Diamond Platinumz Fans' Special Thread: Njooni tukutane hapa

Diamond Platinumz Fans' Special Thread: Njooni tukutane hapa

tena huwa anajisifia kabsa kuwa anatoka tandale.angekuwa anaringa asingepata ujasiri wa kutaja kwao mara kwa mara

Wao mradi chuki zao zinawatuma kusema wanasema tuu....oooh kasema mbeya hakuna hotel yenye hadhi yake na juzi alikua iringa..
Sasa jiji na manispaa wapi kuna hotel nzuri kuliko kwingine???
 
Wao mradi chuki zao zinawatuma kusema wanasema tuu....oooh kasema mbeya hakuna hotel yenye hadhi yake na juzi alikua iringa..
Sasa jiji na manispaa wapi kuna hotel nzuri kuliko kwingine???

watu kwa kupandikiza chuki yaan mtu ana create tu maneno ili kumchafua mtoto wa mwenzie
 
watu bhana kwa kujitia nyama eti king wakati king mwenyewe duly sykes wakat anaanza mziki kibaka alikuwa kwao kariakoo anavaa raizoni na kufuta kamasi na nguo
 
Zai pokea likes milioni laki kumi na tano elfu sabini na mia tatu na nusu......
I always wanted to give them that kind of an example lakini nikaona kwa kuwa their hearts are full of hatred they won't even get my point.
Watu kama Dully Sykes walau you can dare to call them kings..
Coz toka wanaanza hawajawahi kukosea wala kushuka....na ukianza kupanga nyimbo zao na ukaanza sikiliza hata sasa bado zinakupa burudani kama uloipata wakati nyimbo zinatoka..
Msanii ambae anafata hizo nyayo ni chibu kwa sasa...
Ukianza kupanga nyimbo za chibu kuanzia kwa KAMWAMBIE mpaka NUMBER ONE,hakuna wimbo ambao Dogo kakosea....na uzuri zaidi unaona kuna maboresho ktk kila song from music to videos.
Binafsi wakati chibu anaanza nkaona hana muda mrefu baada ya mbagala.mara nkasikia ntarejea nkasema maybe ya mwisho mwisho,kustuka naskia MAWAZO(always my favourite) nkasema hatotoa tena kama mawazo,sijakaa sawa naskia lala salama mara kizai zai yaani mara kesho yaani mradi vurugu...mwenyewe nikakata tiketi ya ushabiki namba moja wa chibu.
So mm mtu akija na Sera zake za ufalme na reference akiwa alli binafsi namuona hayuko sawa.
We unasemaje wewe ? C unasema baada ya kuona Chibu anaanza ukajua hana muda mrefu?? Mi nikakumbuka ilikuwa hivi...!! Enzi hizo nilikuwa sijaacha kusoma magazeti ya Shigongo type! Sasa ilikuwa kila nikikutana na Shigongo type, nakutana na habari za mtu anayeitwa Diamond!!! Mimi nina tatizo moja... nina allergy na majina yanayovuta attention!!! Hata duka lako ukiliita SUPER kufanya nini cjui, kuna hatari nisiingie! Akili yangu inavyonituma ni kwamba u've some weaknesses ambazo unataka kuzi-cover up kwa jina tamu linalovutia huku likiwa limenyunyuziwa marashi! Kwahiyo Dogo ikawa nampotezea tu, kisa, jina la DIAMOND tu! Kama mara mbili tatu hivi nikakuta habari zake kwenye serious newspaper... nikampotezea vile vile... kisa kile kile, sikuwa na sababu za msingi... kwavile tu naona jina lake ni aina ya majina yanayovuta attention ambayo kwa tafsiri yangu ni udhaifu!

