Unajua katika lugha yetu ya Kiswahili unaposema"...tena sababu zenyewe zikiwa hizi za text" maana yake kutumia sababu za text kumpiga mwanamke ndio vibaya zaidi. Kwa hiyo, aidha umetumia lugha vibaya na imesababisha nia yako isieleweke.
Au kingine, ambacho ndio ulichomaanisha, ni kwamba kuna sababu ya kumtwangia mwanamke inayoweza kuvumilika vumilika. Ambayo hakuna. Hakuna sababu nzuri ya kumpiga mwanamke, na kitendo cha kupigwa kwa Wema Sepetu kilaaniwe, na ma Zinjanthropus wa kike na kiume wanaosafisha tabia hii na walaaniwe.