Diamond Platinumz Fans' Special Thread: Njooni tukutane hapa

Baba ni baba tu hata kama mtoto amelewa umaarufu na mashabiki wake nao mmejisahau lakini kumbukeni hata sperm donor anayo nafasi yake kwa huyo kijana wake.

Nachukuwa fursa hii mimi kama mtani wenu ninatoa taslim Tshillings 50,000/= tu ili tuanzishe harambee ya kumsaidia pesa za kujikimu Baba mzazi wa Nasibu Billionare Dangote Platinumz kwani ana uhitaji mkubwa wa msaada na mtoto wake hana time naye amekosa kujifunza hata busara za mzee Badiba za Forgive and forget.

Naomba Team Diamond mratibu michango hii namna ya kuikusanya na mimi Cash yangu nitaikabidhi kwa uongozi wa JF.

Kiroho safi onesha uzalendo sambaza upendo siyo virusi..

Huyu ndio Baba mzazi wa Billionare Diamond Platnumz. Sharing is caring.

Cc [MENTION=40686]Mrembo by Nature atoto Diva Beyonce Ms.Lincoln
 

Attachments

  • 1434826220852.jpg
    20.4 KB · Views: 1,208
Last edited by a moderator:
umempigia kura diamond mtvmama awards? au unatafuta kiki? Matola

Alikiba alivyoibiwa vitu milioni sita alikuwa anatia huruma saaaaaana, vipi mlijikusanya kumchangia anunue vitu vya ndani? afu mpo wengi pengine hata mngepata pesa mumjengee apate hekalu lake na yeye
 
Last edited by a moderator:

Haaaaaa hata shiling kumi hajatoa.....

Mpwa ya Ngoswe muachie Ngoswe mwenyewe
 
Last edited by a moderator:
Mimi sina kitu hapa ila nahaidi ntatoa sukari kilo mbili.
 
huu uzi ni kumdhalilisha mtu ambaye wala hayupo hapa.

Sijui ni malezi gani matola umepewa na wazazi wako kiasa kwamba hueshimu wazazi wa wenzio.

Unasikitisha sana. Na walah nakwambia ningekua mode unge RIP.
 
huu uzi ni kumdhalilisha mtu ambaye wala hayupo hapa.

Sijui ni malezi gani matola umepewa na wazazi wako kiasa kwamba hueshimu wazazi wa wenzio.

Unasikitisha sana. Na walah nakwambia ningekua mode unge RIP.
data wakumuuliza swali hilo ni Diamond na siyo mimi.

BABA MZAZI WA DIAMOND PLATNUMZ ALALAMIKA KUKOSA MSAADA WA MATIBABU.


BABA wa msanii Nasibu Abdul Diamond, Abdul Juma yupo hoi akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu.


Kwa mujibu wa chanzo makini, Baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba hali ambayo imemfanya ashindwe kutembea lakini cha kushangaza mwanaye, Diamond hajaenda kumjulia hali.

Baba Diamond ni mgonjwa kwa muda mrefu sana lakini Diamond hajawahi kuja kumuona hata siku moja,-kilisema chanzo hicho.


Baada ya kuzinyaka habari hizo, waandishi -wa habari hizi walifunga safari mpaka nyumbani kwa mzee huyo, Magomeni-Kagera, jijini Dar ambapo alikiri kuugua kwa muda mrefu na kukosa msaada kutoka kwa Diamond.


Nasumbuliwa na miguu kwa muda mrefu sana na ninatibiwa katika Hospitali ya Saint Monica, Manzese-Darajani".


Diamond ana taarifa za kuumwa kwangu lakini hajawahi kuja kuniona.Namshukuru mwanangu Queen Doreen kwa kunijali kwa kila kitu, alisema baba Diamond.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…