Sasa kukimbia nini hapa nifah? Kwanza ni post ya saa 9:18 PM nami ndo kwanza naiona 2:54 AM; karibu saa 6 baadae na kama usingeni-mention; wala nisingeiona simply because niliona notification yako na ya
atoto; nikaona hawa "wangu", ngoja ni-login nijue kulikoni... kwahiyo haina kukimbia bhana!!
Baada ya hiyo intro; nimesoma post husika... mbona naona kama ni wa kujibu ni mashabiki wa Ommy Dimpoz kuliko wa Diamond? Manake hapo Diamond kasema yake... wanaopaswa kujibu au kutetea ni mashabiki wa Dimpoz... lakini kwavile imezoeleka kwamba adui wa "adui" yako ni rafiki basi nilitarajia mashabiki wa Kiba ndio hasa wanaopaswa kujimwayamwaya kwenye huu uzi kuliko mashabiki wa Diamond!! Kwahiyo usishangae kutowaona mashabiki wa Diamond kwa sababu; hawana sababu ya kuja kwenye huu uzi na ndio maana ukiangalia... kama ni dongo la gizani aliyepigwa ni Dimpoz na yeye na watu wake ndo wanatakiwa kulia lia humu na sio mashabiki wa Diamond!!!