Diamond kurudisha kwa jamii kwa kujenga hospitali ya Moyo Tandale

Diamond kurudisha kwa jamii kwa kujenga hospitali ya Moyo Tandale

Mnaobisha bisha na kudis anachjaribu kufanya ndo mliosomeshwa na wazaz wenu hamjawanunulia hata vitenge na mashati wazazi wenu...
Kisichowezekana nn hata akina JK wamemaliza uraisi wanafungua foundation zao lkn kunakuwa kuna sponsors wanawezesha kwa asilimia flan,..
Punguzeni majungu,roho mbaya,fitina,choyo,uchawi,wivu,maana akishindwa diamond sio kwamba ninyi mtaweza????

Binafsi....hongera sana brother diamond!! kila la kheri japo ningeomba ukajenge huko vijijini ambako huduma hata ya dispensary zimekuwa shida,

binafsi hapa dar naona hospitali ni nyingi sana ni mda hata wenzetu mikoani wawe na na huduma nyingi za afya kama hapa dar es salaam.

other wise tunashukuru sana coz, ungeweza kufanyia kazi nyingine hizo pesa lakini umekuwa chambo kwa ajili ya kurudisha shukrani zako kwa watanzania wenzako..

Mkuu, hawa wanafunzi alioahidi kuwalipia ada wapo wawili na wanasoma shule inaitwa East Africa International Academy, shule ipo ile njia ya Mwenge kuelekea Coca Cola karibu sana na ofisi za Clouds.

Diamond toka alivyotoka pale nje ya geti baada ya kuahidi kuwalipia ada hawa watoto hakurudi tena mpaka kesho..!!

Hili la Hosp Tandale napata hisia GSM wapo nyuma ya project nzima.
Muongo mkubwa wewe!!unadanganya bila hata haya!!wale watoto wanasoma mpaka leo na Diamond anawalipia Ada,hizo habari alizizusha shigongo na baadae akakanusha mwenyewe shigongo na kusema habari haikuwa na ukweli

Kwanini unaongea uongo?!unataka sifa au?!

UKITAKA KUJUA HIKI NI KICHWA HEBU TAZAMA KINAVYOPASUA ANGA LA MUSIC

Acheni kuharibu biashara ya watu,
Kama hupendi si upite pembeni.
Biashata zikistawi ndugu zako nao hupata humo humo .
Kumbe chibu pafyumu zake ni mkakati wa free mason

Yale maji ya maiti yamechanganywa na damu za paka na binadamu

Kwa mtu atakaye tumia atakuwa ananyonywa damu bila kujua na baada ya muda ataandamwa na mikosi .

Katika harakati za kurudisha kwa jamii kile anachokipata, mkali wa wimbo ‘Marry You’, Diamond Platnumz, ameweka wazi mpango wake wa kujenga hospitali ya moyo na magonjwa mengine katika mtaa aliozaliwa, Tandale Jijini Dar es salaam.

Muimbaji alisema tayari amefanya mazungumzo na wadau mbalimbali na wamemuahidi kumpatia vifaa kwa ajili ya hospitali hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii wakati akizindua perfume yake mpya ‘CHBU’, Diamond alisema hospitali hiyo itawasaidia Watanzania wa hali ya chini.

“Mafanikio yote tunayopata hatusahau kurudisha kwa jamii kile tunachokipata,” alisema Diamond. “Ukiachana na misikiti ambayo nimekuwa nikiijenga katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania habari nje kwa ndugu zangu wa Tandale ni kwamba nataka kuwajengea hospitali ambayo itakuwa inatoa huduma pale kwa bei nafuu,”

Aliongeza, “Kuna wadau wangu wanakaa nje, nimezungumza nao wameniambia nijenge tu nay wao kuna baadhi ya vifaa wataleta. Kwa hiyo nikaona hii ni fursa na tayari kuna baadhi ya mambo ya mwanzo tumeanza kuyashughulikia. Nataka ufike muda watu waache kwenda kusafiri nje kutibiwa magonjwa mbalimbali kama moyo na mengine ambayo yamekuwa akitufanya tusafiri nje kwa ajili ya matibabu,”

Chanzo: Bongo5
Masharti ya free mason

Huyu kafanya kweli research!! Ataweza kulipa hata madaktari kila mwisho wa mwezi? Tuweke macho

Mjita
Kumbe chibu pafyumu zake ni mkakati wa free mason

Yale maji ya maiti yamechanganywa na damu za paka na binadamu

Kwa mtu atakaye tumia atakuwa ananyonywa damu bila kujua na baada ya muda ataandamwa na mikosi .
gani mbea km ww.una ushahidi?

Ali Kiba ashajenga hospitali za moyo kibao sema hapendi show off tu.

Kumbe chibu pafyumu zake ni mkakati wa free mason

Yale maji ya maiti yamechanganywa na damu za paka na binadamu

Kwa mtu atakaye tumia atakuwa ananyonywa damu bila kujua na baada ya muda ataandamwa na mikosi .
duh! panapofuka moshi pana moto

Hadi leo pesa hazijafika msiwe mnatoa ahadi z uongo
Hebu toa uthibitisho.Jamani hivyo vimilioni vichache ni nini kwa Diamond VS reputation yake? Hebu msiwe wazushi kiasi hicho kisa ninini? Chuki? Wivu? Au??? Hebu weka wazi!

Back
Top Bottom