergy zenu za kikaskazini pelekeni huko kwenu.
 
Kumbe pakuanzia ni kwa shonza,mtela,mwigamaba,zito,shibuda na wengine wa aina hii sijui kama wewe ni muumini wa demokrasia pengine wewe ni mnufaika wa hawa wanaowanyanyasa hawa watu na kujiita wao ni miungu watu kwenye jamii na chadema kwa ujumla lakini wanajaribu kina cha maji kwa miguu yote miwili.

Kama wananyanyaswa wanasubiri nini kuondoka? yaani ktk mamilion ya wanachadema wanyanyaswe wao tu? mbona mimi msukuma lakn sinyanyaswi? KAMATI KUU YA CDM INA WAJUMBE WANGAPI? NA WANATOKA MIKOA GANI? unategemea nani awajengee chama then wao waje waongoze tu,mwigamba hata uchaguzi tu wa madiwani aliukimbia wenzake wakahakisha ushindi unapatikana,alikuja magu kuomba ubunge halafu akaingia mitini hata familia ya kwao haimuelewi ipo hapa magu mtaa wa ibidanja.wasukuma ni watu ma giant na huwa si watu wa kulialia na kutegemea kubebwa na ukabila au udini.
 
Hatutamchagua mtu wala kumkataa kwa kabila lake wala dini yake na hatutamchagua mtu msaliliti eti tu yeye ni wa kanda yetu au kabila letu au kwa kigezo tu cha kuwaondoa wachaga au watu wa kaskazini. soure: mimi mwenyewe msukuma wa igoma mwanza
 
Hoja dhaifu sana wangemchagua vipi wakati yeye ndio muasisi wa Chadema kajipange upya mkuu.
Kama Bob Makani ni muasisi sasa suala la ukanda na udini linaloimbwa na chama cha familia yenu linatoka wapi huoni na nyie mnatakiwa mjipange pia?
 
Kwanini swala la ukabila linapozungumzwa watu humkimbilia makani kuwa ndio ngao halisi yakutokuwa wabinafsi? achani ukweli uitwe ukweli na uongo uite jina lake!
 
Bob Makani ndiyo kigezo? Weka hapa majina mengine ya viongozi wa ngazi ya juu wa chadema waisalamu japo 10 nikupe shilingi millioni moja haraka.
 
bob makani ndiyo kigezo? Weka hapa majina mengine ya viongozi wa ngazi ya juu wa chadema waisalamu japo 10 nikupe shilingi millioni moja haraka.

nadhani madai yako ndiyo madai dhaifu kabisa kupata kutokea hapa tangu jf izaliwe ! Hongera sana kwa kuvunja rekodi !
 
CHADEMA ni jitahida za WAKRISTO kutaka kuhodhi madaraka yote nchini! Wamenufaika sana na CCM sasa wameanzisha upinzani pia! CCM na CDM ni baba mmoja mama mmmoja! Ona wanavyokubaliana katika kila issue DHIDI ya Waislamu Tanzania! Kama kuna muislamu CHADEMA ni MURTAD!

Dha'if sana!
 
Bob Nyanga Makani ni mmoja wa waasisi wa CHADEMA, ni Msukuma, Mwislamu kutoka Kutoka Shinyanga na katibu mkuu wa Kwanza wa CHADEMA.

Katibu mkuu ndiye mwenye siri zote Chama, ndiyo anakaa na mafaili yote, ni mwajiri wa wafanya kazi wa makao makuu nk.

Nimejifunza mambo yafuatayo.
Mosi, Kama waanzilishi wa CHADEMA wangekuwa na agenda udini wasingemchagua Bob Makani kwa sababu yeye ni Mwislamu. ( Binafsi nimejua dini yake wakati wa msiba)

Pili kama waasisi wa CHADEMA wangekuwa wanaagenda ya Ukanda wasingemchagua Bob Makani kwa sababu hatoki kanda ya kaskazini.
Tatu, Kama waasisi wangekuwa na agenda ya ukabila wasingemchagua Bob Makani kwa sababu si Mchaga.

