Hodiiiiiiiiiiiiiii Tangu tuzo zigaiwe leo ndo nazinduka na hii ni kutokana na kwamba matokeo na kazi anazozifanya Daimond haviendani. nimejaribu kufikiria nini shida na kupeleleza hapa na pale nikagundua vitu vinavyomfanya Daimond ashuke sio kwamba hafanyi vizuri bali ni;
- Maneno aliyoyaongea kuhusu Kiba ambayo yalichangia adi bifu zikaanza. sio kila aliyesikia yale maneno aliyapenda wengi yaliakwaza ata ambao sio fans wa Kiba na Dai alionyesha kweli dharau na haifai ikiwa yy tayari ni kioo cha jamii.
- Kufanya kufuru na kumdhihaki ALLAH. Hii pia ni sababu ya ndugu yangu Dai kukosa mashabiki na akiendelea hivi ataua soko lake ata nje ya nchi maana kwenu usipokubalika ata nje watakutilia mashaka na tumeona mfano wa wasanii waliokuwa wanavuma ila mambo ya kijinga yakawashusha. Mungu kakujalia fedha mshukuru na zitumie vyema kuna watu ata chai hawanywi maisha yanawapiga kila siku alafu wewe unaanika kitanda cha dhahabu, nyumba ya almasi, hivi kweli ata MUNGU anafurahia icho kitendo? Hapo jua kuna na pigo la Mungu.
- Bifu na kumpuuza baba yako mzazi. milango ya baraka haiwezi kufunguka kama huwezi kumsamehe baba yako mzazi Daimond. sio wewe mwenyew ulitelekezwa ata mimi pia lakini lazma ujue wazazi wakike siku zote wanavutiaga kwao na kusema tuu mabaya yao bila kusema sababu ya kweli iliyofanya baba akae mbali. wewe Mungu amekusaidia amekuinua ni kitendo cha kusema baba nimekusamehe na sio kumdhihaki. Ungemsamehe ata mungu angependezwa na wewe na kukusimamia katika kila jambo adui shetani asikuguse kwani anaagiza ivyo adi kwenye vitabu vyake vya dini.
- Bifu na ma ex zako. Daimond yeye ni staa tayari na kila macho yapo kwake, ata kama umetembea na wanawake wachafu as long as walikufaa katika kipind ambacho una uitaji nao kwa nini uwadhalilishe? waswahili wana sema ukipata kipya cha zaman usikisahau lakin wewe ndugu yangu kutwa nzima kuwaimba na kuwatupia madongo sio vizuri na ni ushamba coz mbona kuna wasanii wengi wametembea na watu na wakaachana still bado wakawa marafiki kwa nini wewe kwako ni tofauti?
Bado una mambo za kizamani joo kwamba ukiachana na mtu msisemeshane msipigiane simu na wakati ishapita na wakati, kwa mwanamke uliyenae kama ana akili atagundua hilo maana huwezi pigiwa simu na ex wako ukaacha kupokea alafu unamtangaza una mwimba na kuendelea.
- Mwisho kabisa kwa leo ni Kauli. mimi ni fan Mkubwa sana wa Daimoond ila kijana hana kauli kabisa. bado ana maisha ya uswahili uswahili wa Tandale. Daimond wewe ni staa maneno ya kiswahili na vijembe kwa ma ex zako usiwe unaweka kwenye page yako halileti picha nzuri ata kwa watu walio nje ya nchi. mara uandike... ndimuu zitawahusu mwaka huu .. wakina nani sasa?
Mimi Kiba simpendi ata kidogo ila Dogo yule ana akili sana na kafunzwa namna ya kuishi na watu wazuri na wabaya. Kiba huwezi kukuta kwenye page yake kaandika upuuzi wa ajabu ajabu maana anajua madhara yake ya baadae. Maneno yanamcost mtu kuwa makini.
Hizo ndo sababu zilizofanya watu wamchukie Daimond na wamdharau na wahame wasiwe fans wake wakawe fans na kuwapigia kura watu ambao hawajamzidi uwezo ata kidogo na wanalijua ilo ila wanataka dai ajifunze na ajutie madhambi yake. Daimond usipojirekebisha nyota yako inayo waka itazimwa na sio na binadamu tuu adi Mwenyeezi MUNGU maana hufanyi yanao mpendeza.
Plz and plz vote for Diamond atakuja kujutia dhambi zake wenyewe. Hata maandiko yanasema tusihukumu tusije tukahukumiwa. Usimwache kijana aliyeipeperusha bendera vyema akaaibika kwa kuchukiwa.