Sijui kwa case ya Mondi hapo juu kuhusu Baba, lakini hebu tukumbushane nafasi ya Baba.
Lazima tukumbuke kuwa maamuzi "sahihi" ya Baba kumchagua Mamayo ndio yaliyopelekea wewe uliyepo leo ukazaliwa.
Huenda baadhi ya Wakina Baba wanaharibu sana baada ya kuzaliwa kwa Mtoto, lakini tujiulize vipi kama angebadili maamuzi kabla hujazaliwa?
Kama angeahirisha wakati huo na kumfuata Mwanamke mwingine basi usingezaliwa wewe angezaliwa mwingine...na kule kwingine kwa Mama mwingine ambapo angeenda angezaliwaa Mtu mwingine, sio wewe.
Wanaume walio wengi wanajua changamoto ya kufukuzia Mwanamke, wapo wanaolala njaa ili "beibe" ashibe vizuri, Wapo wanaofanya kazi za sulubu, kama kuvunja mawe makubwa, kubeba zege ili wapate chochote wapeleke kwa "Beibe", Wapo wanaofanya kazi hatari na haramu, kwenye machimbo hatari ya madini n.k ili "beibe" apate, kuna kushinda kwenye viambaza vya nyumba usiku kuvizia beibe n.k...kwa kifupi kuna panda shuka nyingi mpaka kumpata Mwanamke kwenye himaya yako...sasa kama angekata tamaa je?
Tusihukumiwe tu kwa ya "baada" tufikiriwe pia na yale ya "kabla"