Kitendo cha kumchagua Msukuma, Muislamu, kutoka kanda ya Shinyanga katibu mkuu na baadaye kuongezewa cheo na kuwa Mkiti ina maanisha kuwa alifanya kazi vizuri na alikuwa anakubalika na wajumbe wote bila kujali dini, ukanda wala ukabila.

Wale waliokuwa wanacheza CD ya udini, ukanda na ukabila dhidi ya CHADEMA sasa inabidi watafute CD nyingine ya kucheza dhidi CHADEMA vinginevyo hii ya Ukanda, . ukabila na udini sasa zimechuja. Haiuziki tena.

Ni mawazo yangu tu.

KAMANDA , HAWA WOTE WANAOENEZA HIZO PROPAGANDA HILO WANALIFAHAMU BALI WANAFANYA HIVYO KAMA MBINU YA KUOKOA CCM , wala HATA SI WATU WA DINI HATA KIDOGO , NI WAVURUGAJI TU ! MIMI NAWAONA KAMA WAPAGANI , MAANA KUIUNGA MKONO CCM NI SAWA KABISA NA KUMWABUDU SHETANI .
 
Kwa akili yako ndogo umeona udini ni ukiristo tu!nikikwambia uweke viongozi wa chama fulani wakristo wafike 10 utaweka?
 
Kuna watu wanafurahia Mh Mbowe kuondoka kwenye nafasi ya Uenyekiti,kuna wanaotaka hata kuandamana ili aondoke,je chama ni cha kikabila kwasababu tu kwamba mwenyekiti ana kabila?Kwahiyo mwenyekiti akiwa mgogo basi chama ni cha kigogo?

Kuna anayeweza kuniambia ukabila uko wapi kwenye chama cha cdm?Je ni kweli kuwa mwenyekiti mchagga akiondoka ndo chama kitakuwa si cha wachagga?Ili linanitatiza sana tu!

Wana JF
Ni wazi sasa JK kama Forum ambayo imekuwa na mchango mkubwa kwa kuibua issues na kuleta changamoto kwa Vyama vya Siasa, Serikali na mambo mengine katika Nchi imeacha mwelekeo na sasa tumapiga ngoma ya kuwgawa watanzania kwa uwazi kabisa .Najua nguvu kubwa mnayo tumia ni kwa kuwa majina yenu mnaficha lakini mjue hawakomolewi Chadema tu .Nimeingiwa na wasi wasi Watanzania wamejenfa uhama na WACHAGA direct kisa mgogoro wa Zitto na Chadema yake .

CCM Kilimanjaro iko hai na imechaguliwa na Wachaga .Leo CCM na wasiokuwa CCM wanakuja hapa na kuwarushia wachaha matusi yote .Kukosa heshima ni jambo kwa kusingizia Chadema .Kama mtu ana shida na Mbowe mchaga aseme kwa uwazi na si kusema Wachaga .Mnatugawa kwa UDINI .Mimi Zitto ni ndugu yangu na yeye anajua mie ni Mkatoliki tena mseminary .Hatukuwahi kugombana kwa hilo .Zitto kwangu ni kwake na kwake ni kwangu .Nayasema haya ili wapambe wanaotaka ku verify wamuulize .Muulizeni unamjua Lunyungu ? Atawaambia .Zitto si mdini , si mkabilahata kidogo .Zitto ana marafiki wakubwa ambao ni Wachaga .

Limezuka Wimbi ka kuwatukana Wachaga , kuwabagua watu kwa ukanda wao hadi wengine kusema udini .Chitanda mimi na wewe ni marafiki tangia mwaka 1995 na unajua mie ni Mkatoliki tumecheka , tumekula, tumesaidiana , sikuweza kujua kwamba unanichukia kwa Ukristo wangu .Najiuliza wacha wanao soma habari hizi wanawaza nini juu ya marafiki zao ambao si wachaga .Hizi chuki na maneno ya kutugawa mnayasema kwa kuwa Zitto anavutana na Chadema yao ? Are we sincere au agenda ya udini , Ukanda na Ukabila mmekuwa nayo siku zote ? Hata viongozi wakubwa wa CCM wamediriki kujenga hoja za Ukanda .Mzee wangu Wassira , ndugu Nape , Mwigulu na wengine .Haya mna manufaa nayo ? Ni kweli hizi ndiyo Siasa?Mnadhani matusi haya baadaye CCM mtaenda kuomba kura Kilimanjaro ? Ni kweli watu wa kaskazini ni wabaguzi ? Hebu tuangalie Kaskazini CCM ina Wangune wangapi ? Je walichaguliwa kwa Uwingi wa watu katika madhehenu yao ?

