Diamond azindua Pafyum yake ya Chibu, bei yake ni balaa

watu wana maneno ya ajabu kweli kumbukeni ndo maana iphone simu zao siku zote bei zao ziko juu and bado wanapata wateja , issue ni price discrimination inavo tambua ubora wa bidhaa na hata wateja watakao tumia sio wale wachukua alafu kesho lawama za kutosha mitandaoni, Siku zote ukifuata hao mashabiki wa maisha ya chini tegemea kuwa wa low status tu, sababu kila kitu utafanya bei ya chini
 
We kama huwezi nunua kanunue vi kuruthumu vya 2000 buguruni. Watu wananunua pafyum mpaka 500,000 we unahanya na 105,000?
 
Price discrimination!!!! Sawa watoto wa tandale kashatukosa...ila asije kulazimisha zile za kwetu tunazo zimuda kama Casablanca ziuzwe nazo laki kama walivyotanya bongo muviiiii....[HASHTAG]#usinipangie[/HASHTAG]
 
Watanzania tunapenda kulalamika bila hata kujua bei inachangiwa na nini. Diamond ni International Artist, na anapotoa bidhaa si kwa kulenga TZ peke yake bali ni dunia nzima. Unategemea akitoa product yenye kiwango cha chini si atakuwa anajiharibia jina.
 
Bwana weeee, kama huna 105,000 nenda kibandani kanunue COBRA kwa 3,000
 
[emoji16][emoji16][emoji16] Leo Diamond amekuacha mpweke
 
Ubunifu bila plan ni upuuzi unazindua perfume unauza 105,000/=what is your target, inaamaana unafanya jambo bila kutazama nani unaekwenda kummuzia,mtanzania shabiki wa Diamond ana uwezo wa hiyo hela.
Jamani...kwani mmeambiwa mashabiki zake wote ni watu wa maisha ya chini???! Kwanini mnataka kumpangia bei wakati hajui amegharamia kiasi gani kwenye uandaaji na matangazo??! Besides, wapo watu ambao wanajichangaga na kununua perfume mpaka za laki 3-4 nyie mnalalamikia laki moja?!

Mwenye biashara ndo anaepanga bei. PERIOD!!!
 
Angejua kuwa washabiki wake ni mahousegirl hata asingeweka bei ya ivyo. Imekula kwake kama wema na vile vichupi na lipstick.
 
Unapakaje perfume. Si kwa kupulizia? Sasa wewe una perfume, chupa, mwenzio ana mtoko. Anataka kupuliza makwapa 2. Upande na upande. Si utampulizia mara mbili? Sasa kama kila kwapa ni shs 500. Atakupa shs 1000 kwa makwapa yote mawili.
[emoji3] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Aliamua kukaa kimya, akae tu...hata angeuza kwa shilingi mia...sinunui,huu siyo muda wa kucheka cheka na opportunist.
 
Big up sana.
 
Diamond amezindua rasmi pafyumu yake ya Chibu, itauzwa kwa bei ya 105,000 bei ya rejareja ameomba sapoti kwani anatoa ajirakwa vijana
Zitapatikana GSM Mall, Mlimani City, pia zitakuwa zikipatikana kwenye ndege

Safi nimeipenda hii tena angefanya hata laki 3 kabisa

Nasema hivi kwa sababu ingekuwa ya bei ya chini kila mtu angenunua matokeo yake watu mkitembea mnakuwa mnanukia harufu moja kila mtu kitu ambacho sikipendi

Bora allivyofanya hivyo,wale watanashati tunaojua kutupia tutanunua tu ila wale wazee wakuunga unga waendelee ni spray zao za buku 5 tano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…