Diamond kurudisha kwa jamii kwa kujenga hospitali ya Moyo Tandale

Diamond kurudisha kwa jamii kwa kujenga hospitali ya Moyo Tandale

Yatamkuta yale ya hospitali ya Mengi (Rodney Mutie) Kikavu Moshi na yule daktari wa Moyo kutoka kanda ya ziwa aliyekufa kihoro!
Masikini nafsi ya Dakitari yule. Jamani hii nchi ina mambo hii.
 
Yeye kasema anajenga hospital.. Ili awarahisishie wanainchi.. Sasa tena anasema kaongea na wadau mbali mbali wampe VIFAA...HIVI.. HOSPITAL NI VIFAA au JENGO?
Mkuu hospital ni vifaa jengo ni shelter tu bila vifaa jengo si kitu, hospital inaweza kuwa hata ndani ya Tent na ikatoa Huduma bora sana kuliko zile zenye magorofa !
 
Diamond hana pesa ya kufungua hospitali ya moyo. Ila anaweza akatumiwa kama chambo na wale jamaa wa gms
Mnajifanya kubeza hana uwezo kama mnajua gharama za kujenga hiyo hospitali, wakati huohuo mnajua uwezo na undani wa aliesema atajenga, ebu tupeni basi bajeti ya kujenga hiyo hospitali...
Kumbukeni kasema kwa kushirikiana na wadau
Hayo Maji Materu afadhali angesema kituo cha afya

Hospitali ya Moyo my foot. Anafikiri ni sawa na ku launch perfume!!!
 
Yeye kasema anajenga hospital.. Ili awarahisishie wanainchi.. Sasa tena anasema kaongea na wadau mbali mbali wampe VIFAA...HIVI.. HOSPITAL NI VIFAA au JENGO?
Jengo tupu linawezaje kuwa hospitali bila ya vifaa vya hospitali? Halafu hilo jengo linasimamaje bila ya kupata vifaa vya ujenzi
 
Kumbe chibu pafyumu zake ni mkakati wa free mason <br /><br />Yale maji ya maiti yamechanganywa na damu za paka na binadamu <br /><br />Kwa mtu atakaye tumia atakuwa ananyonywa damu bila kujua na baada ya muda ataandamwa na mikosi .
aaaaa jamani!
imekuwa tena hivyo?
 
Kuna dogo Diamond aliahidi kumlipia ada ya shule baada ya kucheza nyimbo yake vizuri ila mpaka leo wazazi wa dogo na mkuu wa shule wanalia ada haijalipwa mwaka sasa.
Mkuu, hawa wanafunzi alioahidi kuwalipia ada wapo wawili na wanasoma shule inaitwa East Africa International Academy, shule ipo ile njia ya Mwenge kuelekea Coca Cola karibu sana na ofisi za Clouds.

Diamond toka alivyotoka pale nje ya geti baada ya kuahidi kuwalipia ada hawa watoto hakurudi tena mpaka kesho..!!

Hili la Hosp Tandale napata hisia GSM wapo nyuma ya project nzima.
 
Jambo jema kila la heri itahudumia wote, matajiri wa Kikristo wakijenga nyumba za ibada hawabagui ujenga makanisa na Misikiti.
 
Yatamkuta yale ya hospitali ya Mengi (Rodney Mutie) Kikavu Moshi na yule daktari wa Moyo kutoka kanda ya ziwa aliyekufa kihoro!
Tandale kuna nafasi iliyotengwa ya kujenga Hospital? Tandale yenyewe imejaa angejenga Madale bado nafasi ipo.Hata hivyo nakupongeza Diamond ukihakikisha Wazazi na Ndugu zako wana makazi mazuri kabla ya kurudisha ulichopata kwa jamii.
 
Back
Top Bottom