Diamond Platinumz alivyomtembelea Balozi Kairuki alivaa kiholela. Muone 50 cent sasa!

Diamond ni mtu wa jalalani (Tandale) na uzuri pia alijiimba kujisifia wakati anajitafuta kwenye wimbo wake wa "Mbagala." Ni ujinga kumchukulia Diamond kama kioo cha jamii kwani bado hajitambui, yeye kwa ujinga vile anavyo ongea broken English bila kurekebishwa anajiona kafika na Watanzania walivyo wajinga nao wanaona ni ujiko kumbe mwenzao anabóronga tu. Kwa kweli inasikitisha.
 
Diamond ndio nani huko Daslam?
 
Hawa vijana wetu hawana walezi
 
Kuna mambo ya msingi kibao ya kuchambua, sasa mtu anapoielekeza akili yake kwenye maisha binafsi ya mtu mwingine, hajajichunguza yeye mwenyewe...

Hiyo inakuwa ni dalili ya wazi ya upungufu wa akili.
Amechagua cha kuchambua, hata wewe hujakatazwa. By the way, celebrity kuongelewa kwa namna yoyote wala si ajabu.
 
Kuna mambo ya msingi kibao ya kuchambua, sasa mtu anapoielekeza akili yake kwenye maisha binafsi ya mtu mwingine, hajajichunguza yeye mwenyewe...

Hiyo inakuwa ni dalili ya wazi ya upungufu wa akili.
Hili ni jukwaa la celebrities, maisha binafsi yanatoka wapi!? ukidai kuwa ni upungufu wa akili, wewe unayemkosoa, kwa nini unapoteza muda kumkosoa asiye na akili!? Huna kazi nyingine za kufanya!?
 
Chadema inahusika vipi hapa!?
 

Hapa kuna maswali ya kujiuliza ambayo yanaweza kutoa mwanga kwa baadhi ya mambo.

1. Je, kuna uvaaji rasmi unapoenda ubalozini!? Yaani hiki unaweza au hiki huwezi vaa unapoingia ubalozini au hata ukitaka kuonana na balozi!?

2. Je, hadhi ya mtu mfano Celebrity au Kiongozi inaweza kumpa haki tu ya kuvaa vyovyote apendavyo yeye anapoenda ubalozini au hata kuonana na balozi!?

3. Akienda Mtanzania mwingine ambaye hana hadhi kama ya Diamond, je ataruhusiwa kuingia Ubalozini, acha tu kumuona Balozi!?

4. Inawezekana Diamond alijiendea zake tu ubalozini kwa mambo yake binafsi na balozi ndiye akamletea shobo ya kutaka kupiga naye picha ,baada ya kujulishwa kuwa kijana wake kaja ubalozini!?

Binafsi sijawahi ingia kwenye hizi balozi zetu, kwa hiyo sijui taratibu zao. Kama hakuna mavazi rasmi , basi ni wazi Diamond yuko sahihi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…