Diamond hawa ndio wabongo, chukua ushauri wangu

Diamond hawa ndio wabongo, chukua ushauri wangu

Hata wakati kiba ame quite basi watu wangesema hujuma ..!
Diamond amefail ..!
 
jibu lake unaloo hebu masanja aanze kushindanishwa na mtu yeyote maarufu lazima yamkute hayo ya kuchukiwa na kuzomewaaa,kwanza huwezi kupendwa na watu wote hiyo haipooo

basi msilalamike maana kuzomewa kwake ndo kunamuongezea umaarufu...mbeya anaenda lini? Au mpaka hotel yenye hadhi yake ijengwe?
 
Hata d banj alipiga show kwao akazomewa kisa p squire. .kwahyo si lakushangaza kuzomewa ni moja ya changamoto katika mziki..hata kina chege na temba walivyotengana na juma nature ..walikua wakipanda jukwaani wanazomewa juma nature anashangiliwa..haya sasa hivi yuko wapi
 
Jamaa kaandika uzi kama gazeti sijui katumwa na tim dengue15?
 
basi msilalamike maana kuzomewa kwake ndo kunamuongezea umaarufu...mbeya anaenda lini? Au mpaka hotel yenye hadhi yake ijengwe?

sirmaatope kula gwalaA
wamepanik kinoma nomA noma noma nomaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Last edited by a moderator:
Hata d banj alipiga show kwao akazomewa kisa p squire. .kwahyo si lakushangaza kuzomewa ni moja ya changamoto katika mziki..hata kina chege na temba walivyotengana na juma nature ..walikua wakipanda jukwaani wanazomewa juma nature anashangiliwa..haya sasa hivi yuko wapi

temba na chege umenikumbusha leaders miaka km saba au nane hv walitimumiwaje kwenye jukwAAA
 
Jamaa kaandika uzi kama gazeti sijui katumwa na tim dengue15?

Hahahaaaaaa,mimi sijalimalizia linakera kama nini....gazeti kubwa maneno yaleyale....uswahili,mswahili
 
Me sio shabiki wa muziki sana wa tz lkn niliumia sana kusikia kashfa kutoka kwa diamond kwenda kwa ali kiba,,,,,, diamond ajifunze la kuongea kuhusu wasanii wenzake!!!!!!!!!!!
Mf bakhresa mbona hakashifu kuhusu wafanyabiashara wengine japo hawajafanikiwa kama yeye..
 
Hahahaaaaaa,mimi sijalimalizia linakera kama nini....gazeti kubwa maneno yaleyale....uswahili,mswahili

Unataka watu wakale polisi? Boss kanuna Insta anapigwa za uso sasa unategemea maboya kama hawa kina Matumbo wasije na Gazeti hapa JF? Wengine wapo kazini na Madam mama ubaya lazima apite humu kukaguwa kama vibaraka wao wanafanya kazi.
 
Me sio shabiki wa muziki sana wa tz lkn niliumia sana kusikia kashfa kutoka kwa diamond kwenda kwa ali kiba,,,,,, diamond ajifunze la kuongea kuhusu wasanii wenzake!!!!!!!!!!!
Mf bakhresa mbona hakashifu kuhusu wafanyabiashara wengine japo hawajafanikiwa kama yeye..

Na hii ndio sababu kuu ya kuzomewa pale leaders...watu wamekasirika kwelikweli
 
Unataka watu wakale polisi? Boss kanuna Insta anapigwa za uso sasa unategemea maboya kama hawa kina Matumbo wasije na Gazeti hapa JF? Wengine wapo kazini na Madam mama ubaya lazima apite humu kukaguwa kama vibaraka wao wanafanya kazi.

Juzi kashindwa kumwaga damu ya davido leo kaja na gazeti...zote stress tumsamehe tu
 
Kumekuwa na kelele nyingi sana kuhusu Diamond haswa kipindi hiki akionyesha mafanikio makubwa kimuziki.

Wakati yeye akipambana kupiga hatua kuna wanaopambana kuakikisha hasogei na anarudi chini.

