Nimesoma majibu yako naona umeitumia nyundo kuua sisimizi mkuu
Simba hana na hata kuwa na uwezo wa kumbeba yanga kimataifa kamwee anacho fanya simba ni kuvuna pointi za kuwezesha timu 4 kwenda kimataifa
Sasa inabaki juhudi ya hizo timu kuhakikisha zinashika nafasi 1-4 (hapa wanagombania na simba pia) sasa unapo sema anazibeba/anaziwezesha anazipa pointi kufikia zile nne bora
Yeye anatengeneza nafasi tu atakaye kuwa Kati ya 4 bas anaenda
Hapa kwenye viporo nimecheka sana kwamba wazungu waige huu upumbavu (hujui viporo ni njia ya kupanga matokeo)
Umenifurahisha kuweka mfano wa simba iliyo mfunga al ahly kupigwa na dodoma jiji nani? Aliyekwambia haiwezekani kwani ruvu hakumpiga simba kwani kufanya vibaya mechi za awali ndo kunafanya usifanye vyema mechi kubwa mkuu unazungumzia soka/mpira ama wazungumzia ndondo/kabumbu
Labda uzungumzie simba hawezi kuibeba yanga kwasababu yanga haibebeki tumejaribu hata kwa mbeleko ya chuma lakini bado yanga inateleza
Mtu kukupa kazi ni msaada pia, huwezi kusema hujapewa msaada eti kwakua wewe ulitaka upewe hela, umepewa kazi ufanye na ndani ya hiyo kazi ndio kuna hiyo hela unayoitaka, juhudi zako na ustahimili wako ndio utaokuweka karibu na hizo hela.
Kuibeba yanga sio kuipa point, kubebwa nako zungumzia mimi ni kushiriki mashindano ambayo yamesababishwa na timu nyingine kufanya vizuri. Hayo mashindano mngeyatumia vizuri mgepata hizo points ambazo saizi unaziona cake
Hivi kuna mzungu gani mjinga huyo ambaye ana imani kama zenu kua viporo ni mbinu za kupanga matokeo?
Kwamba yanga ikiwa na viporo nane ambavyo inacheza na tp mazembe, al ahly, zamaleki, kaizer chiefs, mamelody, zamaleki, simba, pyramids nk. kuna mzungu anaweza kukubali kua yanga anaandaliwa ubingwa kwa viporo hivyo vya mechi?
Na wakati huo huyo mzungu anajua kua mechi yenu na ken gold mlishinda kwa penalty huku mkiwa mmekamiwa vibaya, na ken gold ni timu ya umiseta kule chunya
Bro ifike wakati utani uwekwe kando tuzungumze uhalisia, simba inayomfunga al ahly sio ya kuitafitia sababu kua inabebwa na TFF ili ichukue ubingwa. Al ahly mpaka anapaki basi nyumbani kwao sio jambo la kitoto halafu tukimfunga dodoma jiji we unasema tuna pangiwa matokeo??
Ebu nihakikishie kwanza kama hiki unachoandika hapa sio utani?
Kwamba unajenga hoja ionekane simba kumfunga al ahly ni kawaida, ila simba kuifunga dodoma jiji kwenye viporo iwe ni kubebwa bmna TFF huh??