Diamond: Ikitokea nimekufa kesho, nusu ya mali zangu apewe mama yangu mzazi

Diamond: Ikitokea nimekufa kesho, nusu ya mali zangu apewe mama yangu mzazi

Sijui kwa case ya Mondi hapo juu kuhusu Baba, lakini hebu tukumbushane nafasi ya Baba.

Lazima tukumbuke kuwa maamuzi "sahihi" ya Baba kumchagua Mamayo ndio yaliyopelekea wewe uliyepo leo ukazaliwa.

Huenda baadhi ya Wakina Baba wanaharibu sana baada ya kuzaliwa kwa Mtoto, lakini tujiulize vipi kama angebadili maamuzi kabla hujazaliwa?

Kama angeahirisha wakati huo na kumfuata Mwanamke mwingine basi usingezaliwa wewe angezaliwa mwingine...na kule kwingine kwa Mama mwingine ambapo angeenda angezaliwaa Mtu mwingine, sio wewe.

Wanaume walio wengi wanajua changamoto ya kufukuzia Mwanamke, wapo wanaolala njaa ili "beibe" ashibe vizuri, Wapo wanaofanya kazi za sulubu, kama kuvunja mawe makubwa, kubeba zege ili wapate chochote wapeleke kwa "Beibe", Wapo wanaofanya kazi hatari na haramu, kwenye machimbo hatari ya madini n.k ili "beibe" apate, kuna kushinda kwenye viambaza vya nyumba usiku kuvizia beibe n.k...kwa kifupi kuna panda shuka nyingi mpaka kumpata Mwanamke kwenye himaya yako...sasa kama angekata tamaa je?

Tusihukumiwe tu kwa ya "baada" tufikiriwe pia na yale ya "kabla"
 
Hahaha siyo sheria ila kiutaratibu siyo vizuri kutangaza kwamba fulani atarithi nini na nini. Najua zamani babu zetu walikuwa wanafanya hivyo wanatangaza na hakukuwa na utaratibu wa kuandika wosia(will) enzi hizo lakini katika dunia ya sasa siyo sawa kabisa kutangaza hadharani kuwa fulani atarithi nini.
Utaratibu mzuri uliopo siku hizi ni kumtafuta wakili unayemwamini pamoja na watu wazima wawili unaowaamini kwenye ukoo au hata rafiki zako ili washuhudie (a will must be witnessed) na kuandaa wosia na kuuhifadhi kwa siri kabisa. Siku ukifa mawakili wataibuka na wosia. Siku ukifa mawakili na mashuhuda wa wosia wanaibuka na wosia tu kila kitu kinaenda sawa.

Hii tabia anayoifanya Diamond Platnumz ya kutangaza hadharani fulani atarithi nini ni hatari sana siyo kwake tu hata kwa huyo mama yake. Wazungu huwa wana msemo "No one should benefit from his own wrongs" that is a principle lakini anachokifanya Diamond kinaenda tofauti na huu msemo. Huyo mama ana vibeniteni vipi kibenteni akiamua kusuka mpango (God forbid) wa kumuua Diamond kwa sababu anajua mkewe ndiye atakayerithi mali?. Au basi ikitokea Diamond akaoa unadhani mke atakuwa anamtazamaje huyo mama akiwa anajua huyo mama ndiye mrithi wa nusu za mali za mumewe? Hivi unadhani mke wa diamond kama akioa atakuwa na bidii au hata na uchungu na Mali za diamond au ndiyo atazitumia hovyo tu maana anajua nusu ya mali zitaenda kwa mama mkwe mumewe akifariki? Au (God forbid) vipi huyo mke wa diamond mfano akioa akiamua kumfanyizia huyo mama yake?

Watu wengi hawajui lakini ukweli ni kwamba mawakili wa watu wenye pesa wamekuwa wakikumbana sana na hii kadhia. Wake wengi wa wenye pesa wamekuwa waki struggle kutaka kujua waume zao wamemwandika nani kwenye wosia. Zipo scenario mpaka mawakili wanaahidiwa penzi ili tu wataje ni nani ameandikwa kwenye urithi wa mume.

Zifuatazo ni sababu za kwanini wosia unashauriwa uwe wa siri wajuao wasizidi hata watatu.

1. Kuepuka chuki na visasi baina ya walioandikwa kwenye wosia na wasioandikwa. Watu mpaka huuana sababu ya mali. Wengine huwakodia hata majambazi wapore mali za familia ili mradi tu wapate share.

2. Kudumisha ushirikiano na upendo kutoka kwa wanafamilia wote. Kuna watu wakijua hawatarithi mali hawatakuonesha ushirikiano na wala hawatakuwa na uchungu. Mfikirie mtoto anayejua baba yake hajamweka kwenye urithi atalindaje hiyo mali isipotee?

Hata hivyo Diamond ni muislam na kwa mujibu wa Muhammedan law hairuhusiwi kugawa zaidi ya one third ya mali zako kupitia wosia (will). Hii ina maana kwamba kama unaandika wosia andika kwa mali ambazo hazizidi 1/3 na hiyo 2/3 inayobaki watagawana warithi halali kwa mujibu wa dini ya kiislamu. Kwa hiyo si sahihi kumgawia 1/2 ya mali zake mama yake.

Tukija kwa upande wa watoto alionao wote ni illegitimate (Haramu) ambao kwa mujibu wa sheria za kiislamu hawatakiwi kurithi upande wa baba wanatakiwa wakarithi kwa mama zao yaani ujombani. Kwa hiyo hapo kazi ipo Diamond afanye namna kuweka sawa hili swala mapema.
 
Ni sawa kwa Diamonds kutoa wasia huo maana kwa Dini ya kiislamu wewe ulizini na wale watoto hawana urithi ila nakuomba na wao uwaandikie
 
Hana watoto wale si wake ni wamama...!!

Siye twasema ana watoto wa nje ya ndoa
Huyo mama kazaa bila mondi?
Listen, wale ni watoto wake dunia nzima inatambua hilo. (kibailojia) kidini (watu ) wachache ndo useme sio wake.

Kama ni hivyo mnavyotaka Likija suala la matumizi kwa mtoto msimshirikishe diamond
 
Huyo mama kazaa bila mondi?
Listen, wale ni watoto wake dunia nzima inatambua hilo. (kibailojia) kidini (watu ) wachache ndo useme sio wake.

Kama ni hivyo mnavyotaka Likija suala la matumizi kwa mtoto msimshirikishe diamond
Hakuna aliyebisha na hilo kaka...dunia inajua kua wake...!!

Dini haitambui kua watoto wale ni wa kwake..daimond kidini hata asipowahudumia hapati dhambi hata moja

Ila akiwahudumia anapata thawabu maana anatoa sadaka ni kama analea mtoto asiye na baba vile au mayatima..
Hao wanaoenda kumsumbua kimalezi kwanza ktkt dini wanapata dhambi maana wanamsingizia....wakati si wake

Pili hata asipotoa hana muamana wanajua ila ndo hvyo tena wanafanya ila dini ndo inasema hvyo na haitokaa ibadilike chochote kile
 
Back
Top Bottom