Dhana ya udini, ukabila na ukanda wa CHADEMA

Dhana ya udini, ukabila na ukanda wa CHADEMA

Kuna watu wanafurahia Mh Mbowe kuondoka kwenye nafasi ya Uenyekiti,kuna wanaotaka hata kuandamana ili aondoke,je chama ni cha kikabila kwasababu tu kwamba mwenyekiti ana kabila?Kwahiyo mwenyekiti akiwa mgogo basi chama ni cha kigogo?

Kuna anayeweza kuniambia ukabila uko wapi kwenye chama cha cdm?Je ni kweli kuwa mwenyekiti mchagga akiondoka ndo chama kitakuwa si cha wachagga?Ili linanitatiza sana tu!

Usitatizwe na wapuuzi wanaopotosha ukweli. ccm wanatafuta mbinu nyingi kuididimiza chadema kwa kutumia ukabila na udini kama mtaji. Mimi ni Mnyiramba naichukia ccm kwa kuwagawa watanzania kwa dini zao. Mwenyekiti wa chama hiki alipokuwa Mzee Makani ccm waliimba wimbo wa udini weeeee, baada ya Mbowe kuingia Ukabila ukashika kasi, nashukuru watanzania wamewapuuza chama linasonga mbele
 
Mkuu hizi ni kauli za kule chit chat,hazina nafasi humu.

can you stand the heat?? au kwa sababu una share JF unaweza anzisha thread ambayo huwezi kuijibu

wewe mchaga , CHADEMA NI WACHAGA, CDM======CHAGA DEVELOPMENT MANIFESTO

period
 
Chama hiki kimejipambanua kuwa ni cha wachaga kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Viongozi wakuu wa juu hawakuchaguliwa kwa sifa bali ni kwa kabila lao. M/kiti, mtunza fedha akina mnyika. Makatibu wengi wa mikoa ni akina kilewo, munisi, kiwia
2. Kati ya wabunge 25 wa kuteuliwa hakuna wanaotoka mikoa ya kusini ya mtwara na lindi kama wapo tutajie
3. Asilimia kubwa ya wabunge wa kuteuliwa ni wachaga au watu wanaousiana na big fish kama vile rose kamili, dada yake lisu n.k.
4. Kwenye chadema sio tu chama cha kikabila bali ni chama chenye mwelekeo wa kifamilia.

Usiwe mvivu wa kufikiri na kudadisi angalau kwa akili yako ndogo. Usikurupuke kuyasema usiyoyajua ukaonekana --------. Wewe ni mkabila ndo maana unayasema hayo ila ukweli utabaki pale pale. Watanzania wa leo hawadanganyiki. Rose kamili siyo Mchagga, Slaa Siyo Mchagga, Prof Baregu na Prof Safari siyo Wachagga, Kitina na Zitto hawakuwa Wachaga (ila wasaliti wa mageuzi ya Umma), Said Afri siyo Mchaga n.k. Kama hao wasaliti wamekugusa sana wanasubiri huko CCM muwape kadi maana inaonekana imewagusa sana wakati ya CHADEMA hayawahusu.
 
chadema ni chama cha kikabila na hili liko wazi kabisa hakuna mjadala.ni chama cha kichaga chenye lengo la kuendeleza fikra za kibaguzi za akina chief marealle ambazo nyerere alizikataa katakata,msitufanye watz mazezeta kuwa hatujui kilichopo nyuma ya pazia

acha uzembe na upotoshaji
 
Chama hiki kimejipambanua kuwa ni cha wachaga kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Viongozi wakuu wa juu hawakuchaguliwa kwa sifa bali ni kwa kabila lao. M/kiti, mtunza fedha akina mnyika. Makatibu wengi wa mikoa ni akina kilewo, munisi, kiwia
2. Kati ya wabunge 25 wa kuteuliwa hakuna wanaotoka mikoa ya kusini ya mtwara na lindi kama wapo tutajie
3. Asilimia kubwa ya wabunge wa kuteuliwa ni wachaga au watu wanaousiana na big fish kama vile rose kamili, dada yake lisu n.k.
4. Kwenye chadema sio tu chama cha kikabila bali ni chama chenye mwelekeo wa kifamilia.
Nayasoma maswali yako naona kama yana mapungufu ima ya bahati mbaya au ya kukusudia, sijui ni lipi kati ya hayo.

1. Viongozi wakuu una maanisha akina nani? Kwa kadri ninavyoelewa viongozi wakuu ni Mbowe, Salaa na Zitto
Sijui kama una ordhodha ya wajumbe wa kamati kuu na halmashauri kuu kuthibitisha zaidi hoja yako.
Sijui kama wabunge ni sehemu ya viongozi au la, na kama ni hivyo uwiano upoje

2. Kabla ya mwaka 2010 hakukuwahi kuwa na mbunge wa upinzani kutoka mikoa ya kusini. Hadi leo Mtwara haina mbunge wa upinzani kama kumbu kumbu ni sahihi. Pengine ungejiuliza kwanini mikoa hii ni ngome ya CCM na utawezaje kupata wanachama wenye sifa kama hawapo ndani ya chama kwa kuanzia.
Kumbuka wabunge wa kuteuliwa si wabunge wa taifa ni wabunge wanaotokana na uanachama wa vyama vyao.

Pia uende mbali na kujiuliza kwanini umezungumzia Mtwara na Lindi na siyo Ruvuma , Kigoma na Singida.

