Dhuluma na wizi unaofanywa na kampuni zinazokopesha bodaboda (pikipiki)

Ukifunga GPS yako kwa matumizi yako inakuwaje?

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Mule mule....
Hao mimi niliwakopaga simu bahati mbaya ikapotea ndani ya miezi mitatu. Wakaniambia niendelee kulipa watanipa nyingine, nikauliza kuna makubaliano rasmi tunafanya! Wakasema haa we endelea kulipia tu ikifika muda fulani tutakupa simu nyingine.
Nikasema sawaaaaaaa ndugu zangu.
 
🤣😂😁
 
Pole sana... Walikupa sasa?
 
Inasikitisha sana pale mhimili muhimu sana wa kulinda usalama na mali za wananchi unakua hauna msaada wowote kwenye kesi zilizo wazi kama hizi.
Pia wana bodaboda anzisheni umoja wenu kama haupo, mjipange vizuri kulinda haki na maslahi yenu. Wale wauzaji wapuuzi wawekeeni vikwazo mpaka warudi mstarini.
 
Kwahiyo suluhisho ni lipi hapo kwa sisi tunaokaribia kumaliza mkopo wao?
Funga GPS yako kisiri siri.. na pia usilaze PIKIPIKI sehemu unayo lazaga sikuzote au sehemu iliyo zoeleka.. naweza kwenda hata nje ya mkoa sehemu ambayo hakuna ofisi zao..... Deni likiisha siku wana kutumia sms ya kufuata kadi unakaa kwanza siku kadhaa afu unaenda kwa kushtukiza.... Unachukua kadi na unatoa kifaa chao.... Hapo utakuwa salama....
 
Poleni sana. Nadhani kwenye kipengere cha mkataba waongeze sehemu ya kuondoa hyo GPRS ikiwa mtu atakaribia kumaliza mkataba na zimebakia asilimia hata kumi au akishamaliza asilimia zote basi hyo gprs iondolewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…