Mkandara
Katika mambo machache ninayokubaliana na wewe ni hili la majimbo.
Najua tofauti yetu kubwa ni wewe kuwa upande wa ujamaa na mimi kupendelea ubepari ulioenda shule. Lazima tuelewe kuwa CHADEMA na sera yao ya majimbo hawawezi kuitema hata siku moja hata huyu JJ hata kama ataona haifanyi kazi lazima aitetee kwa nguvu zote.
CHADEMA kuitema sera hiyo itakuwa ni kushindwa kisiasa. Mara nyingi huwa nalalamika juu ya halmashauri za miji. Mimi nadhani kama Halmashauri za miji zikiendelezwa na kuwa na nguvu pamoja na kupewa nguzu zaidi za kiutendaji na kuwapunguzia mzigo/nguvu Ma-DC na Ma-RC.
Kama halmashauri zikiwezeshwa na kuwa na uwezo wa kuwatumikia wananchi katika maeneo yao basi mawazo ya JJ yatatekelezeka vizuri zaidi kuliko majimbo ambayo yanahatarisha utaifa. Kuna siku chache zilizopita Mh. Mzee Makamba tuliambiwa amewaagiza Halmashauri kutekeleza matakwa ya Manji. Hayo ndiyo mambo yanayoonyesha Halmashauri zetu hazina nguvu kabisa.
Hivi kama uetekelezaji wa mambo unamsubiri DC au RC au hata waziri mkuu tutaendelea kweli? Leo hii tunaambiwa kuna wizara ya polisi. Hivi kuna jambo gani la kipolisi ambalo lingeshindikana kwenye halmshauri za miji. Leo hii kutokana na uongozi mbovu tunahitaji wizara ya polisi ambayo itakuwa inashughulikia ujambazi.
Kama tungekuwa na watu wanajua nini chimbuko la ujambazi na ni sababu zipi zinasababisha ujambazi tusingekuwa tunahitaji wizara ya polisi.