kabanga
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 37,421
- 18,760
una maana huwa anafanya kazi ya upunda....??? unaweza thibitisha...???? nauliza tuSi unajua ni mwanamziki wetu nyota pia yuko karibu sana na Kinje.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
una maana huwa anafanya kazi ya upunda....??? unaweza thibitisha...???? nauliza tuSi unajua ni mwanamziki wetu nyota pia yuko karibu sana na Kinje.
-Kuuza Ringtones???? Statistic zipo???
-Kapiga show nyingi???? Statistic zipo???
-Endorsement Voda,Coca-Cola,GSM? ??? stats zipo??
Je hizo show alizopiga kuanzia 2009 za mil10 hadi sasa zinaweza kumpa mabanda yote hayo? Je nidhamu ya fedha ndio hiyo ya kufanya bday ya mil90? Kumbuka pia kuna fela,suka,tale na sallam ukiwaacha dancers na groupies.
Ni kweli mkuu maana ndiyo anatajwa kama msanii mwenye fedha nyingi.Haya maswali ni muhimu. Inawezekana anapata pesa kwa njia hizi, basi ni vyema ijulikane ili na wasanii wengine waige. Kusema jumla jumla haiwasaidii wengine kutoka. Kama kuna mtu anajua jinsi muziki ulivyomtoa Diamond kwa mauzo au matangazo, aisaidie jamii ili iige mfanowe!
Nilijua tu Chanzo lazima kitakuwa DAR.
Waandishi na Aibu ya Taaluma.
Waandishi wengi wa habari wanashindwa kuielewa,wao waangalie mfano kwa Madaktari
Wote wataitwa Madokta,ila kila mmoja ana specific profession yake.
Ila waandishi wetu hawa,unakuta mwandishi kama daladala,yaani yeye anaandika chochote tu bila kujua uwezo wake.
Mwaandishi wa Taaluma ya Michezo na Burudani(Sanaa kwa ujumla)lazima awe amesomea Sanaa,na Chuo Kikuu cha Dar wanatoa Degree ya masuala hayo kama sikosei,na kama nakumbuka vizuri Marehem Mzirai alikuwa anasoma Pale.Na Chuo cha Bagamoyo kinatoa Kozi nzuri sana ya masuala ya Sanaa na Uchumi,ambapo utashangaa pale unakuta Wazungu wanasoma ila waswahili na waandishi na wasanii wanapita kama polisi,wanenda kwa warsha tu na vi seminar vya kuzugia ili wapate certificate of attendance
Sasa Mwandishi lazima awe na taaluma.Sasa kwa akili ya kawaida,hivi unashindwa kufanya analysis tangu alipotoka Diamond mpaka leo hii na mafanikio yake?
-Na sio lazima kila biashara mtu aweke wazi,yale ni maisha binafsi,kuna watu humu hata wake zao na waume zao hawajui anapokea kiasi gani kama Mshahara.Na ni mwili mmoja,sasa itakuwa Diamond?
Maisha yanaanza kwa Shilingi moja,then inategemea umeiwekeza vipi.Wapo watu walianza na pesa za madafu tu tena milioni moja tu,leo hii ni milioneaz wakubwa na tunawaheshim.
Diamond ana nidham kubwa sana ya Pesa tena Sana.
Kwa mtizamo wa haraka unaweza kushangaa kwanini Diamond Jina kubwa halafu anahitaji Management?Jibu moja tu ni kwamba anajtambua na anajifunza kwa Wenzie Nje ya Nchi
Hivi Unajua Billionea Dangote,ni maarufu sana Nigeria,ila kuna watu wanaishi Lagos-Nigeria,hawajui kwamba Anakiwanda cha Cement Tanzania.
Sasa maisha ni akili,sio kila kitu mtu anadi.
Big UP Diamond,licha ya kwamba kanikera kuimba Nyimbo ya matusi matupuuu ya Salome(usiingie huku Diamond,matusi matupu hayo jua ni soft copy na mungu yupo na unaiacha milele).
