Diamond "Clouds wamshindwa Fiesta"

Diamond "Clouds wamshindwa Fiesta"

Ngonepi

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2013
Posts
1,872
Reaction score
1,207
Wakati wasanii wakibongo kwa ujumla wao wakihangaika na shoo za Fiesta msimu huu, Diamond ameendelea kujidhihilisha kwamba ni msaanii mkubwa sana kiasi cha jamaa wa Clouds Entertainments kushidwa kumtumia vilivyo mwaka huu kwenye show zao!

Ieleweke kwamba kipindi hiki huwa ni cha neema kwa wasanii nyumbani ambao wengine hufikia kuomba angalau tu wapate fursa japo tu ya kupanda jukwaani kuonana na mashabiki.

Diamond kwa kipindi kirefu sasa amekuwa ni msanii wa Tanzania mwenye show nyingi sana nje ya nchi kiasi kwamba imeshindikana kumbakisha hapa nyumbani kushiriki show za hapa.

Pamoja na upizani mkubwa mno naoupata kijana ameendelea kukomaa na kujenga heshima hata kwa wale ambao bado walikuwa wabishi kumkubali Diamond.

Tunachoweza kusema kwa sasa ni kumtakia mafanikio mema na aendelee kufanya haya mapinduzi makubwa kabisa kimuziki wa Tanzania. Keep it up Diamond.
 
Humsaidii Diamond kwa kupost upuuzi kama huu, Diamond is more than this akihitaji promo zipo kampuni profesional kwa kazi hizo.

Nyinyi ndio wabaya wa Diamond na wala Diamond hawahitaji msidhani yeye anapenda utokee zuzu kama wewe uanzishe thread ya kipumbavu halafu atukanwe Diamond.
 
Mkuu leo utakuwa una stress si bure Maana kila uzi niliona umetoa comment ni kubwatuka tu hata pasipo stahili.Pole lakini,usiwe serious sana na haya maisha utapata vidonda vya tumbo
 
Kuna mjingamjinga jana kaanzisha uzi hapa eti Fiesta inawalipa wasanii haizidi laki 5.

Nikamtolea uvivu kuwa wasanii wanaingia mikataba kutokana na ukubwa wa majina yao na nyimbo zao. Diamond hawezi kula mpunga sawa na Young killer au Ommy D akala sawa na Jokate huo nio ukweli. Habari za kulipwa laki 5 watakua wanalipwa ma underground au wasanii waliofulia kama akina Juma nature.

Ndio maana Diamond wamemtumia Show moja tu ya ufunguzi Mwanza. Na si fiesta tu hata kill wamechemka kwa Dangote.
 
Sijawahi kufikiri hii makitu "Ukiwa sirias sana na maisha haya unaweza kupata vidonda vya tumbo!!"
Mkuu Matola naona anatumia nguvu kubwa hata pasipostahili, anaua mende kwa nyundo badala ya kutumia ufagio tu!! Pole Matola ndio maisha!!
 
Last edited by a moderator:
Duh eti mawingu wanamshindwa Diamond??inawezekana vipi kinyago walichokichonga wenyewe leo kiwatishe?
Spidi ya jeneza wanachagua waliolibeba sio maiti mkuu....!
duh! mkuu maneno yako balaa
 
Kuna mjingamjinga jana kaanzisha uzi hapa eti Fiesta inawalipa wasanii haizidi laki 5.

Nikamtolea uvivu kuwa wasanii wanaingia mikataba kutokana na ukubwa wa majina yao na nyimbo zao. Diamond hawezi kula mpunga sawa na Young killer au Ommy D akala sawa na Jokate huo nio ukweli. Habari za kulipwa laki 5 watakua wanalipwa ma underground au wasanii waliofulia kama akina Juma nature.

Ndio maana Diamond wamemtumia Show moja tu ya ufunguzi Mwanza. Na si fiesta tu hata kill wamechemka kwa Dangote.[/QUOT
Dada arola achana na mambo ya juma nature fata yako sio kila mtu anamtazamo wa mateam. yenu ya wakinamama
 
Wakati wasanii wakibongo kwa ujumla wao wakihangaika na shoo za Fiesta msimu huu, Diamond ameendelea kujidhihilisha kwamba ni msaanii mkubwa sana kiasi cha jamaa wa Clouds Entertainments kushidwa kumtumia vilivyo mwaka huu kwenye show zao!

