Diamond azindua Pafyum yake ya Chibu, bei yake ni balaa

Diamond azindua Pafyum yake ya Chibu, bei yake ni balaa

Ila watu wa JF mnaongoza kwa kukatisha watu tamaa jamani khaaa!!!

Mshauri mtu kuliko kumponda,
Kama ww huwezi kununua wengine wanaweza na chenji hawadai.
 
bora useme maana ukisema unaonekana hater nani anunue pafyumu ya chibu 105,000? yaani haitakiwi izidi elf 20 hyo parfume . soko lake ni la raia wa kawaida watu wenye hela zao hawatanunua kamwe.kachemsha sana
Utajiskiaje siku upo mbele ya kadamnasi halafu unakuta watu kama 20 mnanukia harufu moja?
 
Hivi ile clothing line yake aliyoanzisha ya WCB inafanyaje sokoni?

Kama ile ameshindwa hivi kweli perfume nani atanunua kwa hiyo bei? Exposure yote aliyonayo pamoja na kwenda ulaya kila siku bado hajui apart from mziki nini kitampatia pesa matokeo yake yeye kila siku kujaribu jaribu tu mambo.. Mara App sijui ya kuuza mziki, huko hajafanikiwa karukia perfume..

Diamond una jina kubwa sana, clothing line sijui maperfume havijawahi kumtoa msanii yeyote mkubwa hata huko duniani. Tafuta biashara ambayo inagusa matumizi ya watu ya siku kwa siku.. Angalia biashara wanazofanya akina Mo na Bakhressa.. Ushauri tu ebu jaribu hata kutengeneza kinywaji chako, iwe Juice au Soda kama za Azam au Mo hapo utatoboa mara moja maana mashabiki wako wengi ni wanafunzi na watoto wa uswazi ambao hawana kipato kikubwa ukilinganisha na hizo bei unazoweka kwenye bidhaa zako.. Na hata biashara ya Juice mteja mmoja anaweza akawa anakunywa Juice yako angalau mara tatu kwa wiki lakini hizo Perfume na nguo anaweza purchase once in a lifetime.. Akina Pdidy na 50 Cent wao wanatajirikia kwenye liquor sasa wewe si mnywaji basi fanya hata Juice hizo au hata Non-Alcoholic drinks..

Demu wako Wema alikuja na biashara gani sijui lakini pamoja na mvuto wake kwa mashabiki wake alifeli, kuwa tofauti usifate mkumbo na usifanye biashara za sifa (kwamba perfume yangu inauzwa ghali).. Hujafikia level za kutengeneza prestigious products maana mashabiki wako ni watu wa hali ya chini..
Umemaliza.
sumbai Iceman 3D hebu mkuje niwanuse au hamjanunua?
 
Sanaa yetu bado ina safari ndefu, almasi (Diamond) yetu imeva attire yq ki naijeria na hereni ( ya almasi siju?).

Angezindua ubani, utuli na marashi yangeuza zaidi.....
 
ha ha ha..namkumbuka mwalimu wangu wa marketing alitufundisha akasema unapoingia dukani ukasoma price tag au ukatajiwa bei ya bidhaa fulani ukajikuta moyoni unalalamika kuwa bei ni ghali ujue hapo si mahali pako,...ondoka katafute kile unachokimudu..naishi kwa hiyo kanuni hadi leo...
 
Usawa huu wa magu mbona kazi anayo

Kama target yake ni soko upande wa kina mama anaweza kupumua kidogo, sidhani kama wanaume wanaweza kupitia trouble zote za kutoa misimbazi 10+ kua na perfume Lina jina chibu
Mimi hiyo hata bure sichukui msiniulize kwa nini.!
 
Kweli maisha magumu kitu cha $48 watu wanalalamika kuna sehemu ukienda hapa DSM hata shati zuri hupati kwa dola 48 cha msingi ni kuangalia ubora wake ukoje na kama ni wa dubai lazima itakuwa katika kiwango cha juu...yeye hajatarget watu wa instagram/facebook wengi wao ni jobless hawana faida yeyote zaidi ya kupiga blah blah tu mungu amsaidie dogo azidi kufika mbali kwenye kazi zake.
 
Kusema kweli chibu na mkubali sana lkn perfume duu, hebu fikiria kidogo kupunguza. Ila sitoshangaa, zikifanya vizuri sokoni kwani kila mtu na mfuko wake, so usiseme watu hawana ela, sema mimi sina ela, Kuna watu watazinunua tu.
Bora alivyofanya hivyo bila hivyo huoo mtaani kila mtu akipita mnanukia harufu moja
 
Japo na kaushabiki kwa mbaliiii nakaona ila umetoa bonge moja la point....unajua huyu jamaa angeamua ata kutengeneza ata madaftar tu ya wanafunzi akabandika picha yake angeuza sana coz almost kwa wasanii wa bongo domo anakubalika sana na watt wa kitaani kuanzia primary mpk secondary....siyo izo perfume tena za ghali kiasi icho 100k tsh hahahabaaaa nafwaaaaaaz
Mkuu kama mtu mtupiaji na unajijali hiyo laki na elfu tano ni ndogo sana labda uwe na pesa za kuunga unga

Pia kitendo cha kuuza kwa bei ya chini huko mtaani pasingekarika hata mabeki tatu wangenukia harufu moja na mabosi zao.
 
Kwani hakuna size ya vichupa vidogo (vile vya jerojero gulioni)
Na je hawauzi ya kupima au ya paketi ndogo kama viroba.?
Ahghh..! Kumbe mmesema perfume mie nlikuwa sijaelewa vizuri!
 
Huyu nae sifa zitakuja zimfilisi abakie historia tu.....kipindi shigongo anamdisi kuhusu gharama za show nilimuona kama hater kumbe alikuwa sahihi......toa bidhaa ambayo hata shabiki yako wa kawaida ataimudu....ingekuwa za buku ten au angalau twenty iv tungejichanga.....akanunue mwenyewe na wasafi wenzio.
[emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
ha ha ha..namkumbuka mwalimu wangu wa marketing alitufundisha akasema unapoingia dukani ukasoma price tag au ukatajiwa bei ya bidhaa fulani ukajikuta moyoni unalalamika kuwa bei ni ghali ujue hapo si mahali pako,...ondoka katafute kile unachokimudu..naishi kwa hiyo kanuni hadi leo...
True mkuu.. Unakuta mtu analalama kuhusu bei huko ni kutaka kulazimisha maisha amabayo si ya saizi yake..Kama huna hela akatafute vya saizi yake. KWa tunaojua pafyumu laki moja mbona ya kawaida sana. Mbona tunalipia pafyumu za watu wa nje hela hizo kwa nini tusisapoti vya kwetu. Anayeshangaa pafyumu ya laki ina maana hiyo si ya saizi yake. Awachie wenye saizi zao😀😀😀
 
Back
Top Bottom