Diamond: Manara ana mchango mkubwa kwenye mpira, tukiendekeza chuki za mtu mmoja mmoja ni kudidimiza mpira. Aiomba Serikali imfungulie

Hatumuombi msomari bali tunaiomba serikali imfungulie ,si unakumbuka serikali ilivyomaliza sakata la Fei toto? Msomari ana chuki binafsi na manara.
Msomari ndiyo kitu gani mbona hueleweki? Mwiba hutolewa pale pale ulipoingilia,mamlaka iliyomfungia ndiyo inayoweza kumfungulia. Alipewa ushauri wa kukata rufaa akadharau,hivyo mamlaka ya juu haiwezi kuingilia shauri hilo bila kupelekewa rufaa. After all Haji Manara mwenyewe ameshaamua kuendelea na maisha mengine nyie wengine ni kama mnaleta uchochezi tu.
 
Kwani yeye ni nani asiambiwe ukweli? Msomali amejiwekea kinga kuliko Rais wa nchi, SHAME ON KARIA!
Haji alitakiwa akate rufaa mamlaka ya juu akakataa sasa mnapiga kelele za nini,Haji Manara mwenyewe ameshaamua kuendelea na maisha mengine.
 
"Ana mchango mkubwa kwenye mpira"

Hivi soka la Tanzania limekuwa kwasababu ya mdomo au sababu ya investors?
Manara katengeneza sana fan base ya simba, kupitia mashabiki ndio wawekezaji wanavutika

Remember War In Dar, Do or Die, Kwa mkapa hatoki mtu...n.k. zote ni kauli zilizoanzishwa na manara Kwa target ya kuinua ari ya mashabiki Simba

Kaipa hadhi idara ya usemaji yeye na Jerry Muro. Maneno yake yalifanya hata watoto wadogo waipende na kiikubali simba na upande wa pili waongeze bidii ya kupambana na simba na hapo ndio mchango wake unaonekana.
 
Huyo Manara hata Serikali haiwezi kumuokoa hapo alipo atulie amalize adhabu yake na tunajiandaa kumshtaki upya kwa maana hajatumikia adhabu yake kwa 100% amekiuka vitu vingi na ushahidi tunao
Baada ya hii miwili tunampiga miwili mingine ndio atajua nguvu ya mamlaka
 
Huyu Diamond bora angepiga kimya tu anaongea vitu hata havijui,ushawishi wake huko huko..
 
We ni nani??
Au mke wa Karia
 
Trash
 
Sikatai nafasi ya msemaji kwenye uhamasishaji lakini uhamasishaji huo hauna nguvu kama timu inafanya vibaya au timu haina mashabiki

Hizo war in dar ni slogan tu zinazojaza mashabiki kutokana na mwenendo mzuri wa timu wala usione kama ni mdomo wa Manara.

Nakupa mfano

Game za Simba za hivi karibuni umeona uchache wa mashabiki uwanjani unafikiri sababu ilikuwa ni kukosekana kwa promo?

Unahisi Manara angekuwepo angeweza kubadilisha chochote kuwavuta mashabiki waliotia mgomo?

Jibu ni hapana.

Nakubali kuwa Manara kafanya mazuri ila sio katika kuinua mpira, mpira hauinuliwi kwa mdomo ni pesa watu wanawekeza.

Je influence ya Manara inaweza kufanya kazi nje ya Simba na Yanga?

Imagine leo Manara amepewa usemaji kwenye timu ya Ihefu, ana hiyo power ya kuwafanya mashabiki wa Ihefu wawe na altitude kama ya mashabiki wa Simba na Yanga?

Kama hilo haliwezekani kwanini tuseme haya maendeleo yamesababishwa na yeye?
 
Yeye manara Soka ndio lina mchango mkubwa kwenye maisha yake. Na sio yeye ana mchango mkubwa. Ametumia vibaya nafasi zake kwa kujinufaisha mwenyewe, kujitengenezea brand yake.

Yeye ndio kapata jina kwa sababu ya soka la tanzania na sio soka la tanzania limepata jina kwa sababu yake.. muwe na adabu na akiba ya maneno
 
Kwani yeye ni nani asiambiwe ukweli? Msomali amejiwekea kinga kuliko Rais wa nchi, SHAME ON KARIA!
Huyo Manara angekuwa bado yupo alipokuwa, yaani upande wa pili, wewe na wenzio, mngetamani hata ANYONGWE kabisa!
 
Haji alitakiwa akate rufaa mamlaka ya juu akakataa sasa mnapiga kelele za nini,Haji Manara mwenyewe ameshaamua kuendelea na maisha mengine.
Mpumbavu mkubwa hatupigi kelele bali tunaeleza ukweli!
 
Huyo Manara angekuwa bado yupo alipokuwa, yaani upande wa pili, wewe na wenzio, mngetamani hata ANYONGWE kabisa!
Anyongwe kwa kutumia haki yake ya ushabiki! You are not serious!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…