Kama ndivyo tunavyoishi kivipi Avemaria? Issue ni kwamba, mtu huwezi kuwa na control over someone else's maamuzi! Inawezekana unaishi na watu vizuri kabisa, wakipata matatizo au sherehe unahudhuria! Lakini bado haimaanishi kwamba na wewe ukipata matatizo wale ambao ulikuwa unaenda kuwa-support nao lazima watakuja kuku-support! Sasa hoja hapa ni kwamba, kama wewe ulikuwa unawa-support lakini wao hawajaja kuku-support, piga kimya mshukuru Mungu na sio kulalamika lakini tayari utakuwa umefahamu ni nani rafiki wa kwenye shida na raha na nani ni wa kwenye raha tu!! Hawa watu Avemaria, am certain hata huko kwenu wapo... kila mahali wapo! Wanapokuwa na shida unawa-support lakini ukipata wewe huwaoni... kwahiyo wala haina haja kusema "fulani nimepata tatizo wala sikumuona" ya nini... mwache tu!!Kama ndo mnavyoishi hivyo na kwenye jamii zenu basi hongereni.
Btw; unafikiri ni kwanini Diamond ameamua kujielezea? Hivi kweli kulikuwa na ulazima wowote wa kujitolea sababu?
Kwamba Diamond alikuwa na sababu ya kutolea ufafanuzi, kwa mtazamo wangu mimi wala hakuwa na sababu ingawaje nadhani kinachomsumbua ni ile kuona yeye ni public figure halafu watu wanaona hahudhurii matatizo ya wenzake! Ilitosha kabisa kutoa ufafanuzi wake kwa Dully, PERIOD! Lakini kubwa kuliko yote, si Diamond wala yeyote yule alikuwa analazimika kuwepo kwenye msiba huo... hapo ndipo nilipomshangaa Dully as if wasanii walikuwa wanalazimika kuwepo kwenye msiba wa baba ake! Yeye alitakuwa tu kuwashukuru wale waliohudhuria basi!