Ieleweke kwamba kipindi hiki huwa ni cha neema kwa wasanii nyumbani ambao wengine hufikia kuomba angalau tu wapate fursa japo tu ya kupanda jukwaani kuonana na mashabiki.

Diamond kwa kipindi kirefu sasa amekuwa ni msanii wa Tanzania mwenye show nyingi sana nje ya nchi kiasi kwamba imeshindikana kumbakisha hapa nyumbani kushiriki show za hapa. Pamoja na upizani mkubwa mno naoupata kijana ameendelea kukomaa na kujenga heshima hata kwa wale ambao bado walikuwa wabishi kumkubali Diamond.
Tunachoweza kusema kwa sasa ni kumtakia mafanikio mema na aendelee kufanya haya mapinduzi makubwa kabisa kimuziki wa Tanzania. Keep it up Diamond.

- Ungefanya utafiiti kwanza nani ni the real manager wa Diamond anayempangia hizo safari na show zake zote, usingesema haya mkuu kama hujui si unauliza kwanza kwa wanaojua wakusaidie kuliko kuzusha uzushi uso na kichwa wala miguu!!

- For sure you have absolutely no clue na kinachoendelea na division of labor ya hizi fiesta sio kazi ya Clouds kuwapandisha Wasanii majukwaani kwenye Fiesta Tour ni kazi ya Serengeti jamana si muulize kwanza kabla hamajapayuka payuka na uzushi wa klijinga kama huu

Le Mutuz
 
Kuna mjingamjinga jana kaanzisha uzi hapa eti Fiesta inawalipa wasanii haizidi laki 5.

Nikamtolea uvivu kuwa wasanii wanaingia mikataba kutokana na ukubwa wa majina yao na nyimbo zao. Diamond hawezi kula mpunga sawa na Young killer au Ommy D akala sawa na Jokate huo nio ukweli. Habari za kulipwa laki 5 watakua wanalipwa ma underground au wasanii waliofulia kama akina Juma nature.

Ndio maana Diamond wamemtumia Show moja tu ya ufunguzi Mwanza. Na si fiesta tu hata kill wamechemka kwa Dangote.

My dear..diamond alipiga show kwao kigoma na ilikua ya kill music tour..ila ni hiyo 1 tu
 
Sidhani kama wameshindwa Diamond Kwa Ruge hata hata bure anafanya show Meneja wa Daimond ni Babu ila mwenye Remote Control ni Ruge
 
- Ungefanya utafiiti kwanza nani ni the real manager wa Diamond anayempangia hizo safari na show zake zote, usingesema haya mkuu kama hujui si unauliza kwanza kwa wanaojua wakusaidie kuliko kuzusha uzushi uso na kichwa wala miguu!!

- For sure you have absolutely no clue na kinachoendelea na division of labor ya hizi fiesta sio kazi ya Clouds kuwapandisha Wasanii majukwaani kwenye Fiesta Tour ni kazi ya Serengeti jamana si muulize kwanza kabla hamajapayuka payuka na uzushi wa klijinga kama huu

Le Mutuz

Nakuelewa unachotaka kusema mkuu, but haijalishi sana ni nani anayempangia show au afanye nini wapi bw. Diamond.

Kama umenielewa uzuri maana yangu ilikuwa kwamba bw mdogo sasa kibongofleva amekua sana na show za hom hasa Fiesta zimekuwa si saizi yake!
Nieleweke hapa, simaanishi Diamond yuko kwenye mashindano na Clouds kama unavyotaka kufikiri kuwa mimi nilimaanisha hivyo HAPANA!

Kwa yeyote anayemmanage dogo iwe Babu Tale, Fella au hata jamaa wa Mawingu kama unavyotuaminisha, basi watakuwa na akili nyingi! Haiwezekani Diamond akawa na mialiko mingi Ulaya na Marekani kisha wewe kama director wake ung'ang'anie kumpigisha show za Mtwara!! Wakati kuna wasanii kibao tu hapa ambao wangekidhi kuliko kutaka kwenda sokoni kununua kitunguu kwa kutumia lori aina ya Fuso!!

Viwango vya Dogo kwa sasa ni show za hela ndefu anbazo ana uwezo wa kuzipata.
Niwapongeze mameneja zake bila kujali ni Ruge au Tale kwa kumwezesha kijana kukamua kokote Duniani ikiwa ni pamoja na juhudi zake binafsi.
Kiip it ap Domo!!
 
Back
Top Bottom