Hapa ni wivu wa watanzania uliokithiri, huu ni ugonjwa sugu wa watanzania usokua na dawa wala hospitali. Kutwa tuko negative na maendeleo ya wengine, kila mtu amesema aliloweza kusema kwa uwezo na upeo wake lakini kila ukiangalia ni wivu tu unawasakama. Diamond na mama yake hawakwenda shule ndio maana hafikirii nini afanye, nime quote mliyoandika. Nyie ambao vidato vimepanda hamkupaswa pia kuongea haya mnayoyaongea. Watu wasiosoma ndio wanaweza kuongea haya.
Kujenga au kuangalia kesho haihusiani na elimu wala darasa la mtu, bali akili na wito wa kufanya kile kitu. Sio Marehemu Kanumba au Diamond ambao wana pesa Tanzania na hawakufanya hayo mnayotaka, wako viongozi walioshika nyathifa mbali mbali kubwa tu na uwezo ulikuwepo lakini akili ya nitafanya kesho iliwatawala, walipoondoka madarakani walirudi kwenye vibanda vya wazazi wao vijijini bila chochote. Hawakua na nyumba wala magari ya kifahari waliyokua wanatembelea hapa mjini, hao ni wazee kabisa lakini hawakuangalia kesho.
Diamond na Marehemu Kanumba (RIP) bado hata 30 hawajafika, they still have time kama wana uhai na uzima.
Nitafurahi kama nyie ambao mmesoma sana mtatuorodheshea hapa rasilimali zetu tuzisome japo kwa uchache ili tujue na nyie wasomi mmefanya ya maana na mmeona kesho mkiwa bado vijana.
Acheni hizo, mpeni sifa Diamond pale anapostahili.