Diamond ajisalimisha Polisi baada ya kuvunja sheria za Barabarani

Hakuna lolote. Hakuna kampeni yoyote hapo.

Kwa nini na watuhumiwa wa madawa akina wema nao hawajapiga picha na Sirro??
 
Daaa nimechekaa saana yaani mtuhumiwa kapiga na picha ya pozi na polisi

Kaole sanaa group
 
Hakuna lolote. Hakuna kampeni yoyote hapo.

Kwa nini na watuhumiwa wa madawa akina wema nao hawajapiga picha na Sirro??
Yani kitendo chao cha kuwekwa ndani tayari ilikuwa kampeni tosha wewe huoni kuwa imesambaa hadi humu ndani ulikuwa mjadara mkubwa na picha juu.
Sasa angelipa faini tu akaondoka tungelijua wapi lakini hizo picha si unaona hata mwenyewe kazipost na ujumbe murua kabisa wa kutukumbusha kufunga mkanda tofauti na madawa kukamatwa kwao tu ilikuwa gumzo na watu wanaofanya walianza kaa chonjo.
Ila ingekuwa mimi ndiye nimepiga picha nikapost hata zisingekuwa na impact.
Ingekuwa mimi ndiye niliwekwa ndani kwa ajili ya tuhuma za dawa hata isingekuwa na impact and no body would have known labda watu wangu wa karibu.
Hii ndiyo tofauti ya mtu mashuhuri na wengine na ndiyo maana hata makampuni yakitaka matangazo yanatafuta watu mashuhuri japo wanawalipa pesa kubwa tofauti na wangemtumia mtu wa kawaida.
 
Jeshi la police linapotumika kutoa kiki kwa msanii.. Toka lini police wameanza kupiga picha na mtuhumiwa aliyeendesha gari bila kufunga mkanda?
 
Bahati yake.

Ila soon asipoitwa na kamishina mpya wa madawa basi ataitwa na Naibu Waziri.
 
Kwani hakujifunza kwa wale jamaa wa Itigi..!
 
Una akil sana aisee... Nimekusoma
 
...kumbe haka kademu kana roho ya kutu hivi;
..bora kamekula umeme kapumzike kaache udwanzi,
.blalfuu!
 
Wampeleke kwa mkemia mkuu apimwe mkojo na damu kwanza halafu waende nyumbani kwake wampekue chumba hadi chumba.
Mkuu....
Nawewe unakua muongo kiasi hiki[emoji45] [emoji45] [emoji45]
 
Hivi washitakiwa wote huwa wanapiga picha na Trafic officer
Au usaniii usanii tuu

Kwanini inaandikwa kwa Kiingereza au ndio lugha ya taifa
 
Siku na Mimi nikikamatwa kwa over speeding nitagoma kulipia eneo la tukio mpaka nikalipie makao makuu ili nipige selfie na Kamanda Mpinga over.
 
Mimi ni mshabiki wa muziki wa Bongo fleva na pia mshabiki mzuri wa Diamond. Najua nitakera watu wengi lakini kwenye ukweli wengi watanielewa ni kitu gani namaanisha.
Labda Diamond hajitambui kama yeye ni mwanamuziki mkubwa na anastahili kuwa na matendo mema kwa jamii. Sote tunajua kila tukio laa Diamond ni lazima vyombo vya habari viliandike. Hata kama akiachia ushuzi, lazima magazeti yataandika!! Nimesikitishwa sana na tendo la Diamond kukamatwa na Polisi wa Usalama Barabarani. Yaani mwanamuziki mkubwa kama yeye anafanya tukio la kuendesha gari barabarani huku ameuachia usukani na kucheza muziki!!
Sote ni mashahidi na tuliona jinsi ule wimbo wa Darassa ulivyoleta zahma kwa wale Vijana wa Singida. Hawa vijana walikwenda mung'anda na kunyea debe. Sijui hatma yao ikoje mpaka hivi sasa. Walifanya lile tukio kwa mzuka wa ule muziki wa Darassa na kwa bahati mbaya mwenye wimbo hakushirikishwa kabisa kwenye lile tukio. Darassa hakujua na wala hakuwatuma katika kuandaa lile tukio, hakutaka kutumia mbinu chafu ili kuupa kiki wimbo wa "Muziki". Ule wimbo ulijiuza wenyewe kwa kuwa unavionjo vya kupandisha mzuka, wimbo umepangwa kiufasaha.
Leo Diamond anafanya tukio la ajabu ili kuupa kiki muziki wake. Anahatarisha maisha ya watumiaji wengine wa barabara na familia yake ambao wote walikuwepo ndani ya gari wakati akilifanya hilo tukio. Lengo lake ni kuupa 'extra mile' wimbo wake wa "Marry You".
Hivi wimbo wake umekwama kuwavutia mashabiki mpaka anaamua kutafuta mbinu za ajabuajabu ili kuupa kiki wimbo wake? Atambue waungwana wanasema kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
Kwa hili tukio la kujitakia alistahili adhabu kali zaidi ya wale vijana wa Singida ili kuukomesha kabisa mtindo huu wa kuhatarisha maisha yake na viumbe wengine.
Si kwamba naandika ili kumkwamisha. Au namchukia. La hasha. Lengo ni kuwaasa wengine wasifanye mzaha au mambo ya ajabu ili kutafuta sifa za kijinga ili kutafuta umaarufu au kuongeza idadi ya mashabiki. Najua kuna watu hawatopenda haya maneno, lakini kwenye mambo yasiyofaa tuambizane ukweli!!



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…