Diamond kwa nyimbo hizi mbili mpya: Hata ukistaafu Mziki leo sina cha kukudai Kamanda, hebu sikiliza na wewe.

Diamond kwa nyimbo hizi mbili mpya: Hata ukistaafu Mziki leo sina cha kukudai Kamanda, hebu sikiliza na wewe.

inapendeza, yaonyesha katoa frustration zake kwenye hizo nyimbo....
 
Naona bado sana......kwa maoni yangu hizo mbili hazifikii hata nusu ya record hits zake za awali yeye mwenyewe! Sorry.
Mara yako ya mwisho ni lini kuona Diamond anatanguliza audio badala ya video?!

Anyway, ngoma za aina hii zinakuja kama kifungua kinywa au "starter" tayari kwa main dish au pale uletwaji wa main dish unaposogezwa mbele! Na ni nyimbo ambazo zinakuwa hazipo kwenye ratiba... so long as mtu ana studio na anaweza ku-record muda wowote akitaka, basi anarekodi na kuziachia!!!

Na ndio maana unakuta amezi-post tu Youtube bila kuzifanyia promo yoyote kama ilivyo kawaida yake!!! So, kama zingekuwa ni sehemu ya hits zake anazozitegemea, asingezitoa kwa staili hii!!
 
Mkuu mbona nyimbo zenyewe mbovu?!

Unaanzaje kumsifia mwanaume mwenzio anaelia lia na mapenzi kama mtoto wa kike?!
 
Nyimbo zake saiv kwa nini hazipigwi tena radioni au ana bifu nao
 
Mamaaaee hilo song niache ni bonge la kitu, wimbo haswaa, diamond anajua sanaaaa.
 
Jana nimesafiri toka Mwanza mpaka kahama masaa manne...kwenye earphone zangu ni nyimbo mbili tu zinajirudia....sikomiiii,niache.....sikomiii,niache....safari ilikuwa fupi sana kwangu
 
Katoa audio tu, inatrend YouTube kwa kushika namba moja na haina hata, siku tatu je akitoa video?
 
Mkuu mbona nyimbo zenyewe mbovu?!

Unaanzaje kumsifia mwanaume mwenzio anaelia lia na mapenzi kama mtoto wa kike?!


Biblia au Msaafu upi unaokataza kumsifia mwanaume mwenzako..
 
hizi nyimbo ziache km zilivyo sikomi kuzisikiliza japo zinanikumbusha machungu
 
Diamond anajitahidi saana anastahili sifa.....

Hallelujah ni track kubwa saana.
 
Back
Top Bottom