bayfe
JF-Expert Member
- Aug 13, 2013
- 548
- 255
Unajua nini kuhusu mahusiano ya watu na vyombo vya habari?Utadhani hili ni jambo la kawaida kwa msanii kutoka ardhi ya Tanzania akapewa heshima ya kutumbuiza uzinduzi wa mashindano makubwa kuliko yote Africa.
Diamond ameipa heshima Tanzania kwa kuwa msanii wa kwanza na pengine asitokee mwingine kutumbuiza uzinduzi wa mashindano ya AFCON. Lakini vyombo vyetu vya habari kimyaa kama hichi kitu ni cha kawaida. Sio blogs sio magazeti sio radio sio Tvs.
Wazalendo wa nchi hii tulitegemea hii habari iwe kubwa ili kuinspire hata wasanii wengine na vijana kwa ujumla. Lakini chuki roho mbaya majungu uswahili na utimu unatusumbua na kuturudisha nyuma wabongo.
Ndio maana Mrisho mpoto aliamua akaiwakilishe Kenya maana sisi wabongo buana!
Kuna tofauti gani kati ya utamaduni wa vyombo vya habari na utamaduni wa jamii?
Unafahamu namna na kiwango ambacho vyombo vya habari wanachuja habari na kuamua namna hadhira inavyopaswa kufikiri?
Unadhani ni kwa kiasi gani vyombo vya habari nchini vinauza utamaduni wa jamii kwa kuzingatia dhana ya biashara inayotawala vyombo hivi?
JIBU HAYO KWANZA KISHA NTAKUIBIA SIRI.