Diamond aachia wimbo mpya "Acha nikae kimya"

Akae kimya yeye ila wengine tutaendelea kusema kwa kuwa taifa ni letu na si la watu wachache.

  • VYETI FEKI
  • BENI YUKO WAPI?
  • WAKUNA ROMA WAKO WAPI?
  • UTAWALA WA SHERIA.
Mkuu hujamuelewa haja kaa kimya kasema chochote ila katumia akili kwenye wimbo huu namna yakufikisha ujumbe wake
 
uhalisia upi ww? acha pumba
 
Kusema ukweli hapa Diamond kachochora. Na huyo jamaa aliyemtumia kwenye cover hanaga desturi ya kukaa kimya kwenye vitu vya kipumbavu kama hivi vinavyoendelea.
 
Jitu lina familia yake alafu kulialia eti mama kaniambia,ndo majitu yanayoahribu ndoa hayo,badala ya kuskiza ushauri toka kwa mkewe linaskiza ushauri toka kwa mama;sasa si liachane na Zari libaki kwa mama?Mi toto ya kiswahili bhana!
Akili zako umezikalia au zimeondoka na mvua za juzi?
Umeisikiliza wimbo na kutambua kuwa amekaa kimya??
In fact hajakaa kimya!
 
Lakini kiuhalisia kaimba vizuri sana, kaonesha hisia zake juu ya sakata LA yanayoendelea sasa nchini!
Amefanya vema, wanamuziki au wasanii wengi huonesha hisia Zao katika kazi zao za sanaa. Theme ya wimbo huu umebebwa katika beti ya mwisho. Amefanya vema sana kama utajaribu kum judge pasipo kuweka mapenzi au chuki juu yake.
 
Hivi huu wimbo mmeusikiliza kwa umakini na kuutafakari kweli wakuu?? Maana inawezekana bado kuna shida katika kuuelewa vizuri na maudhui yake lakin mimi naona ni wimbo mzuri tu ila ndani yake una direct and indirect themes.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…