Kamw kanzu haifanani na dera [emoji23][emoji23]
Nenda kitengo husika polisi ukareport upeleke na ushahidi wa uyasemayo, na kama unaona Diamond anafaidi kuuza Unga nawe kauze tukuone.Tuache utani maisha ya diamond hayalingani na kipato chake..... Biashara ya Pablo Escobar na El Chapo inahusika hapa
Sasa kama anajua kuna vyanzo vingine kwanini anauliza maswali yakitoto hivyo? Madhumuni ya makala yake ni yapi.Kuna kitu kwenye hii makala ambacho mwaandishi hajakifafanua tusiishie kusema mwaandishi hajui kama album hailipi,hata yeye amesema kuwa kuna vyanzo mbalimbali ambavyo vinaweza kumpatia msanii hela na pamoja na show.
Nategemea waandishi wa hizi habari ni wasomi either wana Masters, Degree or Dip.
Nasikitika kuona mwandishi anatoa hoja isiyo na utafiti wa kisomi, kumvutia msomaji.
Waandishi wa sasa msidhani elimu ya darasan tu inatosha kupima idea za hoja zenu mnazotuletea.
Nategemea kuona waandishi mnafanya taaluma kulingana na mabadiliko ya technology. Huwezi kumpima msanii wa sasa kwa kulinganisha na wa mwaka 2005 or back, mziki wa sasa sisi wa kuuza albamu kama fikra za huyu mwandishi.
ila kanzu bila barghashia ni dera tu!!😀
mnataka angebaki pale tandale alipokulia na mamake kama yule jamaa yenu wa kariakoo !!mngekua roho kwatuuu!!!eehh??Tuache utani maisha ya diamond hayalingani na kipato chake..... Biashara ya Pablo Escobar na El Chapo inahusika hapa
waandishi kama hawa ni miongoni wa wenye vyeti feki.wameungaunga were adi wakawa waandishi lakini kichwani weupe!!!Mwandishi ni kanjanja yeye anajua pesa inaingia kwa kuuza albamu tu, hajui kwamba digital system ndo inaingiza pesa nyingi mfano
- youtube views unalipwa
- miito kwenye simu unalipwa
- mirabaha nyimbo ikipigwa redioni hasa nje
- kufanya shows
- kufanya matangazo
- kuwa balosi wa kampuni
Vyanzo ni vingi sana ambavyo mwandishi hajui
How?Every TIME the Music played somebody get PAID!
Sure broAlbum hazilipi si kama zamani nilimsikia master Jay akihojiwa alisema kwa sasa soko la album halilipi, ila watu wanatoa kwa ajili ya kuipa hadhi na heshima mziki wake basi, zinazolipa sana ni tour na ndio maana msanii akitoa album faster tour zinaanza , ila soko album halilipi, labda hizo ring tone, ela inayotokana na airplay basi lkn TOUR ndio mpango mzima. Diamond platnumz mwaka huu amepiga show nyingi alikuwa na tour ulaya na sasa anatour ya Africa, tusiwe na mawazo kila anayefanikiwa ni muuza ngada au freemason kwani hayo ni mawazo ya kimasikini.
Mbona unaingiza maneno ambayo sijayasema mkuu?una maana huwa anafanya kazi ya upunda....??? unaweza thibitisha...???? nauliza tu
Na ndiyo maana nikasema mwaandishi hajafafanua,hajaeleweka nini alikuwa anataka kutufikirisha.Sasa kama anajua kuna vyanzo vingine kwanini anauliza maswali yakitoto hivyo? Madhumuni ya makala yake ni yapi.
Ingawa kuna ukweli lakini fans wake watakuparura we subiriSasa yeye mwandishi ambae kabla hajaandika anatakiwa kwanza kufanya utafiti na kutoa majibu kinyume chake ndo kwanza anakuja na maswali... sasa anataka amjibu nani?! Au ngoja mimi nimrahisishie--
- Jamaa anauza dawa za kuleya
- Freemason
- Anasafirisha meno ya tembo
- Illuminat
- (Nafanya utafiti kufahamu vyanzo vingine)