Dharau gani uliwahi kuonyeshwa ugenini?

Dharau gani uliwahi kuonyeshwa ugenini?

Kuna principle moja naona ni nzuri, ukiitumia ndani kwako inaweza kupunguza matatizo madogo.

Akitaka kuja ndugu yangu, ampigie wife kumwambia anategemea kuja, mimi hata asiponiambia akanishukiza sina shida, ila wife ajue mapema...inapunguza maneno.
Nakweli binafsi sipendi suprise..unaambiwa tu fulani yuko njiani hapo bado 2 hrs afike sjandaa chochote wala pa kumlaza sjui ..taarifa muhimu hasa kwa mke mama mjengo
 
Kipindi kile ukimwi ndio umeingia watu bado walikua wanajua Ni gonjwa hata mtu akikaa karibu unaweza kuupata. Baasi bwana, Yuko dogo mmoja aliukwaa akiwa Nyanda za juu kusini wakati kwao Ni Mwanza. Kipindi kile hakuna usafiri wa moja kwa moja toka kusini Hadi Rock City, inabidi uje mpaka Dar kwa sisi wajanja ndio ununue tiketi ya train uende Mwanza.
Dogo alivyofika Dar alifikia kwa ndugu zake Oysterbay, ndugu zake walipomcheki na kuona Hali yake walipeleka godoro servant quarter ambàko walikua wanafugia mbuzi na kumpa dogo hifadhi huko huko kwenye chumba jirani nachumba Cha mbuzi.
Kwa dharau Ile dogo hakuchukua round.
 
Sijui ni tabia yangu au laa,spendi kwenda kwa watu hata ndugu zangu tuliozaliwa nao,japo zamani kwetu tuliishina ndugu wengi sana
 
Nashukuru mpaka utu uzima huu sijawahi kwenda kwa watu nikadharauliwa,labda ni vile na sisi kwetu ilikua kama jalala kila ndugu ilikua lazima aje kwetu kulilia shida zake na wazazi wetu waliwatreat vizuri tu.
 
Sijui ni tabia yangu au laa,spendi kwenda kwa watu hata ndugu zangu tuliozaliwa nao,japo zamani kwetu tuliishina ndugu wengi sana
Una tatizo somewhere mkuu..it's either mchoyo au something else
 
Back
Top Bottom