Diamond alalamika baada ya show yake Ujerumani kuvurugika

Diamond alalamika baada ya show yake Ujerumani kuvurugika

tatizo lilianza saa tatu usiku baada ya kunusa cocaine akajioverdose,akalewa tikitiki,ikabidi wamfiche mpaka kilevi kimekuja kuisha saa tisa usiku si ndo wamkimbize mbiombio ukumbuni akatumbuize japo nyimbo 2.kumbe ikawa balaa zaidi.
 
bado hajafkia anga hzo za kimataifa aje apige shoo kahama kwani ndio kwenye viwango vyake.
 
bmpingo

Hapo ni kwenye parking ya magar mkuu. sio ukumbin
 
Last edited by a moderator:
sipati picha angemaliza show salama,vilaza lzm wangeenda airport kumpokea,chezea sifa ww!!!
 
Usiku wa Jumamosi Agosti 30, 2014, majira
ya saa 10 alfajiri, mwanamuziki nyota wa
Bongo Flavor, Nasib Abdul maarufu kama
Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya
hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,
Ujerumani, baada ya washabiki waliokuwa na
hasira kuchoka kusubiri show.


Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na
washabiki mjini Stuttgart, Ujerumani.
Mashabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi euro
25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show
ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta
wakisubiri hadi majira ya saa 10 alfajiri ndipo
mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na
promota wake raia wa Nigeria anayejiita Britts
Event.

Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa
hawakutendewa haki walianza kurusha chupa
na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond
na promota wake, Kilichowakera zaidi
washabiki ni pamoja na vyombo vibovu
vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho
kiliwafanya mashabiki kuvunja hadi vyombo
vya muziki, ma-Djs walishambuliwa na wapo
hospitalini kwa sasa.


Mmoja wa Djs hao alipoteza lap top yake,
mwanadada DJ Flor alipatwa mstuko wa moyo
na kukimbizwa hospitali, washabiki hao
walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi
hospitali. Polisi nchini Ujerumani
wanamesema tukio hili la aibu halijawahi
kutokea, kuwa msanii kuchelewa kufika
jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari
kwani washabiki wa Ujerumani wanaheshimu
sana muda wao.



Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa
onyesho hilo na wamesema wanachunguza
thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia
hizo na pia itamfungulia mashataka promota
huyo raia wa Nigeria ambaye pia
anachunguzwa kwa kujihusisha na mtandao
fulani wa biashara.


Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti hii…

http://www.stuttgarter-nachrichten.de/
inhalt.blaulicht-aus-der-region-stuttgart-31-
august-diamond-platnumz-zieht-aerger-der-
fans-auf-sich.ca1f4b9d-599b-4c95-84c8-
fe25d10b6ed9.html

SOURCE: Salim Kikeke facebookafans page via
taarifa.co.tz/2014/09/diamond-aokolewa-na-polisi-ujerumani/
 
Hizo gharama za uharibifu azilipe Ndomondi!

Hivi unawezaje kutembezwa kama zuzu usijue unatakiwa muda gani ukumbini?

Shida hapa ninayoiona ni Elimu tu!
 
Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na mashabiki mjini Stuttgart, Ujerumani.

Usiku wa Jumamosi Agosti 30, 2014, majira ya saa 10 alfajiri, mwanamuziki nyota wa Bongo Flavor, Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, Ujerumani, baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.
Mashabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anayejiita Britts Event.
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake, Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya mashabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki, ma-Djs walishambuliwa na wapo hospitalini kwa sasa.
Mmoja wa Djs hao alipoteza lap top yake, mwanadada DJ Flor alipatwa mstuko wa moyo na kukimbizwa hospitali, washabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospitali. Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio hili la aibu halijawahi kutokea, kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
Diamond Platnumz akiwapagawisha mashabiki wake katika moja ya maonyesho yake.

Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promota huyo raia wa Nigeria ambaye pia anachunguzwa kwa kujihusisha na mtandao fulani wa biashara.
Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti hii…
http://www.stuttgarter-nachrichten.de/inhalt.blaulicht-aus-der-region-stuttgart-31-august-diamond-platnumz-zieht-aerger-der-fans-auf-sich.ca1f4b9d-599b-4c95-84c8-fe25d10b6ed9.html
Na Blogu ya Wananchi.
 
Kilichotokea Stuttgart ni utapeli wetu sisi waafrika, ni kuwa Diamond alipatana na Promoter alipwe Euro 3250 kitu kama Tshs.mil 6.5. ila huyu Promoter alianza kumzungusha Diamond, na ndipo Diamond alipomwambia ,,mkataba wetu ilikuwa nipewe pesa nifikapo Airport, na mpaka sasa sijalipwa hivyo sitakwenda ukumbini mpaka nilipwe changu'' basi ikawa zunguka nikuzunguke mpaka mishale ya saa 1:30 (saba na nusu)usiku ndipo walipo mpatia kiasi cha Euro elf 3..Lakini Diamond aligoma mpaka apewe Euro 250 iliyokuwa imebaki na ilipotimia mida ya saa 3:30 (tisa)usiku ndipo kilipopatikana kiasi cha pesa kilichokuwa kimepelea (250) na ndipo walipokwenda ukumbini na kukuta mashabiki kimechacha....


Kumbuka kipindi cha nyuma kuna wabongo walitaka aje Ujerumani aliwambia wamkatie tiketi ya ndege first class, Hotel room presendetial suite na Euro 12,000 (mil 24) na pesa hatumiwe Tz.. Sasa cha ajabu hawa wanageria aliwakubalia kwa Euro 3,250 na Hotel ya kawaida.
 
Haya mambo ya kuleta U-Africa kwenye nchi za watu unaweza kujikuta unaumizwa alafu unapumzikia Lupango..., When in Rome do Like Romans.. By the way nadhani hio show wengi waliochukua ticket watakuwa ni wabongo wa huko.., ila nadhani uzalendo uliwashinda...,

Duh yaani saa nne mtu anakuja saa kumi this is beyond hata wanavyofanya huku Bongo.., kwahio alitaka apige mpaka saa sita mchana au ?
 
Saa nne hadi saa kumi.? Hii haikubaliki hata kidogo.
 
Jameni makosa yalikua ya waandalizi ila sio Diamond, mbona wengine mnatoa comments kana kwamba mna lingine dhidi ya jamaa.
 
Jameni makosa yalikua ya waandalizi ila sio Diamond, mbona wengine mnatoa comments kana kwamba mna lingine dhidi ya jamaa.
Hayo makosa ya wote ndio maana wote walikoswakoswa na Chupa.
 
Mie sijaona kosa la Diamond hapa, pengine ndio maana hata polisi hawashughuliki nae. Mwenye kosa ni muaandaaji wa hiyo shoo ndio maana hata hao polisi wanamtafuta muaandaaji na siyo Diamond
 
Back
Top Bottom