Dhuluma na wizi unaofanywa na kampuni zinazokopesha bodaboda (pikipiki)

Dhuluma na wizi unaofanywa na kampuni zinazokopesha bodaboda (pikipiki)

Habari wana jamvi.

Kuna baadhi ya KAMPUNI za kukopesha BODABODA (mkihitaji sana nitaitaja).. kuna tabia ya DHULUMA, utapeli au UWIZI naweza sema inafanya kwa vijana wa tanzania... Kila kijana anaye kopa PIKIPIKI kwenye hizo KAMPUNI pale anapo maliza deni, watu 9 kati ya kumi ambao nimekutana nao ndani ya mwezi wanalia PIKIPIKI zao zimeibiwa. Na pia wakati mwingine hat wale waliokaribia kumaliza madeni mathalani mwezi 1 au miwili wanakumbwa na adha ya PIKIPIKI kuibiwa.

PIKIPIKI mkopaji anapochukua inakuwa na GPS, ambayo imewekwa na KAMPUNI. Lakini mteja akitala kujua namna GPRS ilivyo wekwa au mteja aweke mwenyewe, KAMPUNI inakataa inasema mteja anaweza kimbia na chombo, ilihali mteja anawadhamini na pia kaweka rehani baadhi ya mali na pia kuna barua ya serikali ya mtaa..

Kinacho nishangaza said, PIKIPIKI ikipotea ama kuibiwa, masaa 2 mengi ukienda kuitrack hazionekani, na pia ukiwafuata KAMPUNI wanakwambia wewe sio mteja wetu tushamalizana ma wewe.... Ukienda polisi napo hakuna msaada zaidi muwakilishi wa KAMPUNI akipewa wito wa polisi anapiga simu kituoni yanaishia kwenye simu tu na mteja akijitahidi kufuatilia sana.. kauli anazopewa polisi ni sawa sawa na majeruhi aliye gongwa na gari na akasahau kusoma pret namba ya gari iliyo mgonga.

MASWALI YA KUJIULIZA.
* GPS wanaweka KAMPUNI hata mteja hajui, PIKIPIKI inapo ibiwa tu! Dakika chache GPS haisomi.

* Ukitoa taarifa ushirikiano haupati kutoka kwenye KAMPUNI.

* Kwanini wateja wakimaliza mkopo au wanaokaribia kumaliza, asilimia kubwa huibiwa.

* Kwanini polisi hawachukulii seriouse sana malalamiko ya KAMPUNI hiyo ilihali yanatokea mara kwa mara...

Ifike wakati basi hata watu wawe na hofu ya Mungu... Na

pia serikali iwe inafuatilia mienendo ya KAMPUNI inazozisajili na ikitokea ulakini na ikathibitisha inazifungia tu. Maana zinazidi kuongeza umasikini kwa vijana wa Tanzania...

Kwenu ninyi vijana wa tanzania... Hebu mjitambue.. mkiona sehemu kuna shida, achaneni napo ili washindwe kuendesha biashara wafunge.. hiyo itakuwa fundisho hata kwa KAMPUNI mengine watakuwa waaminifu katika huduma zao. Maana itakuwa katika ikili zao kuwa ukiwa mdhulumati tanzania hufanyi biashara....

Wenu Mzee wa old school, ambaye kwa akili zangu timamu niliyeamua kutumia elimu yangu na maarifa aliyonipa Mungu kusaidia uma wa watanzania kujitambua...

Cc GENTAMYCINE
Robert Heriel Mtibeli na watanzania wengine mliopo jamvini na msiokuwepo
Ukifunga GPS yako kwa matumizi yako inakuwaje?

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Mule mule....
Hao mimi niliwakopaga simu bahati mbaya ikapotea ndani ya miezi mitatu. Wakaniambia niendelee kulipa watanipa nyingine, nikauliza kuna makubaliano rasmi tunafanya! Wakasema haa we endelea kulipia tu ikifika muda fulani tutakupa simu nyingine.
Nikasema sawaaaaaaa ndugu zangu.
 
Hao mimi niliwakopaga simu bahati mbaya ikapotea ndani ya miezi mitatu. Wakaniambia niendelee kulipa watanipa nyingine, nikauliza kuna makubaliano rasmi tunafanya! Wakasema haa we endelea kulipia tu ikifika muda fulani tutakupa simu nyingine.
Nikasema sawaaaaaaa ndugu zangu.
🤣😂😁
 
Hao mimi niliwakopaga simu bahati mbaya ikapotea ndani ya miezi mitatu. Wakaniambia niendelee kulipa watanipa nyingine, nikauliza kuna makubaliano rasmi tunafanya! Wakasema haa we endelea kulipia tu ikifika muda fulani tutakupa simu nyingine.
Nikasema sawaaaaaaa ndugu zangu.
Pole sana... Walikupa sasa?
 
Inasikitisha sana pale mhimili muhimu sana wa kulinda usalama na mali za wananchi unakua hauna msaada wowote kwenye kesi zilizo wazi kama hizi.
Pia wana bodaboda anzisheni umoja wenu kama haupo, mjipange vizuri kulinda haki na maslahi yenu. Wale wauzaji wapuuzi wawekeeni vikwazo mpaka warudi mstarini.
 
Kwahiyo suluhisho ni lipi hapo kwa sisi tunaokaribia kumaliza mkopo wao?
Funga GPS yako kisiri siri.. na pia usilaze PIKIPIKI sehemu unayo lazaga sikuzote au sehemu iliyo zoeleka.. naweza kwenda hata nje ya mkoa sehemu ambayo hakuna ofisi zao..... Deni likiisha siku wana kutumia sms ya kufuata kadi unakaa kwanza siku kadhaa afu unaenda kwa kushtukiza.... Unachukua kadi na unatoa kifaa chao.... Hapo utakuwa salama....
 
Poleni sana. Nadhani kwenye kipengere cha mkataba waongeze sehemu ya kuondoa hyo GPRS ikiwa mtu atakaribia kumaliza mkataba na zimebakia asilimia hata kumi au akishamaliza asilimia zote basi hyo gprs iondolewe
 
Back
Top Bottom