Diamond kainuliwa na Mungu mwenyewe. Binadamu hawezi kumshusha

Diamond kainuliwa na Mungu mwenyewe. Binadamu hawezi kumshusha

giphy.gif
Umegusa hisia za watu wenye mambo ya 'timu', wengine wanakujia na cheap excuses eti ana uCCM wakati topic haihusiani na siasa nawe ni CHADEMA kindakindaki maana yake kwenye upande huo hamuendani kabisa. Mapungufu mengine wasanii wengine wanayo zaidi yake.
Kitendo cha kuinua vijana wengine mpaka wanafikia kushindanishwa naye ni yeye tu mwenye moyo huo, wasanii wengine labels zao ni kwa ajili ya kukuza images zao binafsi kwani hawawainui wasanii wao kuwafikisha kwenye mafanikio mpaka angalau wafikie uwezo wa kulinganishwa nao.
Kongole kwa analysis yako.
 
Umesoma heading? Na momi wala sina.mrengo wa dini ni nukuu tu, kama imekukera pole
wala hujanikera mkuu, heading inazungumzia kuinuliwa kwa ujumla, mfano; kama mungu kakubariki uwe genius hakuna wakulizuia hilo bila kujali utautumia vipi.
 
Umegusa hisia za watu wenye mambo ya 'timu', wengine wanakujia na cheap excuses eti ana uCCM wakati topic haihusiani na siasa nawe ni CHADEMA kindakindaki maana yake kwenye upande huo hamuendani kabisa. Mapungufu mengine wasanii wengine wanayo zaidi yake.
Kitendo cha kuinua vijana wengine mpaka wanafikia kushindanishwa naye ni yeye tu mwenye moyo huo, wasanii wengine labels zao ni kwa ajili ya kukuza images zao binafsi kwani hawawainui wasanii wao kuwafikisha kwenye mafanikio mpaka angalau wafikie uwezo wa kulinganishwa nao.
Kongole kwa analysis yako.
Heshima kwako Puncler asante sana ndio maana nikaamua kuwa mtulivu na kuwajibu kwa weledi... Kwa upande mwingine siwalaumu sana maana pengine level yao ya uelewa inaishia kimo cha mbilikimo
 
Achana na mapungufu yake, haya tumeumbiwa wote chini ya jua.. Kwakuwa sisi wa mwili wa damu na nyama si wakamilifu..

Mungu huwainua wachache kati ya kwa kila taifa, ukoo hata familia.. Huwainua kwa vipawa na vipaji mbalimbali... Na wengine baada ya kujitenga na dunia hutunukiwa karama mbalimbali za kiroho

Diamond Mungu kamtunuku kipaji cha uimbaji wa nyimbo za kidunia na kipawa cha kuweza kufanya mambo makubwa ambayo kuna mamilioni ya wasomi wameshindwa kufanya

Usimwangalie Diamond wa sasa bali mwangalie pale alipoanza kuonekana kwenye mwanzo wa msingi wa mafanikio kupitia wimbo wake wa Mbagala..Na baada ya hapo kuzindua brand yake ya WASAFI iliyoanza kama utani

Mtoto wa fukara aliyelelewa na mzazi mmoja, aliyeshindwa kusoma shule bora na pengine kushindwa kumaliza masomo yake kutokana na changamoto za karo sare nk... Mungu hujidhihiri kupitia watu kama hawa
Kumbuka ni mzazi gani ambaye hapendi mwanawe awe kama Diamond? Na ndio maana kila mzazi mwenye uwezo anajitahidi kumpatia mwanawe elimu bora ili aje kuwa fulani katika maisha...

Njia aliyopita Diamond ni ngumu, nyembamba na iliyojaa taabu na misukosuko mingi, lakini kuna sauti na nguvu ya kiroho iliyokuwa inampa hamasa kwa kila hatua aliyopitia.. Ni wengi wamepita na wanapita aliyoptia Diamond.. Wanapambana kufa na kupona, lakini kwa Mungu kila mmoja ana kipimo chake

Diamond sio wa level ya wasanii wengi kwa sasa kitaifa kikanda na hata kidunia.. Usiangalie followers wake tuu mitandaoni, na mali anazomiliki. Bali mwangalie jinsi alivyoweza kutengeneza legacy yake kwa kuwatengeneza wasanii wengine kupitia yeye mpaka wakajulikana mpaka nje ya mipaka ya Tanzania.. Ana hiki kipawa cha kumbrand mtu.

