Diamond: Niliwatolea nje Roc Nation ya Jay-Z

Diamond: Niliwatolea nje Roc Nation ya Jay-Z

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Diamond Platnumz alitosa kusainishwa na label inayomilikiwa na Jay Z, Roc Nation

Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, staa huyo alisema hiyo ni moja tu ya label kubwa za Marekani alizozitolea nje. “Wakati nipo BET, Roc Nation walinifuata wakitaka wanisaini,” alisema Diamond.

“Acha Roc Nation kuna baadhi ya record label nyingi sana kubwa, nyingi sana, tena hawanifuati hivi hivi, wananifuata na ofa,” aliongeza.

“Lakini kila kitu ni target, mimi siku yoyote ukisikia nimefanya kazi na label kubwa duniani, sio kuwa under record label, ila pointi yangu itakuwa kwamba kuona namna gani wanaweza kukuza muziki wangu kidunia zaidi, nitafanya kila kitu mwenyewe. Kupata collabo na msanii yeyote mimi naweza kupata sababu Kimarekani collabo sio story, hela yako, ni biashara, mtu hawezi akakupa bure mfanye nyimbo ili upate hela, ukanye show yeye anafaidika na nini?”

Kingine Diamond alisema kama ni msanii mkubwa inakuwa rahisi kupata collabo za aina hiyo.

“Nataka mtu akinisaini, nataka muziki wangu uuzike kama wanavyouza akina Jay Z, Kanye West. Sitoingia eti Diamond kaingia na record label fulani, WCB itaingia na kampuni fulani na ikiingia ni katika makubaliano ya kuuza muziki katika digital kuona ni namna gani muziki wangu utauza sehemu fulani kwa bei nzuri.”
 
@PATO8221,
Muongo bwana!!![emoji57] [emoji57] [emoji57] [emoji57]

Anadanganya km hatujui kusoma vile!

Hivi hao wenziwe kwani hawatamani kukolabo na kina jiga?

Nafasi za kuwapata mpk waje coke studio km Neyo ndo tusafirie nyota!

Uongo mtupu!
 
Binafsi naamini, tukiacha wivu na kujidharau, ukweli Diamond anashine sana, ananyota kali.. So far amafika mbali sana, na anatupeleka mbali sana.

Hivi utafananisha zama za hapo kati na hizi za kwake? Anabidii na Kazi yake, kuna kipindi alitangaza kua hafanyi kazi jukwaani bila 10mil kuna watu waliongea sana, ila leo wako wapi?

Ifike mahali tukubali kua tunazidiana, wewe ukijua mbele wenzako wanajua nyuma. Najua wengi wanabeza kwa kufikiria kua Jay Z ni Mungu flani hivi.

Kazana Diamond.. Utafika Mbali.. Hawa wa kutembea na bahasha za kaki achana nao
 
Ukiondoa Hiyo Roc Nation ya Tandale pia Hadi Kevin Hart alishangaa jamaa kuwa na View Nyingi kwenye youtube na kuwapita hadi kina Rick_rozay.

KevinView.jpg
 
Sioni ajabu kwa sababu Jay Zee ni mtu mdogo sana ukilinganisha na kina Richard Turnbull,Donald Cameroon lakini walikuja Africa na kutafuta watu wa kuwatimia katika malengo yao.Jay Zee ni mfanyabiashara na Diamond ni bidhaa kwa hiyo si kitu cha ajabu kuona Jay Zee akitaka kupata faida zaidi kupitia Almasi Platinum.Kinachomdatisha Jay Zee ni followers na Africa inakuja juu sana katika biashara ya music.Bila kusahau Illumin.....ati
 
[emoji23][emoji23][emoji23] diamond hakupaswa kuyasema hayo inamaana anahisi yeye ni mkali kuliko hao waliosign huko rocnation na Sony
Ana malengo makubwa zaidi ya hiyo Lebel so sishangai kuona akiyaheshimu malengo yake hata kama hayatatimia.Uhuru wa mtu upo ndani ya nafsi na si kwenye material shits.Wewe usiyesimamia malengo ni rahisi kuhama njia kwa sababu ya tamaa.Be concious...[emoji4]
 
Ana malengo makubwa zaidi ya hiyo Lebel so sishangai kuona akiyaheshimu malengo yake hata kama hayatatimia.Uhuru wa mtu upo ndani ya nafsi na si kwenye material shits.Wewe usiyesimamia malengo ni rahisi kuhama njia kwa sababu ya tamaa.Be concious...[emoji4]
point taken unamawazo makubwa sana bila shaka ulikua wa kwanza darasani Big appreciate

watu wanamuona j zee km mungu vile wamesahau kua hata mbuyu ulianza kama mchicha

mwacheni bwana almasi afanye yake kwanza HAPPY BIRTHDAY TO HIM
 
Huyu kijana kwa jinsi anavyo hangaika kutafuta collabo na wasanii maveterani kama neyo ili aweze kutoboa kimataifa sijui kama angekataa hilo shavu maana hiyo label kubwa ina ukaribu na wasanii wa kimataifa labda kama anatudanganya kutafuta kiki!
 
Aise wewe ni ******** dogo ...sasa ukinitukana ndo utabadilisha mawazo ama alichokisema mr diamond? Kipi ambacho kimekukera sana we masikin had unatukana watu usiowajua...mana kama umefikia hatua ya kutukana kisa thread bas una mawazo ya kimasikini sana ..jibu kwa hoja ama pinga kwa hoja ...najua kejeli zipo lakin sio matusi..nikiamua kukufatilia wewe dogo nafikir unaweza kua mfano, sijawa chokoraa ktk maisha yang so nakuonya kwa mara ya mwisho.
kaka achana nae huyu ana stress za bodi ya mkopo boom mpk octoba mwishoni
 
Back
Top Bottom