Usiku wa Jumamosi Agosti 30, 2014, majira
ya saa 10 alfajiri, mwanamuziki nyota wa
Bongo Flavor, Nasib Abdul maarufu kama
Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya
hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,
Ujerumani, baada ya washabiki waliokuwa na
hasira kuchoka kusubiri show.
Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na
washabiki mjini Stuttgart, Ujerumani.
Mashabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi euro
25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show
ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta
wakisubiri hadi majira ya saa 10 alfajiri ndipo
mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na
promota wake raia wa Nigeria anayejiita Britts
Event.
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa
hawakutendewa haki walianza kurusha chupa
na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond
na promota wake, Kilichowakera zaidi
washabiki ni pamoja na vyombo vibovu
vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho
kiliwafanya mashabiki kuvunja hadi vyombo
vya muziki, ma-Djs walishambuliwa na wapo
hospitalini kwa sasa.
Mmoja wa Djs hao alipoteza lap top yake,
mwanadada DJ Flor alipatwa mstuko wa moyo
na kukimbizwa hospitali, washabiki hao
walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi
hospitali. Polisi nchini Ujerumani
wanamesema tukio hili la aibu halijawahi
kutokea, kuwa msanii kuchelewa kufika
jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari
kwani washabiki wa Ujerumani wanaheshimu
sana muda wao.
Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa
onyesho hilo na wamesema wanachunguza
thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia
hizo na pia itamfungulia mashataka promota
huyo raia wa Nigeria ambaye pia
anachunguzwa kwa kujihusisha na mtandao
fulani wa biashara.
Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti hii
http://www.stuttgarter-nachrichten.de/
inhalt.blaulicht-aus-der-region-stuttgart-31-
august-diamond-platnumz-zieht-aerger-der-
fans-auf-sich.ca1f4b9d-599b-4c95-84c8-
fe25d10b6ed9.html
SOURCE: Salim Kikeke facebookafans page via
taarifa.co.tz/2014/09/diamond-aokolewa-na-polisi-ujerumani/