Nimekerwa na ninazidi kukerwa na siasa hizi .Lakini mkae mkijua karibia tutapiga kampeni kwa kilugha na imani zetu za dini maana ndivyo mnavyo taka .Gharama zake ni kubwa sana kutaka kuziba ufa wakati mkiona hali si hali .

Nawasilisha
 
Kuna watu wanafurahia Mh Mbowe kuondoka kwenye nafasi ya Uenyekiti,kuna wanaotaka hata kuandamana ili aondoke,je chama ni cha kikabila kwasababu tu kwamba mwenyekiti ana kabila?Kwahiyo mwenyekiti akiwa mgogo basi cha ni cha kigogo?

Kuna anayeweza kuniambia ukabila uko wapi kwenye chama cha cdm?Je ni kweli kuwa mwenyekiti mchagga akiondoka ndo chama kitakuwa si cha wachagga?Ili linanitatiza sana tu!

Chama hiki kimejipambanua kuwa ni cha wachaga kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Viongozi wakuu wa juu hawakuchaguliwa kwa sifa bali ni kwa kabila lao. M/kiti, mtunza fedha akina mnyika. Makatibu wengi wa mikoa ni akina kilewo, munisi, kiwia
2. Kati ya wabunge 25 wa kuteuliwa hakuna wanaotoka mikoa ya kusini ya mtwara na lindi kama wapo tutajie
3. Asilimia kubwa ya wabunge wa kuteuliwa ni wachaga au watu wanaousiana na big fish kama vile rose kamili, dada yake lisu n.k.
4. Kwenye chadema sio tu chama cha kikabila bali ni chama chenye mwelekeo wa kifamilia.
 
Chama hiki kimejipambanua kuwa ni cha wachaga kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Viongozi wakuu wa juu hawakuchaguliwa kwa sifa bali ni kwa kabila lao. M/kiti, mtunza fedha akina mnyika. Makatibu wengi wa mikoa ni akina kilewo, munisi, kiwia
2. Kati ya wabunge 25 wa kuteuliwa hakuna wanaotoka mikoa ya kusini ya mtwara na lindi kama wapo tutajie
3. Asilimia kubwa ya wabunge wa kuteuliwa ni wachaga au watu wanaousiana na big fish kama vile rose kamili, dada yake lisu n.k.
4. Kwenye chadema sio tu chama cha kikabila bali ni chama chenye mwelekeo wa kifamilia.
nina ubhakika kuna watakaokuja na kuweka kujibu baadhi ya maswali yako hapo juu,however Lissu ni mchagga?chama ni cha kifamilia kwasababu tu kuna wenye uhusiano ambao wako ndani ya chama?je ccm ni chama cha kikwere kwasababu mwenyekiti na familia yake wana nfasi ndani ya chama?je chama hicho ni cha kifamilia?
 
Hakuna ukabila kwenye Chadema ni maneno ya watu wavivu kufikiria. Kuna viongozi wengi wa kaskazini kwasababu kuna wabunge wengi kaskazini. Zitto mafano wakati anaingia Chadema alikuwa kijana kidogo na hakuwa na kitu hivyo sio ukabila vilevile wanaosema Chadema ni chama cha Wachagga ni wana Chama au? kwasababu huwezi kuwa kiongozi kama si mwanachama. Sugu, Msigwa, Lissu, mbunge wa Mwanza wote hawa hawajatokea kaskazini!. Kama unataka kukosoa chama jiunge kwanza huwezi kuchagua watu tu wa Lindi wakati hawako kwenye harakati.
 
Back
Top Bottom