Hakuna aliewakataza kuwa na mahusiano mazuri na serikali, ambacho wananchi wamechafukwa nacho ni unafiki. Tumeona jinsi wanavyoibuka kutoa pole wakati waliofanya ukatili ndio hao hao waliowanadi na kwenda kutumbuiza kwenye mikutano yao ya kampeni.
Miaka michache kidogo nyuma diamond alikemea ukatili wa polisi uko Nigeria na kutoa rai kwa AU kuingilia kati, lakini safari hii suala hilo limefanyika nchini kwake kauchuna.
Dada ake diamond, quuen darling alienda mbali akasema yeye angekua Rais angepiga na kuvunja wote watakaoandamana, hopeful uko alipo moyo wake una furaha kubwa sana maana alichokitaka kimetimia