3. Hilo la kuhusiana na big fish nalo pia naweza kukuuliza vipi umeshangaalia chama tawala kama ni tofauti? na kama ni sawa kwanini tusidhani mfumo wa demokrasia una tatizo sehemu fulani bali tuchague chama kimoja? Je, inawezekana umechukua CDM kama sample ya tatizo unalokusudia kuli address au ndio ukweli ulivyo?

4. Ulitakiwa uonyeshe mwelekeo wa kikabila pia. Kusema kina mwelekeo bila kuwa na takwimu kunavunja nguvu ya hoja hii.
Ninaweza kusema CDM ina mwelekeo wa ushemeji nikawa sawa kama wewe na sote tukawa sahihi kwasababu ndivyo tunavyoona. Lakini basi, je ndio ukweli wenyewe. Je, tuna takwimu za kuonyesha madai hayo?

Ni katika senti sumuni tu
 
kazi nzuri sana

"Tunapopongeza juhudi zao hizi tunahitaji pia kuwapongeza wakuu wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wa kutong'ang'ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu."
 
Sera ya majimbo ni ya kibaguzi kvipi?na uchaggani kungekuwa na rasilimali kama mafuta na madini si ndo mngechonga sana na uongo kuukolezea?Ujinga ni kuhakikisha rasilimali zinawanufaisha wananchi wanaotokea maeneo hayo?Sera ya majimbo kwa maoni yangu ni kama kurudisha madaraka kwa wananchi.
Tena sera ya majimbo ilitakiwa ifurahiwe zaidi na watu wa Mtwara na kwingineko kwenye mali asili kama gesi,dhahabu nk
 
Usitatizwe na wapuuzi wanaopotosha ukweli. ccm wanatafuta mbinu nyingi kuididimiza chadema kwa kutumia ukabila na udini kama mtaji. Mimi ni Mnyiramba naichukia ccm kwa kuwagawa watanzania kwa dini zao. Mwenyekiti wa chama hiki alipokuwa Mzee Makani ccm waliimba wimbo wa udini weeeee, baada ya Mbowe kuingia Ukabila ukashika kasi, nashukuru watanzania wamewapuuza chama linasonga mbele

"Tunapopongeza juhudi zao hizi tunahitaji pia kuwapongeza wakuu wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wa kutong'ang'ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu."
 
Hii dhana kuipinga ni ngumu sana na ndiyo kirusi kinachoitafuna Chadema.
 
Chama hiki kimejipambanua kuwa ni cha wachaga kwa kuzingatia mambo yafuatayo:
1. Viongozi wakuu wa juu hawakuchaguliwa kwa sifa bali ni kwa kabila lao. M/kiti, mtunza fedha akina mnyika. Makatibu wengi wa mikoa ni akina kilewo, munisi, kiwia
2. Kati ya wabunge 25 wa kuteuliwa hakuna wanaotoka mikoa ya kusini ya mtwara na lindi kama wapo tutajie
3. Asilimia kubwa ya wabunge wa kuteuliwa ni wachaga au watu wanaousiana na big fish kama vile rose kamili, dada yake lisu n.k.
4. Kwenye chadema sio tu chama cha kikabila bali ni chama chenye mwelekeo wa kifamilia.
Kweli kabisa mkuu hapo umenena kama hawaoni hili kama ukabila au ufamilia basi dhana hizo zimewakaa sana akilini mwao hivyo wanaona jambo dogo tu.
 
Kuna watu wanafurahia Mh Mbowe kuondoka kwenye nafasi ya Uenyekiti,kuna wanaotaka hata kuandamana ili aondoke,je chama ni cha kikabila kwasababu tu kwamba mwenyekiti ana kabila?Kwahiyo mwenyekiti akiwa mgogo basi chama ni cha kigogo?

Kuna anayeweza kuniambia ukabila uko wapi kwenye chama cha cdm?Je ni kweli kuwa mwenyekiti mchagga akiondoka ndo chama kitakuwa si cha wachagga?Ili linanitatiza sana tu!

Kwa taarifa yako katika kujaribu kuikataa hii propaganda, CDM watawaweka Waislamu ambao sio wachaga kwenye nafasi za ZZK na Arfi hata kama kutakuwa na wakiristo/wachaga wenye vigezo zaidi ya vya hao watakao kuwa wamechaguliwa.

Baada ya hapo wewe mwenyewe utakaa ujiulize wanataka kujustify nini?
 
Huu ni uongo,uko kwenye kamati kuu?Na uliweza kuingia kwenye kikao hicho kwasababu wewe ni mchagga ama mkristo?Zitto alisema nini hadi akaambiwa maneno hayo na Mbowe?Ccm mna mpaka viongozi waganga wa kienyeji.Wengine walikamatwa wakiwanga bungeni,kwahiyo tuseme basi ccm ni chama cha kichawi.

Ulichouliza nimekujibu kuamini au kutokuamini ni kwako.
 
Kwa taarifa yako katika kujaribu kuikataa hii propaganda, CDM watawaweka Waislamu ambao sio wachaga kwenye nafasi za ZZK na Arfi hata kama kutakuwa na wakiristo/wachaga wenye vigezo zaidi ya vya hao watakao kuwa wamechaguliwa.

Baada ya hapo wewe mwenyewe utakaa ujiulize wanataka kujustify nini?

Direct to the point,kwa hiyo Bwana Mushi kama unahitaji ushahidi juu ya hilo subiri uteuzi wa kujaza nafasi hizo ndani ya Chadema,Chadema wataprove hilo wenyewe.
 
Hili la LEMA kumfukuza Zitto CHADEMA ndio limedhibitisha uchaga unatawala CHADEMA.
 
Back
Top Bottom