Diamond kupiga shoo ya bei ghali zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Muziki wa Tanzania

Diamond kupiga shoo ya bei ghali zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Muziki wa Tanzania

el nino

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2013
Posts
4,712
Reaction score
5,058
Katika kile kinachoonyesha kwa wasanii wa bongo kuanza kujitambua na kutumia brand zao vizuri katika kujipatia kipato, Msanii kinara katika muziki wa Tanzania ambaye haishi kutajwa katika vinywa vya watanzania "Dimond platnumz" atapiga shoo ya bei ghali zaidi kuwahi kutokea(msaniiwa ndani) tangia Tanzania iumbwe maeneo ya Mlimani city.

Imefahamika kuwa wahuni wa zomeazomea waliotamba maeneo ya pale leaders hawatoweza kuhudhuria kwa kuwa bosi wao aliyewakodisha atashindwa kulipa viingilio ambavyo ni kati ya 50000 mpaka 70000 per kichwa.

Kitendo cha Dimond kupiga shoo za bei ghali kimewaamsha wasanii wengine ambao walikuwa hawatambui ukubwa wa brand zao hivyo basi na wao kuanza kudai hela nyingi katika shoo wanazopiga, ikumbukwe katika tamasha la Fiesta lililofanyika mwaka huu Dimond alipiga shoo mbili tu kutokana na mahitaji yake makubwa ya mtonyo katika shoo zake.

Dimond amebadilisha mfumo wa kinyonyaji uliokuwepo katika muziki wa Tanzania na sasa tunaona kumbe msanii wa Tanzania anaweza kutoa video nzuri, kumbe msanii wa Tanzania anaweza kujaza ukumbi kwa malipo ya shilingi 50000 kwa kichwa na yeye kunufaika na kazi zake.

Kabla ya Dimond walikuwepo wengi ila walikuwa hawafaidiki na kazi zao , kama Tanzania tukiwapata wakina Dimond hata wanne basi tasnia yetu itafika mbali, tuacheni majungu na wivu kwa shujaa wa muziki wetu ila tutengeneze mazingira mazuri ya kuwapata watu wengine kama Dimond.
 
aisee kazi ipo ndgu yangu !!!
we lala kwanza amka andika thread vizuri
km unashindana na mtu!
 
Katika kujipa promo sitoshangaa mameneja wake vilaza wakamshauri kununua ticket zake mwenyewe.
 
Mi si mpenzi wa bongo-niger flava lakini naona utoto unawasumbua
 
Hiv siku zile kwa TI kiingilio kilikua shngapi vilee
 
Katika kile kinachoonyesha kwa wasanii wa bongo kuanza kujitambua na kutumia brand zao vizuri katika kujipatia kipato, Msanii kinara katika muziki wa Tanzania ambaye haishi kutajwa katika vinywa vya watanzania "Dimond platnumz" atapiga shoo ya bei ghali zaidi kuwahi kutokea(msaniiwa ndani) tangia Tanzania iumbwe maeneo ya Mlimani city.

Imefahamika kuwa wahuni wa zomeazomea waliotamba maeneo ya pale leaders hawatoweza kuhudhuria kwa kuwa bosi wao aliyewakodisha atashindwa kulipa viingilio ambavyo ni kati ya 50000 mpaka 70000 per kichwa.

Kitendo cha Dimond kupiga shoo za bei ghali kimewaamsha wasanii wengine ambao walikuwa hawatambui ukubwa wa brand zao hivyo basi na wao kuanza kudai hela nyingi katika shoo wanazopiga , ikumbukwe katika tamasha la Fiesta lililofanyika mwaka huu Dimond alipiga shoo mbili tu kutokana na mahitaji yake makubwa

mbona kama anawalazimisha mashabiki! na % kubwa ya mashabiki wake ni wale wenye vipato vya halali ya chini!
 
tutawapataje hao wanne wakati uandishi wako tu unaonyesha we ni muumini wa selikali moja na wengine wakijaribu mnasema wanamuonea wivu dadamond wenu anyway kiboko ya dadamond ninamjua hata wewe unamjua

hili ni bonge la point
yaonyesha amepaniki sana daimond anataka kurudisha heshma kwa nguvu
angetulia ajipange tu upya
humu matumbo ndo atakayeenda labda wengine hapa sijui
 
Natudia tena mods azisheni jukwaa la DAYAMONDI
 
Back
Top Bottom