Dharau gani uliwahi kuonyeshwa ugenini?

Dharau gani uliwahi kuonyeshwa ugenini?

Huwa nashangaa hadi wanaume kuwa na tabia za kimama kwa wageni,hata kama humtaki mpe muda ndo umzingue lakin hata wiki haijaisha mwanaume mzima unanuna
 
Huu Uzi ni Kwa wasio na Hela tu wataujibu vizuri maana dharau huwa zinawafuata hata mijusi ikikaa juu ya mti inawadondokea Kwa dharau
Na ni kweli, ukiwa vizuri kiuchumi utakaribishwa vizuri sana, na kwanza huko ugenini utaendaje kulala zaidi ya kupita tu..

Shida ni sisi kina kajamba nani unaenda ati utakaa siku mbili tatu(hizi siku hazinaga mwisho)..
Mwenyeji anajua kabisa hili zigo hili
 
Kuna principle moja naona ni nzuri, ukiitumia ndani kwako inaweza kupunguza matatizo madogo.

Akitaka kuja ndugu yangu, ampigie wife kumwambia anategemea kuja, mimi hata asiponiambia akanishukiza sina shida, ila wife ajue mapema...inapunguza maneno.
Nakazia hapa
 
Mgeni alikua anakula mtoto akamwambia Mama huyu mgeni anakula sana mchele wetu utawahi kuisha 🤣
Hii ilinikuta,mtoto aliniambia napakua chakula kingi,ni miaka mingi imepita ila inanikata sana nikikumbuka.
Sisi Huku kijijini wageni wakija tunawahudumia vizuri tatizo ni sisi tukija huko mjini
Kweli kabisa
 
Mimi huwa ukinionyesha dharau nakutunzia najua ipo siku utazihitaji na lazima nikurudishie.!!
 
Back
Top Bottom