Wiki kadhaa baadae(siku chache kabla Mbagala haijakuwa released), hiyo cku nilirudi ghetto mapema! Nikiwa nimetulia nacheki EATV, mara akatokea dogo mmoja hivi ambae simfahamu! Binafsi nikiona mwanamuzi cmfahamu, nabadili channel instantly! Ile nagusa remote... naona jina DIAMOND... mi ehe, kumbe "mbwiga" mwenyewe ndo huyu! Kwa ubishi tu nikataka ku-change hivyo hivyo! Kabla cjafanya hivyo... nikavutiwa na beat ya nyimbo... nikakausha lakini kidole bado kikiwa kwenye remote tayari kwa kubadili channel sekunde yoyote akinizingua!!!

Sekunde chache baadae, dogo akaanza kuimba... mi, eh, kumbe dogo anajua! Nikataka ku-rewind chap chap, nikaona aiyaaa kumbe naangalia tv! Hili la kutaka ku-rewind watu wanaweza kudhani nanogesha lakini wenzangu waliokuwa addicted kwenye movie na series wanaweza kunielewa manake kv kwenye movie na series ni full mambo ya ku-rewind ili utamu uupate vizuri!!! Basi mazoea ya kucheza na remote kwenye series huwa tunayahamishia hadi kwenye tv programs!

Basi bwana, Nenda Kamwambie nikaisikiliza mwanzo hadi mwsiho... nikaona aaaanhaaa, kumbe ndo maana dogo kajiita Diamond ni kweli Diamond! Ikawa sasa nategeshea nimuone tena... ah wapi... sikupata tena hiyo bahati lakini siku chache baadae, nikamuona tena... mi aaaha, yule dogo si ndo huyu... kumbe ndo siku Mbagala inaoneshwa on TV stations kwa mara ya kwanza! Nikamkubali zaidi na zaidi... alipotowa Nitarejea, aaaaah... dogo ndo akamaliza kabisa! I short, simjui na hanijui... yeye anatoka Kigoma mimi natoka Lindi... mbali mbali, wala ukaribu hakuna lakini hata hivyo, kuna wakati nilikuwa nataka kumuunganisha kwenye mchongo fulani, unfortunately ukabuma... nikapiga kimya, lakini Inshallah, naamini ipo siku nitakuja kutoa mchango wangu wa aina yoyote kwake coz' chanda chema huvikwa pete! Na wala sipo Team Diamond... hayo ni mambo yenu nyie wa 1990's lakini penye ukweli lazima usemwe... dogo anajua, na more importantly, he's creative and hardworking than any musician in EA na ndo maana nashangazwa sana na mburullaz wanaosema kwamba Chibu ni mtu anayekwenda kwa kiki za kashfa lakini kila ninapowatwangwa maswali... hakuna anayejibu zaidi ya shouting! Yaani kwa makusudi wanashindwa kuona jitihada binafsi zinazofanywa na Chibu na ndio maana mie nawaita majirani wa Bwana Mcharo wanaokerwa na Bwana Mcharo kula nyama kila siku!!!

Duh! Nimeongea kweli kweli... utafikiri nipo jukwaa la siasa!!
 
Makamanda nina video ya mchina akiimba wimbo wa nitampata wapi ila nashindwa kuiupload ambaye ana acess Aseme nimrushie watsaap aje hta pm ili aje aweke kwenye jukwaa watu wapate udambwiudambwi
Dah... naitamani sana hiyo video unfortunately sipo watsapp... anyway, in short i hate any social network ambazo zinatumia simu peke yake... nimeumbwa vibaya, nina allergy sana na simu hasa linapokuja suala la ku-text kutumia simu!!

By the way, kama unatumia simu, weka hapa link ya wapi uliichoropoa hiyo video mie nitaifuata huko huko kisha nije kuimwaga hapa!!!
 
Ndo maana tumekata passport tangu mwaka 2005 bado haijajaa na tunajiandaa kwenda kurinyuu ili mradi tu!!! We Eshy m.s mjeuri....

Kwa akili yako fupi unadhani Passport ya Obama imejaa mihuri kama passport ya Profesa Kikwete?
 
