Baada ya sokosoko kuu la kwanini?? muda wote huu kijana
Nassib Abdul Diamond Platnumz pamoja na list yake
ndeeeefu ya mabinti wa bongomovies aliowahi kutembea
nao hajawahi kuwa hata na mtoto wa kusingiziwa,
HATIMAYE jana kupitia kwenye nyezo za kiteknolojia
tumeweza kudokezwa juu ya ujauzito alionao mwanadada
ZARI ambao ni fika utakuwa wa kijana huyu anayetamba
na wimbo wa Nitampata wapi ambao wachunguziwa
mambo wanadai ETi ni dedication kwa mpenzi wake
maarufu wa zamani.
USHAHIDI WA UJAUZITO HUO
Usiku wa jana, Dimaond aliweka ujumbe unaosema I can
not wait to have you on my hands
#Chibu_Junior
akimaanisha siwezi kusubiri kukuweka kwenye
mikono yangu
#Chibu_Junior huku akiambatanisha
na picha ya Ultra sound aliyoupiga na Zari (Kama hujui
Ultra sound ni nini Tafadhali google) na baadaye Zari naye
akapost picha yake akichukuliwa vipimo hivyo bila
kuandika kitu chochote na kuwaacha wananchi
wakimwagika na comment za kutosha kuhusu picha hizo
ambazo fika zinaonesha wawil hao wanaweza kujaliwa
mtoto mwaka huu
Je unafikiri hii inaweza kuwa Project nyingine au ni kweli
wawili hawa wanatarajiwa kuwa wazazi?? Tupe maoni yako