Mimi nimejitolea kumpa ushauri wa bureeee kabisa akiwa kama mdogo wangu.

Ukiangalia kelele zote na matukio ya hivi karibuni utagundua hakuna ishu ya maana sana ya kumchukia diamond ila ni roho mbaya zetu waswahili...Diamond kafanikiwa sana kuna watu linawauma ili jambo yani inawauma inawauma ata wangepata nafasi ya kumuwekea sumu wangemlisha ..Jamani hakuna mtu mbaya dunia hii kama mswahili ndio maana mimi uwa sipendi kuwa karibu na mtu mswahilimswahili,nchi haiendelei sababu ya roho mbaya za kiswahili.

Mswahili anaweza kukuchukia ata hakikosa sababu ya kukuchukia na yote hii sababu ya roho mbaya unakuta mtu ana roho mbaya mpaka akicheka kuna taswira inatokea kama analia vile.

Tukifanya leo tafiti lazima tutakuta asilimia 98 ya waswahili either ni wachawi au wana tabia zote za kichawi.mbongo yupo tayari kuchoma nauli hapa mpaka nachingwea ili akakuroge kisa umenunua gari mpya, ukimpa challenge anunue la kwake atakwambia ye hapendi makuu ila atakuchukia wewe ulieamua kupenda vya kwako

Mbongo atakuchukia ata kwa kumzidi kuvaa vizuri, awezi kujipanga nae atoke smart kukuzidi ila atataka muwe wote wachafu... We ukitaka kumpima mswahili imani mkute anakula alafu akukaribishe msosi na wewe ukaribie utaona uso unavyombadilika na roho yake mbaya.

Mtu anaibuka uko alipoibuka anakwambia dogo ana dharau siku hizi, lakini ukitafakari vizuri hapa tafsiri ya neno dharau ni mafanikio....yaani tatizo dogo ana mafanikio siku hizi.

Wabongo tuna roho za kwa nini ndio maana hatuendelei kamwe, sijui tulitoa wapi hizi roho ama ni ule ujamaa ulituaribu au vipi ! ila kama ni ujamaa wenzetu China mbona wanatumia ujamaa kumfanyia roho mbaya mtu anayerudisha nyuma maendeleo ndio maana ukilisha watu drugs wanakunyonga.....sisi wabongo ujamaa wetu tunatumia kuwafanyia roho mbaya wanaopiga hatua mbele. Yani kwetu mtu akipiga hatua anafanya makosa.

So dogo diamond mimi nakushauri utulie ufanye mambo yako kimpango wako wavumilie tu awa waswahili, ila ishi nao kiakili sana. Jiamini fanya kazi nzuri zaidi watachoka tu na watakubali matokeo.

Watu wanatengeneza maneno kisha wanayapenyeza kwenye media ili kukuharibia, leo mtu anakuja na maneno eti umedharau hotel za mbeya ukimuuliza hizi kauli ulizitoa wapi hana cha kusema, kama umelala hotel za Kigoma utadharau vipi hotel za Mbeya? majuzi hapa umepiga show Tunduma inamaana huko sio Mbeya?

Unakuta mpaka radio zinaingia kwenye ujinga huu unamuuliza mtu swali akitoa majibu, mnayarusha majibu bila swali kisha mnasema haya maneno Diamond kayasema kwa Kiba. Yote ni kufitinisha tu.

Imefikia kipindi watu wanachukia mpaka wanazomea, lakini sio ishu mtu ashushwi kwa kuzomewa ingekuwa ni hivyo Chege na Temba wangeshapotea zamani maana walishapigwa mpaka makopo stejini enzi za Wanaume family na Halisi..Leo halisi wako wapi? Ata AY anayeheshimika sana kwa sasa ameshazomewa na kupigwa makopo enzi za East coast vs Temeke.

Pia chukua tahadhari na Kiba, Kiba wa sasa anamtumia diamond kupata kurudi kimuziki kiukweli bila Diamond hakuna Kiba kwa sasa but kuna Diamond bila Kiba...Kiba kwa sasa hawezi kusimama kwa kazi zake ila kwa jina la Diamond tu.