Tuna wasanii wengi na wazuri sana lakini bado hakuna mpaka sasa aliyeweza kufanya aliyofanya Mond..hata kama baadhi wameweza kujisimamia lakini kusimamia wengine wakawa kama wao wameshindwa kabisa.. Kwasasa WASAFI ni BRAND tishio kwenye hilo...!

Nitarejea[emoji1541]
[emoji1541]
Naendelea
Dunia ina wasanii wakubwa wengi, maarufu na matajiri sana waliofikia mafanikio yao kwa njia mbalimbali haramu na halali lakini Mungu akamuinua mmoja tu kati yao naye si mwingine bali ni mfalme wa pop duniani Mwendazake Michael Jackson mwafrika kwa jina la mmarekani mweusi... Ukimwengu utapita vizazi vingi kabla ya kumpata MJ mwingine

Diamond is almost there.. Japo hajafika lakini aliyoyafanya mpaka sasa anastahili kupewa heshima yake kitaifa.. Huyu ni mmojawapo ya tunu za taifa kupitia sanaa ya mziki wa kisasa.. Ni mbunifu, ni mtunzi ni muibua vipaji na mwendeleza vipaji, ni mjasiriamali na yuko very smart kwenye kazi zake..!

Action speak louder than words.. Si muongeaji sana lakini matokeo ya kazi zake yanaonekana.. Ufahari wa kununua vitu vya gharama kubwa ni kiu ya binadamu yoyote yule, lakini vilevile ni kuudhihirishia umma kwamba yeye ni above next level ...!

Ndege yake inakuja iko njiani.. Gharama za kumiliki hiki chombo si mchezo hata kama hataitumia sana Lakini tayari ameshatengeneza historia nyingine ya msanii wa kwanza Tanzania na wachache ulimwenguni kumiliki chombo Kama hicho..

Waswaheli wanasema usimwingilie aliyepewa kapewa! Mond kapewa kama wewe hujapewa mwombe sana Mungu katika ukoo wenu kama si familia basi amuinue mmoja kati yenu atengeneze legacy ya familia na ukoo... ! Chuki dhidi yake ni roho ya washindwa na kijicho..

LA Mwisho wainuliwa wengi huwa hawana maisha mengi.. Lakini kwa Mond tunaweza kumfanyia ibada mwenyezi Mungu amjaalie maisha mengi mengi[emoji1545][emoji818]
Nidhamu na kujali anachofanya
 
Kuinulia ni kuinuiliwa ni kuinuliwa u bila kujali ni falme gani imekuinua.. anaweza kuwa ameinuliwa kiMungu au na kuzimu yote ni kuinuliwa na kufanikiwa......

Kitu pekee ninachokijua hata kama umeinuika namna gani au ni upande gani ndio unakuinua ila ukianza kutumia nafasi yako kugusa taasisi za za kiMungu vibaya hapo unakosea.

Mfano kuna nyimbo mbili ambazao diamond ameligusa kanisa. na kanisa ni taasisi ya kiroho ambayo inataratibu zake na usafi wake na sherehe zake.. sasa unapotumia nyimbo za kidunia kwenye taasisi ya kiMungu tegemea matokeo baada ya mda fulani hata kama hayataonekana sasa ila lazima yatatokea...
tofauti na hapo diamond anajitahidi sana na anajituma
Thread 'Ujue ugonjwa wa Mgunda na jinsi ya kujikinga' SoC 2022 - Ujue ugonjwa wa Mgunda na jinsi ya kujikinga
 
