Diamond aachia wimbo mpya "Acha nikae kimya"

Diamond aachia wimbo mpya "Acha nikae kimya"

Diamond afafanua sababu za kuachia wimbo ‘Acha Nikae Kimya’

Diamond Platnumz ameachia wimbo wake mpya kwa kushtukiza uitwao ‘Acha Nikae Kimya.’ Wimbo unazungumzia masuala mengi yanayotokea sasa ikiwemo hofu iliyotanda baada ya Roma na wenzie kutekwa.

Ili Nchi ipate maendeleo inahitaji Upendo na Ushirikiano wa Wananchi na Serikali..Na Nikiwa kama Msanii, jukumu langu ni kuhakikisha natumia Hekma na busara kukemea jambo nilionalo haliko sawa ili lirekebishwe, lakini pia panapokuwa hakuna maelewano jukumu langu pia ni kupatanisha ili kwa pamoja tujenge nchi yetu kusudi wazazi wetu, watoto pamoja na familia zetu waishi kwa Upendo Amani na kufurahia nchi yetu…Na ndiomaana kwenye nyimbo nakwambia “MI NA WEWE WA TAIFA MOJA…KAMBARAGE BABA MMOJA….SASA TOFAUTI ZA NINI TUSHIKAMANE TUKAIJENGE TANZANIA”…
Unatakiwa utambue kuwa kila kiongozi ni Binadamu na kama wote tujuavyo, Binadamu hatujakamilika… hivyo katika nchi yoyote lazma wakati mwingine kuna jambo linaweza likawa haliko sawa, ila sisi kama wananchi tunatakiwa tutumie Hekima na Busara kwenye kufikisha ujumbe ama hoja zetu ili viongozi walieke sawa…Busara na Hekima itafanya viongozi watuelewe kirahisi na pengine mengi tuyatakayo tutimiziwe kirahisi… mfano mzuri, juzijuzi kupitia kipindi cha Clouds360 cha clouds Tv nlipopata bahati ya kuongea na Mh Raisi nilimuomba atufungulie Mabanda ya Chipsi na Bodaboda ziruhusiwe kufanyakazi hadi asubuhi maana zilikuwa nwisho saa 4 ama 5 usiku…kwakuwa nilitumia Hekima na busara kwenye Kufikisha hoja ama Ombi langu..alikubali na tukapewa ruksa na sasa hivi maeneo mengi ya Chipsi na Bodaboda yanafanya kazi hadi usiku mnene… hivyo tusikubali tu kulishwa Sumu za kuleta ugomvi kati yetu wenyewe kwa wenyewe eti Mara Tutukane mara sijui fanyeni hiki, wakati hata baadhi ya wanaochochea mambo hayo hawaishi Tanzania wanaishi Ulaya / Marekani / kifupi nje ya nchi…ikija kutokea bahati mbaya kimenuka wao watakuwa wanakula kuku kwa mrija huko walipo…halafu sisi na familia zetu ndio tutateseka na kuhaha kunusuru roho zetu usiku kucha.. Hatutaki makelele ya Uchonganishi mitandaoni, kama mtu kweli anauchungu na nchi na kweli akisemacho anamaanisha aje, na kwa pamoja twende sehemu husika kupeleka malalamiko sio kukaa kitandani kupost kuchochea Ugomvi kumbe anatuchora na kutufanya kama sie mataahira wake, anatupeleka mara kushoto mara kulia… Akikaa pekeake anatucheka kuwa sie wajinga wake katueka mkononi…

MY INTAKE; HUYU JAMAA AMEMPA DONGO DADA MANGE KIMAMBI!!
Hana jipya,huyu anajulikana move zake, awadanganye mapoyoyo!
 
Kuna Nyimbo Mpya katunga Diamond --FT CCM

--Kuna watu wanaacha kazi wanaongelea Vyeti

Sasa Ajira zipi Serikali imetangaza tangu 2015?

Private sekta biashara zimedorora, watu wamepunguzwa kazi

Ajira zinapotea Mahoteli yanapunguza watu kazi

Utalii umedorora

-- Amani ya nchi inapotea...kuna watu wanaandika kwenye mitandao

Je---Amani wakati watu wana njaa...watu wanakula wadudu...Kusema kuna njaa ni uchochezi...Amani ipo Diamondi wewe uliyeshiba

Uhuru wa kusema no, kuongea tu ni uchochezi

Vyombo vya habari vinavamiwa na mtutu wa bunduki

Bastola anatolewa mtu mkubwa kama Napeee...Je wewe masikini?

Watu wanatekwa na kupotea...Ben Saa Nane na Roma ex

Mikutano ya vyama vya siasa...Demokrasia iko wapi?

[HASHTAG]#freeroma[/HASHTAG]

[HASHTAG]#freebensaanane[/HASHTAG]
 
Diamond is just like...
2157313d54c05326fecc6e64491efcb3.jpg
 
Huyu domo siku izi Sijui anakula maharage ya wapi cjui hana washauri.......jimbo bayaaaaa alafu anaongea upupu tu.....kwa mara ya kwanza nashindwa kumwelewa huyu domo
 
unakumbuka remix ya Ccm number one? au umeshaanza kujisahaulisha
Alikua kazini hata wewe ungepewa hiyo tenda sidhani kama ungekataaa. Unataka kusemaje , unataka kuniambia CDM wanawalipa wasanii iliwatukane viongozi wa serikali? Msanii anaejielewa hatakiwi kukurupuka nakulaumu anapaswa kuitumia Sanaa bila kuegemea kokote namaanisha CCM wakifanya ujinga anawasema na UKAWA wakifanya ujinga anawasema vilevile sasa hii tabia ya kuona upande mmoja wanakosea na upande mwingine ndiyo malaika si yakisanaa ni yakisiasa zaidi.
 
Ndio anapotea kimuziki huyo..hayo maneno amwambie Mzee Kipara aliyewapiga mkwara watanzania wasiende kumuona mtanzania mwenzao Lema alipokuwa gerezani
 
Kufanikiwa huwa hakuleti elimu unabiki 4m4 tu na Elimu huwa haileti mafanikio pia ni juhudi zako tu.......Tatzo kubwa Ya elimu Yetu hailet uthubutu ambao diamond anao na Tatzo kubwa Ya uthubutu hauambatani sawa na uwezo wa kuanalyse situations kitu ambacho DIAMOND hana na hata kipata kamwe
 
Umeandika saana lakini umeshindwa kukumbuka kuwa diamond ni msanii! Na hapo ndo unaweza kupima ukubwa/uwezo wa msanii!
 
Back
Top Bottom