Tangu Kiba arudi kazi yake ni kuzunguka kwenye media kueleza ubaya wa Diamond, media zote kuanzia radio mpaka Tv amezimaliza akionyesha wewe ni mbaya.

Mimi nakushauri achana na kiba wewe concentrate na muziki wako kwanza mfanye kama haexist vile.

Hakuna ataekuwa juu milele ila hatushushani kwa style ya kampeni, nature ndio uwa inaamua. Muda wa mtu ukiisha haitaitajika nguvu yoyote hatutaanza kumuona kwenye headlines, hatutaskia nyimbo nzuri n.k nature itaamua.

Siku zote ridhki anayegawa ni Mungu tu hakuna binadamu anayeweza kunyang'anya ridhki ya mtu. Mungu ndio anajua nani ampe nini ndio maana yule anapewa sauti nzuri wewe ukapewa nyota. nyota ikiwaka sio rahisi kuizima ndio maana yote yaliyotokea watu wanazungumzia Diamond tu sio nani kafunika wala nini habari bado ni wewe .

Zidane alikuwa bonge la mchezaji lakini matangazo mengi na project za hela alizibeba Beckam ndio ridhki iyo kila mtu na yake.

Nakushauri fanya kazi kwa juhudi zote wataelewa tu, tena kwa sasa ndio uzidishe mara mia hasikuvunje mtu moyo bongo fleva bado inakuhitaji mno. na mashabiki wako wamezidi kukupenda amini usiamini.

Kuna wataokupenda ukifa kama Kanumba na Amina chifupa

kweli inasikitisha sana kuona ni namna gani watu hawapendi maendeleo ya wenzao, wanamchukia kijana wa watu bila sababu za msingi.
hoja zao za ajabu sana eti sikuhizi anadharau, kamdharau nani na kivipi, majibu yake hayana evidence.
wamesahau hata kiba baada ya kutoka kwa Rkelly kule walisema dogo siku hizi ananata na kujiskia sana kisa kafanya collabo na R kelly??? mmesahau mlimponda???

mmesahau mlimponda kuwa anabemendwa na wamama watu wazima na kusahau mziki???mmesahau???

utamskia mtu anasema kiba hana scandal, tumpe kazi shigongo aingie kazini atuletee file lake???
inshu ya yeye kuzaa na wanawake wawili tofauti?? vipi ingekua ni daimond ndio kafanya hivyo?? kwa kiba mtasema ni kawaida, kwa dai mtasema ni mchafu wa tabia.
vipi kuhusu kiba kutoka na spora, lulu na ritha ?? hizo sio scandal?? hayo hayazungumzwi, mmekaa kumuhesabia daimond wanawake, mbona wa kiba hamuwahesabu???

mnakuja na msemo wa eti kiba hapendi showoff, nini maana ya huu msemo?? zote hizi ni chuki tuu, na kukosa uzalendo.
soo sad kwa kweli
 
hivi kwa nini masanja mkandamizaji hachukiwi, maana gari anayoendesha ni sawa na hizo bmw za diamond na wema plus ile murrano, hata kihela yuko vizuri zaidi

masanja hapa kafikaje?? has nothing in common na daimond neither kiba, na kumbuka watu walianza kumpigia kelele kiba arudi kwa kumtaja daimond na si mwingine yoyote.
madai yakiwa kiba unakubalije kupitwa na daimond ili hali wewe ndio ulimtoa, mara rudisha heshima bongoflava haiwezi shikiliwa na daimond? na ndio kiba nae akavimba kichwa kumbe napendwa akasema nimerudi kuchukua kiti changu mara sijui kukifuta vumbi, hapo ndio ugomvi ulipolipuka.
hivyo usitake kumtafutia daimond sababu, sababu inajulikana ni hatua aliopiga kimziki tuuu na hakuna sababu nyingine yoyote ya msingi wala ya secondari hapa
 
Back
Top Bottom