Niemekuelewa sana na mimi na ndio maana nikakueleza kwamba MAJORITY ya wale unaowaona wanafyumu kwenye mitandao tangia hapo sio mashabiki wake bali ni mashabiki wa Kiba waliokuwa wame-take advantage ya Diamond kupanda jukwaani pale Jangwani na hivyo na wao kujifanya watu wa UKAWA!
Chakaza wewe sio mfuasi sana wa hili jamvi ukilinganisha na jamvi la siasa unless kama unatumia ID nyingine kuingia hili jukwaa! Binafsi, naingia majukwaa yote mawili kwa rate ile ile but usiulize mbona hujawahi nione... itoshe tu kushangaa niliposema "I know you're smart" wakati si ajabu ID yangu kwako ni ngeni! Wakati Diamond alivyopanda jukwaani pale Jangwanil hili jukwaa la celebrities lililkuwa halikaliki toka kwa watu waliokuwa wanajifanya wafuasi wa UKAWA lakini ajabu majority ya hao waliokuwa wanajifanya UKAWA damdam walikuwa wanampongeza Ali Kiba kwa kutopanda jukwaani! Sie wengine from the very same days tukasema suala la Kiba kutopanda jukwaani is just a matter of time... na kweli, it didn't last long Ali Kiba akapanda jukwaani Mtwara! Inaelekea walidhani anatania... haikupita muda, akapanda tena jukwaani Morogoro! Hoja ya Kiba kutopanda jukwaani ikafa na ikabaki Diamond ku-post picha za CCM instagram! Within few days, Kiba nae akaanza ku-post mapicha ya CCM kama hana akili mzuri!!! Kuanzia hapo, biashara ya Diamond na kampeni ikaisha za CCM ikafa kibudu coz' waliokua wanazileta kila leo hizo hoja ni mashabiki wa Ali Kiba lakini baada kuumbuliwa na huyo huyo "King" wakapiga kimya na matokeo yake hizo hoja zikawa zinajitokeza mara chache sana kutoka UKAWA wenyewe na sio wale waliokuwa impersonated!!!
Sisemi kwamba hao sio UKAWA per se bali ninachosema kitu ambacho walikuwa wanasukumwa sio issue ya UKAWA bali minyukano ya Team Kiba na Team Diamond na hivyo wakaamua tu kuitumia UKAWA! Na ndio maana nikasema hao watu hawana madhara coz' tangia hapo majority sio wapiga kura wala wafuasi wa Diamond!! Na hao watu hawajaanza leo wala jana kubashiri kuanguka kwa Diamond...!!!! Itoshe tu kusema wameanza kupiga ramli za kuporomoka kwa Diamond tangu Ali Kiba atoe Mwana Dar es salaam.... zaidi ya mwaka mmoja uliopita! Au labda ukitaka kunielewa, rejea matukio mawili ambayo Diamond na Ali Kiba wamepanda jukwaa moja--- kuanzia kwenye Fiesta hadi Tamasha la Tigo! Matamasha yote hayo Diamond alizomewa! Yaani maonesho yoooooooote, Diamond anaonekana safi lakini akipanda jukwaa moja na Kiba ndo aonekane hafai na anastahili kuzomewa!!! Na ndio hao hao leo hii wanaojifanya UKAWA--- inaelekea walikula yamini/kiapo kuhakikisha wanamuaharibia kila mahali! Lakini kwavile kiapo chenyewe ni cha kishetani, ndio maana mara zote ramli zao zimeshindwa!