Ni wazi kabisa Diamond hawezi kupendwa na kila mtu. Hilo ni jambo lisilowezekana kabisa
Ni wazi si kila mtu atapenda kazi zake
Ni wazi si kila mtu atapenda lifestyle yake
Ni wazi si kila mtu atapenda mafanikio yake... Lakini haya yote hayaondoi ukweli kwamba Diamond kainuliwa juu zaidi kati ya mabilion ya walimwengu

Vipawa havifanani, Kila mtu amebarikiwa chake lakini pia kwa kipimo chake kwa ukubwa wake

Unaizungumziaje JamiiForums ya Maxence Melo ..! Huyu ni kipawa kingine kwenye haya mambo ya mitandao ya kijamii... Impact yake kwa jamii nzima inajulikana mpaka nje ya Tanzania.. Lakini ana maadui pia na mchango wake haupewi kipaumbele mbele ya organs za kitaifa officially.. Hawa ndio binadamu tulionao.

Ku appreciate kipawa cha mtu ni sumu kwao
 
wala hujanikera mkuu, heading inazungumzia kuinuliwa kwa ujumla, mfano; kama mungu kakubariki uwe genius hakuna wakulizuia hilo bila kujali utautumia vipi.
Popote anapotajwa "Mungu" jua imani inahusika kwa namna moja ama nyingine, na imani yangu ndio imepelekea kuhusisha na maandiko yetu yanavyosema.
 
Mshana umekula mkataba kwa Mond et, maana hii sio desturi yako kuweka mapambia na sifa za wasafi
 
Na ni kweli, kuna matukio yanadhihirisha anachosema mkuu Mshana. Mojawapo ambalo huwa napenda kuliwazia ni pale marehemu Ruge alivyojaribu kumzima Diamond, hakuweza kufanikiwa hata kidogo na hila zake ovu, marehemu inasemekana aliweza kuwazima wasanii wengi tuu pale ambako aliona hapati ulaji wake. Huwa nawaza kama angekuwa msanii mwingine sijui kama angetoboa.
 
Nashangaa mbona Kanumba katika kipindi Cha uhai wake hakufunguliwa Uzi mzuri Kama huu wa Monday Hapa jf.

R. I .P Kanumba
Naamini hakuna anayekatazwa au aliyewahi kukatazwa kufungua uzi kwa ajili ya Kanumba, mafanikio, karama na kuwafikisha vijana wengine kwenye mafanikio vilivyoainishwa na mleta uzi Kanumba hakufika mafanikio hayo hata chembe. He was a big star/a good actor for sure lakini anayezungumziwa na mleta mada ni big star hata nje ya mipaka ya Tz.
 
comment za namna hii hunichekesha sana, hua nahisi wanaozitoa hawapo serious wanatania tu.

Mungu ni mfano wa fikra, fikra hazionekani bt hudhihiri ktk picha ya vitendo, mfano fikra hazionekani bt hutusaidia kuunda vifaa tiba ajili ya kuona magonjwa mbali mbali yasoonekana kwa macho ya mwili, hivo kitu kisichoonekana kwa macho ya mwili, haimaanishi kua haki-exist.
Kwa hivyo nikifikiria kuwa pembetatu duara ipo, hilo linamaanisha pembetatu duara ipo?

Nikikwambia uongo wowote, kwa mfano, wewe ni shetani, ukabisha, nikakwambia hilo jambo ni mfano wa fikra, halionekani, utakubali kwamba wewe ni shetani?

Unajuaje Mungu yupo na haonekani? Unajuaje hii si hadithi iliyotungwa na watu tu na Mungu kiukweli kabisa hayupo?
 
Achana na mapungufu yake, haya tumeumbiwa wote chini ya jua.. Kwakuwa sisi wa mwili wa damu na nyama si wakamilifu.

HAPA UMEANZA MKUTAKATISHA, NI KWELI KILA BINADAMU ANAMAKOSA YAKE.
HUYU MTU NI WAKALA (UNAJUA VIZURI), NA NDIO MAANA KAKUMBATIA MASHOGA KWENYE LEBO YAKE.

MASHOGA+MUSIC+MEDIA=?
 
Back
Top Bottom