Dharau gani uliwahi kuonyeshwa ugenini?

Dharau gani uliwahi kuonyeshwa ugenini?

Ugenini Jamani kuna mambo Mengi sana. Na si ajabu unapoenda ugenini ukakutana na majanga tofauti tofauti.
Ugenini kuna watoto waliokosa adabu, ugenini kuna watu wasiopenda wageni anaweza kuwa mume au mke.
Unaweza kufika ugenini kumbe mmoja hana taarifa ile tu unaingia unaona watu Hawana furaha.
Kuna ndugu yangu aliwahi kunisimulia kuwa alikwenda mahali kumsalimia Shangazi yake.Mawasiliano yote alikuwa akifanya na Shangazi yake.
Mara baada ya kuwasili tu nyumbani na hata hajaingia ndani mume wa Shangazi yake anauliza huyu kijana amekuja kufanya nini hapa?
Chagua moja niondoke mimi au aondoke shangazi yako?
Mwenye Shangazi yake akakaa Kimya na kuendelea kumwandalia mgeni Chakula.
Anaeleza kuwa hakujisilia vizuri.
Wewe ulikumbana na nini ugenini?
Mkuu hiyo Stori ya shangazi mimi ndiyo niliyeleta kisa hicho Kwa kweli sitokuja kusahau over my died body. Yaan mgeni Mme WA shangazi anauliza mmemtoa wap huyu mgeni! Mtoto akajibu ndugu Yake na mama, Mme anajisemea tena yaan analetaleta watu ovyoovyo Tu😭😭😭😭😭yaan mm WA ovyoovyo😭😭😭😭😭😭😭
 
....nilikuwa na njaa sana ,mgongoni nina begi la madaftari ,nilipoingia pale uwani ninamuona shemeji anaweka sinia la ubwabwa chini katika mkeka huku akifuatwa na binti yake mdogo mkononi akiwa na bakuli la mboga,aliponiona tu alikunja uso na akaitikia salamu bila ya furaha na kugeuka haraka mlango wa kuingia ndani na lile sahani la "ubweche"..roho iliniuma mno huku nikiwa na njaa na kiukweli nilipitia hapo kwao kwa lengo la kupoza njaa yangu....

Imepita miaka zaidi ya 10...amesahau ila nikiwa nacho shida zake ndogondogo ninamtatulia....

#Tutende Wema ,Kesho ni fumbo[emoji7]
 
Inasikitisha kwakwel
 
Ubarikiwe sana
 
Hata sitaki kukumbuka dah! Wenye wtoto jitahidini kulea watoto wenu wenyewe na sio kwa kuwaacha kwa ndugu au jirani . Mambo mengine hata nikikumbuka ni kama childhood trauma. Very disturbing kwa kweli.
...am sorry [emoji7]
 
Beki tatu aligoma kunifungulia mlango. Na mabegi yangu nikatamani nigeuze sema ilikua mbali mkoa.
Kaniambia boss wake kamwambia asimruhusu mtu kuingia ndani.
Nilikaa nje ya fence mpaka mwenyeji wangu alivyorudi kutoka job ndio nikazama ndani.
..hana kosa
 
Kuna jamaa yangu akiwahi kuniambia kipindi akiwa dogo hivi mzee wake alikuwa mkoloni kweli alikuwa haangalii ni ndugu zake (mzee) au wa mke wakija ni wanalala kwenye mkeka na kila siku nguna ngumu na dagaa , unaambiwa ndugu walikuwa wakikaa siku nyingi ni mbili wanaaga 😁
Noma sana mkuu😆
 
Back
Top Bottom