Usimpoteze jamaa kuingia bongo movie aisee.
Kutengeneza video ya nyimbo siku kadhaa sio sawa na kuandaa Movie Bora. Hapa nazungumzia movie bora sio bora Movie.
Bongo movie bado hajapatikana mtu makini anaeweza kuleta mapinduzi.
Wengi bado wanadhani actor mzuri wa kike basi awe na matako makubwa, mzuri wa sura, wa kiume awe na mwonekano mzuri, maarufu na mengineyo.
Technology, uthubutu, uhalisia bado upo chini mnooooo. Mtu anaigiza daktari lakini maskini ya Mungu hajui hata ABCs za udaktari ni nini.
Kuna mambo mengi sana na ideas nyingi sana za kuigiza ila kila siku utakuta wanaigiza daktari, boss wa kampuni, Meneja wa baa, jambazi, mkulima, Mwenyekiti wa mtaa, balozi wa nyumba kumi. Navyo hawana ideas kuhusu vitu vya KITAALAMU kuhusu hizo nafasi.
Ila kwenye ideas za kudanga, umalaya, kusalitia, huko ndo ma experts.
Sasa ulimwengu wa movie ni mpana sana.
Usimpoteze huyo jamaa.
Angalia Behind the Scene ya Movie ya TOP GUN: Maverick ya 2022 utanielewa.