Ndugu zangu sielewi kabisa, huyu jamaa Nasib mzee wa kick na skendo watu wamempuuza sana, anatumia gharama nyingi kutengeneza video kali lakini watanzania wanaishia kuipongeza video na sio nyimbo tena.
sasa hivi jamaa anachojivunia ni video kali na kukata mauno tu kwenye waimbaji bora hayupo kabisa, ukisikia kama ni tuzo yeye atabeba tu kipengele cha video bora ambapo kimsingi ni juhudi za director, pia utasikia kabeba tuzo ya mnenguaji bora ambapo kimsingi hata twanga pepeta hata wao wakikomaa watachukua.
Jamaa nyimbo zake zinaingia top 10 kwny tv na station zile zile tu huko nje kwa wachumia tumbo lakin huwezi kusikia hata siku 1 akishika chat hapa bongo kwanini?
Skendo sasa hamna hata kick ya kudandia hana tena, vya kupost hana maana kama ni kick ya tiffah basi kashazaliwa, kama ni wema basi mwenzake kashapata mtu wake.
Kijana hajui kick gan atokee, anajarbu kumchokonoa mfalme kiba, ila ndo hivyo kashazibwa mdomo na
#Nagharamia sasa kabakia tu kupanick insta ooh i swear sijui nikifa hahahaha
Watanzania kwanini mmempuuza Nasib?