Chama hiki kimejipambanua kuwa ni cha wachaga kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Viongozi wakuu wa juu hawakuchaguliwa kwa sifa bali ni kwa kabila lao. M/kiti, mtunza fedha akina mnyika. Makatibu wengi wa mikoa ni akina kilewo, munisi, kiwia
2. Kati ya wabunge 25 wa kuteuliwa hakuna wanaotoka mikoa ya kusini ya mtwara na lindi kama wapo tutajie
3. Asilimia kubwa ya wabunge wa kuteuliwa ni wachaga au watu wanaousiana na big fish kama vile rose kamili, dada yake lisu n.k.
4. Kwenye chadema sio tu chama cha kikabila bali ni chama chenye mwelekeo wa kifamilia.
Nayasoma maswali yako naona kama yana mapungufu ima ya bahati mbaya au ya kukusudia, sijui ni lipi kati ya hayo.
1. Viongozi wakuu una maanisha akina nani? Kwa kadri ninavyoelewa viongozi wakuu ni Mbowe, Salaa na Zitto
Sijui kama una ordhodha ya wajumbe wa kamati kuu na halmashauri kuu kuthibitisha zaidi hoja yako.
Sijui kama wabunge ni sehemu ya viongozi au la, na kama ni hivyo uwiano upoje
2. Kabla ya mwaka 2010 hakukuwahi kuwa na mbunge wa upinzani kutoka mikoa ya kusini. Hadi leo Mtwara haina mbunge wa upinzani kama kumbu kumbu ni sahihi. Pengine ungejiuliza kwanini mikoa hii ni ngome ya CCM na utawezaje kupata wanachama wenye sifa kama hawapo ndani ya chama kwa kuanzia.
Kumbuka wabunge wa kuteuliwa si wabunge wa taifa ni wabunge wanaotokana na uanachama wa vyama vyao.
Pia uende mbali na kujiuliza kwanini umezungumzia Mtwara na Lindi na siyo Ruvuma , Kigoma na Singida.
3. Hilo la kuhusiana na big fish nalo pia naweza kukuuliza vipi umeshangaalia chama tawala kama ni tofauti? na kama ni sawa kwanini tusidhani mfumo wa demokrasia una tatizo sehemu fulani bali tuchague chama kimoja? Je, inawezekana umechukua CDM kama sample ya tatizo unalokusudia kuli address au ndio ukweli ulivyo?
4. Ulitakiwa uonyeshe mwelekeo wa kikabila pia. Kusema kina mwelekeo bila kuwa na takwimu kunavunja nguvu ya hoja hii.
Ninaweza kusema CDM ina mwelekeo wa ushemeji nikawa sawa kama wewe na sote tukawa sahihi kwasababu ndivyo tunavyoona. Lakini basi, je ndio ukweli wenyewe. Je, tuna takwimu za kuonyesha madai hayo?
Ni katika senti sumuni tu