Rutorial k
JF-Expert Member
- Jun 8, 2014
- 960
- 855
niwazi kuwa art is subjective...yaani kila mmoja huja na interpretation yake jinsi alivyoelewa kazi ya sana....hilo liko wazi...tatizo la diamond ni undumilakuwili( neutrality) ila ney alichagua wapi pa kusimamia....diamond haijulikani either anapinga vyeti fake au anavisapoti..kwa muktaza huu lazima alaumiwe tuu hakuna namnaDiamond anaweza kuwa kachemka kama unavyodai.....lakini unamuona kachemka kwa kuwa amekwenda kinyume na matarajio ya nafsi yako.......
Msanii ney wa mitego hivi karibunu ametoa maoni yake kupitia wimbo wake unaoitwa wapo......ni moja kati ya nyimbo zinazopendwa sana ingawa unaonekana kuwa na mashairi yenye kejeli kama sio matusi kwa viongozi......Ney ameutoa wimbo huo hali ya kuwa anajua kuwa kuna chuki kubwa au mitazamo mibaya dhidi ya serikali hasa ukiangalia mtiririko wa matukio ya hivi karibuni ndio maana amepata support kubwa nA hatakukamatwa kwake kulizua huzuni sana kwa wanajamii.....kwa kuwa ni kama vile msanii huyo ameyachukua maneno kutoka kwenye vinywa vyao.......lakini mwisho wa siku yanasimama kuwa ni maoni yake na ametumia uhuru wake wa kutoa maoni.......
Na msanii Diamond amefanya kama alichokifanya Ney wa Mitego....lakini yeye ametoa maoni yake kupitia wimbo wake lakini maoni hayo yamekwenda kinyume na utashi wa wengi hasa kwa wakati kama huu.....lakini kwa mtu aliyekomaa kifikra na kidemokrasia hawezi akatoka pozi kiasi cha kutukana kwani anajua kuaa tunaishi kwenye jamii yenye watu mchanganyiko na wenye mitazamo tofauti.....
Kama jamii hatuwezi kuwa na mitazamo inayofanana hata kwenye jambo linalofanana.....ndio maana pamoja na madudu ya CCM mpaka leo hii bado kuna watu ni wanachama wa kutupwa wa CCM na wako tayari kufa kwa ajili ya CCM....na wao wanapaswa kuheshimiwa kwa kuwa ni haki yao kufanya hivyo kama ambavyo wewe unavyoona una haki ya kuamua kuwa mwanachama wa chama chochote bila ya kubugudhiwa......
Bado nasisitiza kuwa msawazo kwenye jamii inatokana na wanajamii kuvumiliana na kukubaliana katika mambo mbalimbali ya kijamii......
Mungu ibariki Tanzania....