permanides
JF-Expert Member
- May 18, 2013
- 11,682
- 14,241
'little knowledge is a poison of truth' kuna watu wanaoituhumu chadema katika misingi ambayo ni ya uongo na yenye lengo la kupotosha ukweli. Kwa mfano watu ni chama cha kikristu. cha wachagga na zaidi cha kikanda.Ni vizuri watu wajue kuwa kwa muda mrefu kanda ya kaskazini imekuwa na dhana za upinzani kwa muda mrefu. Hili liko wazi kwani mbunge wa kwanza wa upinzaji alitokea mbulu tena wakati wa nyerere. Upinzani mkubwa pengine katika level ya kitaifa ni pale Mrema alipogombea uraisi kupitia NCCR-MAGEUZI. CAF ilikuja lakini upoteza umaarufu kwa muda mfuupi, huku kambi zake ikiwa ni Zanzibar na ukanda wa bahari ya hindi. Chadema nayo ndio ipo sasa. Kutokana na ukweli kwamba chadema ilianzishwa na watu ambao katika maeneo wanayotekea dhana ya upinzani ilikuwa imeeleweka tayari,hivyo ikawa rahisi kupata watu wenye sifa na uwezo wa kufanya makumu maalum katika chama.Lakini baada ya operations za mikoani watu wameelewa dhana ya chadema na ndio maana hata viongozi wamewanza kutoka katika maeneo mbalimbali ya nchi. Na jee mbona sijawasikia watu hawa wakisema Cuf ni chama cha kiislam kwa sababu viongozi wake wengi ni waislaam? au CCM imekuwa na majina kama mwinyi, karume,makamba, mnauye na jee tuseme hiki nacho ni chama cha kifamilia? naomba kuwasilisha