Last edited by a moderator:
G'morning wadau,bila shaka jirani zetu pia wame amka salama.majukumu yanaendelea nawatakia uwajibikaji mwema na kwa wale wagonjwa na wenye matatizo mbali mbali Mungu awatie nguvu,wale walioko shule basi masomo mema.....!!
 
Kwah kwah kwah... cjui ulijuaje kwamba natoka jimbo a Mchinga wakati Lindi likuuuuuubwa... una akili wewe!!!

Me mtabiri Muheshimiwaa.....Usinisahau yakija madili ya maana kama escrow manake kushinda ushashinda unasubiri wavunje lijibunge lao uapishwee.....
 
Me mtabiri Muheshimiwaa.....Usinisahau yakija madili ya maana kama escrow manake kushinda ushashinda unasubiri wavunje lijibunge lao uapishwee.....
E bhana ee..., n'shaanza kunenepea kitandani Kim!! Wallah kama we ni mtabiri mahiri kiasi hicho, acha nishoneshe suti kabisa, naamini hata nikikuomba unipigie kampeni, hutaniangusha na fwedha za kikao cha kwanza tu, zote zako ili mradi tu usije kutoa shindano hapa la atakayefikisha page ya 100 manake Mond anajiuza mwenyewe!!!
 
E bhana ee..., n'shaanza kunenepea kitandani Kim!! Wallah kama we ni mtabiri mahiri kiasi hicho, acha nishoneshe suti kabisa, naamini hata nikikuomba unipigie kampeni, hutaniangusha na fwedha za kikao cha kwanza tu, zote zako ili mradi tu usije kutoa shindano hapa la atakayefikisha page ya 100 manake Mond anajiuza mwenyewe!!!

Kuhusu Campaign manager hapa umepata......na fedha za kikao usijali ntauza mikorosho yangu ya urithi...hahahaaa Siku hizi tuna gesi korosho sio dili......!
Siwezi kutoa Shindano wakati jimbo lako lilee.....yani ukiamka we anza kutembea kwa kujitanua kama makwapa yana jipu vilee.....Jimbo lote lako hilo.......
 
Kuhusu Campaign manager hapa umepata......na fedha za kikao usijali ntauza mikorosho yangu ya urithi...hahahaaa Siku hizi tuna gesi korosho sio dili......!
Siwezi kutoa Shindano wakati jimbo lako lilee.....yani ukiamka we anza kutembea kwa kujitanua kama makwapa yana jipu vilee.....Jimbo lote lako hilo.......
Unaona sasa... kumbe mtaji wa kuanzia ni wa kumwaga... nami napiga bei mikorosho yote... mikorosho nini bwana, wakati migesi imejaa hadi sebuleni! Yaani lazima nikutafute tuanze mikakati...
 
Topic: Diamond awapiku P square on youtube

By heaven on desert
.
Tumeshazoea kuona baadhi ya mastaa wa Afrika
wanapoweka video zao kwenye youtube
wanapata views nyingi ndani ya siku chache lakini
Good news time hii imeangukia kwa mkali wa
Tanzania.

Mmiliki wa hit single ya ‘Mdogo Mdogo’ Diamond
Platnumz ameipiku video ya wakali wa Nigeria P
Square baada ya kupata views nyingi ndani ya
siku nne.

Diamond ambaye video yake ‘Nitampata Wapi’
iliyoweka youtube november 20 ina views
419,112 ,likes 3500,dislikes 400

Huku Shekin ya P aquare iliyowekwa november
17 ina viewers
325,514

ANGALIZO:Kuna watu watakuja na kusema
tunashindana na psquare,hapana isipokuwa kwa
nia njema tuanajaribu kuonesha ni kias gani
diamond anazidi kuukuza mziki wetu ,kwamba
kama wana ijeria wanaweza hta sisi sasa
tunaweza,Ahsanteni)
 
Back
Top Bottom